tag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post1126424257773061419..comments2024-02-19T01:07:06.277-08:00Comments on Hapa Kwetu: Nimechapisha Mwongozo wa "Song of Lawino"Mbelehttp://www.blogger.com/profile/16077261126944002622noreply@blogger.comBlogger2125tag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post-22791739107945326742016-04-03T13:04:45.831-07:002016-04-03T13:04:45.831-07:00Ndugu Mhango
Shukrani kwa ujumbe. Ni kweli kuwa &...Ndugu Mhango

Shukrani kwa ujumbe. Ni kweli kuwa "Song of Lawino" ilileta mwamko mpya kote Afrika Mashariki, na sehemu zingine, kuhusu ushairi katika lugha ya ki-Ingereza. Ni utungo uliohamasisha utungaji wa mashairi wa aina mpya. Nilipokuwa nasoma Chuo Kikuu Dar es Salaam, tulifundishwa "Song of Lawino" na mwalimu Grant Kamenju (marehemu sasa), ambaye alituchangamsha akili kwa kutumia fikra za akina Karl Marx, Frantz Fanon, na wengine wa aina hiyo.

Ni muhimu kukumbuka tulikotokea katika safari ya uandishi, na ni ukweli pia "Things Fall Apart" ni utungo mwingine ambao umeathiri na kurutubisha uandishi katika Afrika. Muhimu pia kuweka katika maandishi ushahidi kuwa tulikuwepo hapa duniani, kama walivyofanya waliotutangulia, ambao wanakumbukwa na wataendelea kukumbukwa ingawa hawako hai.Mbelehttps://www.blogger.com/profile/16077261126944002622noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post-89383840821578484982016-04-03T08:01:54.014-07:002016-04-03T08:01:54.014-07:00Ndugu Mbele,
Hongera kwa kufanikisha hili la kuich...Ndugu Mbele,
Hongera kwa kufanikisha hili la kuichambua na kuichapisha Song of Lawino. Kila niendapo -pamoja na kuacha tani nyingi za vitabu vyangu -huwa siachi kuandamana na nakala za Song of Lawino na Things Fall Apart. Kwani hivi vitabu viwili ndivyo vilivyonichochea kuwa mwandishi na mshairi kama nilivyo leo. Nikiwa sekondari, pindipo niliposoma Song of Lawino, nilijikuta navutiwa kiasi cha kutamani kuandika kitabu au vitabu ya mashairi huria kama nipendavyo kuyaita. Tokana na msukumo huu, nimeishachapisha vitabu viwili yaani Born with Voice na Souls On Sale. Kitabu kingine cha Psalm of the Oppressed ktatoka hivi karibuni wakati kile cha Perpetual Search kikikaribia kuisha huku Hello John Pombe Magufuli ikiwa imeshachapishwa gazetini.
Kuhusiana na Things Fall Apart -tokana na riwaya hizi kutotumika sana -niko namalizia kitabu ambacho hata hivyo nahagaika na kukipa jina stahiki. Kwa sasa nakiita How the High and the Mighty Eat National Cake japo baadaye naweza kulifupisha au kulibadili. Sijui kama Song of Lawino bado inafundishwa mashuleni. Hata hivyo, ni ushairi mulua tena unaosomeka kirahisi.
Nakupongeza ndugu Mbele kwa mchango huu adhimu na muhimu kwenye ushairi wa kiingereza ulioandikwa kiafrika.
Kazi njema.Ndugu Nkwazi N Mhangohttps://www.blogger.com/profile/11640087613265490788noreply@blogger.com