tag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post1963257919952340315..comments2024-02-19T01:07:06.277-08:00Comments on Hapa Kwetu: Hadithi za Wa-Matengo Chuoni MontanaMbelehttp://www.blogger.com/profile/16077261126944002622noreply@blogger.comBlogger4125tag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post-13539101563087798992015-02-17T09:19:40.792-08:002015-02-17T09:19:40.792-08:00Dada Yasinta, shukrani kwa ujumbe wako. Nilijua ku...Dada Yasinta, shukrani kwa ujumbe wako. Nilijua kuwa unacho kitabu hiki, na kwamba unakipenda, kama ulivyowaeleza walimwengu katika blogu ya "Jielewe."

Kama nilivyogusia katika makala yangu, nilikiaandaa kitabu hiki kwa miaka mingi, miaka yapata 23, ili kuhakikisha kuwa kinafaa kufundishia hadi kiwango cha chuo kikuu. Nami nikiwa ni mhadhiri wa somo hili pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, nilijua ninachofanya.

Insha za maelezo nilizoweka baada ya kila hadithi, na insha niliyoweka mwishoni kujumlisha mambo muhimu ya fani hii ya hadithi za mapokeo, ni changamoto kwa taaluma sio tu kwa hadithi ya ki-Matengo, bali kwa hadithi za Afrika na ulimwengu.

Hii ndio maana kimeingia katika madarasa ya maprofesa kadhaa hapa Marekani wanaofundisha masomo kama "folklore," "fairy tales," au "mythology."

Lakini kinafaa kwa yeyote anayetaka kujua au kutafakari maana na umuhimu wa hizi hadithi za mapokeo, ambazo mara nyingi watu hawaelewi kuwa zina masuala mengi na falsafa.

Miaka 23 ya kutafiti, kutafakari na kuandika, hasa kutafakari, sio michache. Ingekuwa ni kulipwa, kwa kazi yote niliyofanya, na taabu niliyopata, ningekuwa tajiri sana.

Lakini, kwa kuandika kitabu cha aina hii, lengo lako haliwezi kuwa hela bali kuchangia elimu, na hizo pesa unazoweza kupata hazitoshi hata kugharamia utafiti, tafakari na uandishi niliofanya. Lengo ni kuchangia elimu, na ndio furaha yangu.

Ninapangia kuendelea na utafiti wa hadithi za wa-Matengo, kwa sababu lugha ninaifahamu na utamaduni wake. Hilo ni jambo muhimu sana. Nikipata hela na likizo ya utafiti, nitaenda kuendeleza utafiti huo.

Wakati nangojea fursa hiyo, ninaendelea na kufundisha na kutafakari. Kwa mfano, zao moja la tafakari niliyofanya miaka ya karibuni ni makala hii hapa.

Mbelehttps://www.blogger.com/profile/16077261126944002622noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post-22914161363897396082015-02-17T02:57:43.790-08:002015-02-17T02:57:43.790-08:00Ni kitabu chenye mafunzo mengi ninacho hapa nyumb...Ni kitabu chenye mafunzo mengi ninacho hapa nyumbani na nimekisoma . Hongera kwa hilo.Yasinta Ngonyanihttps://www.blogger.com/profile/09314172793959023532noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post-26045178502734255162015-02-16T18:54:37.510-08:002015-02-16T18:54:37.510-08:00Ndugu Anonymous, shukrani sana kwa ujumbe wako. Kw...Ndugu Anonymous, shukrani sana kwa ujumbe wako. Kwa heshima na taadhima, nitaandika maoni yangu katika blogu hii, kama unavyoelekeza, pamoja na kuelewa kwangu kuwa mawazo yangu sio bora kuliko ya wengine. Insh'Allah, nitafanya hivyo wiki hii hii.Mbelehttps://www.blogger.com/profile/16077261126944002622noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post-47019037351048025752015-02-16T04:39:10.551-08:002015-02-16T04:39:10.551-08:00Prof Mbele. Pole na kazi za kila siku.
Ningependa...Prof Mbele. Pole na kazi za kila siku.
Ningependa kujua nini maoni yako kuhusu kutumia kiswahili kama lugha kuu ya kufundishia mpaka chuo kikuu. Je unalionaje hili, unaona kutakuwa na athari zozote kutokana na elimu?. Je ni kweli tutakuwa tumejitenga na dunia?.

Ningeomba kama ungepata nafasi basi ukaliandika hili kama post katika blog na wala si comment. Nakutakia siku njemaAnonymousnoreply@blogger.com