tag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post2048419006339938006..comments2024-02-19T01:07:06.277-08:00Comments on Hapa Kwetu: Hatimaye, Nimeonana na Mzee Patrick HemingwayMbelehttp://www.blogger.com/profile/16077261126944002622noreply@blogger.comBlogger7125tag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post-88478802414468388682017-02-22T04:43:15.250-08:002017-02-22T04:43:15.250-08:00Nimekaribia Prof,maarifa kiu yangu.
Sinong'one...Nimekaribia Prof,maarifa kiu yangu.
Sinong'onezwe na hofu,ibashiriyo uchungu.
Hino kazi ashirafu,impendezayo Mungu.
Matundaye maarufu,jaza mafungu mafungu.

Mudhihiri Njonjolo.
Mtwara-Mjini.Anonymoushttps://www.blogger.com/profile/11788658319123439351noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post-244997618897019822016-07-12T22:53:17.753-07:002016-07-12T22:53:17.753-07:00Ndugu mudhihiri njonjolo,
Shukrani kwa kutembelea...Ndugu mudhihiri njonjolo,
Shukrani kwa kutembelea hapakwetu na kuweka ujumbe. Nakukaribisha wakati wowote, na nakutakia kila la heri.Mbelehttps://www.blogger.com/profile/16077261126944002622noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post-36158296489944522652016-07-11T07:17:12.884-07:002016-07-11T07:17:12.884-07:00Waswahili twasema 'mwana wa mhunzi asiposana h...Waswahili twasema 'mwana wa mhunzi asiposana huvuvia'.Heko Prof.
Anonymoushttps://www.blogger.com/profile/11788658319123439351noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post-24538433489506545542013-09-13T12:25:07.055-07:002013-09-13T12:25:07.055-07:00Binafsi naamini huyo jamaa hajui maana ya kukutana...Binafsi naamini huyo jamaa hajui maana ya kukutana na mtu kama huyu, mtu ambaye kazi za baba yake na zakwake unazipenda. Binafsi nafahamu, nimekuwa nikisoma machapisho yako mbalimbali kwa muda mfupi tu, na nilitamani kuonana na wewe. Wakati mmoja nilifanikiwa kukuona ukiw ababati-manyara, nilifurahi sana na kutamani kuongea na wewe, lakini sikufanya hivyo kwani bado sikuwa tayari. Kwa hiyo nafahamu namna inavyokuwa unapotaka kukutana na mtu ambaye unamkubwali na unayethamini kazi zake. Watanzania wengi hatuthamni kazi za watuMakengonoreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post-49568477172640446662013-04-30T13:48:42.777-07:002013-04-30T13:48:42.777-07:00Prof achana nao hao, wajuaji wasiojijua. Ungekutan...Prof achana nao hao, wajuaji wasiojijua. Ungekutana vipi na mwandishi mwenyewe wakati alishakufa zamani?

Hongera sana kwa juhudi zako usivunjwe moyo na watu ambao hata kukamata kalamu wakaandika abstract tu hawawezi.Anonymousnoreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post-80829558707704096442013-04-30T10:43:44.196-07:002013-04-30T10:43:44.196-07:00Anonymous wa 30 April, 2013, 6:53, unajifanya unaj...Anonymous wa 30 April, 2013, 6:53, unajifanya unajua taratibu za taaluma, lakini napata picha wewe ni mbabaishaji.

Kwanza, ingekuwa vema iwapo ungejitambulisha ufahamike. Kwenye masuala ya taaluma ndivyo tunavyofanya.

Hayo uliyosema yanathibitisha kuwa wewe huna hata chembe ya ufahamu wa hiki unachoongelea. Mzee Patrick Hemingway anaheshimika duniani kwa maandishi yake yanayohusu uandishi wa baba yake. Ameandika utangulizi katika vitabu mbali mbali vya Ernest Hemingway na hivi kuwapa walimwengu mwanga kuhusu mambo mengi.

Patrick Hemingway amehariri maandishi mengi ya Ernest Hemingway, na pia ndio mmiliki wa urithi wote wa Ernest Hemingway, anayeratibu machapisho na matumizi na mapato yatokanayo na kazi za Ernest Hemingway.

Kila mtafiti anayehusika na masuala ya Ernest Hemingway anatambua kuwa Patrick Hemingway ni mtu wa pekee, mtu pekee aliyebaki, anayejua mengi yasiyojulikana kwa walimwengu.

Kwa msingi huo, fursa niliyopata ya kuwasiliana na Patrick Hemingway na kisha kukutana naye, ni bahati kubwa kwangu. Wewe anonymous zingatia hilo.

Mimi ni mtafiti. Kazi yangu ni kutafuta elimu muda wote. Ujinga ni kama ugonjwa. Natafuta elimu sawa na mgonjwa anayetafuta matibabu. Hii dhana yako kwamba natafuta sifa naiona ni ya mtu asiyeelewa maana ya elimu na taaluma.

Halafu, umethibitisha kuwa wewe ni kilaza wa kutupwa, pale unaposema kuwa ulidhani nimekutana na mwandishi mwenyewe. Huyu mwandishi Ernest Hemingway alishakufa miaka mingi iliyopita. Ningekutana naye vipi wakati huu?

Hata kwenye hii taarifa yangu fupi, nimesema kabisa kuwa Ernest Hemingway alishafariki.

Kati yako anonymous na mimi, ni nani aliyechemsha?
Mbelehttps://www.blogger.com/profile/16077261126944002622noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post-53799540879210854302013-04-30T06:53:26.384-07:002013-04-30T06:53:26.384-07:00Nilidhani umekutana na mwandishi mwenyewe. Taaluma...Nilidhani umekutana na mwandishi mwenyewe. Taaluma hairithishwi hivyo umechemsha na kutafuta sifa tu mkuu.Anonymousnoreply@blogger.com