tag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post2545007932018540480..comments2024-02-19T01:07:06.277-08:00Comments on Hapa Kwetu: Mtunzi Haji Gora HajiMbelehttp://www.blogger.com/profile/16077261126944002622noreply@blogger.comBlogger2125tag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post-49530967255845166432015-12-10T21:00:49.298-08:002015-12-10T21:00:49.298-08:00Ndugu Pascal Bacuez
Shukrani kwa ujumbe wako. Kwa...Ndugu Pascal Bacuez

Shukrani kwa ujumbe wako. Kwa kweli, watunzi kama Haji Gora Haji ni hazina kubwa. Kwa upande wangu ninashukuru kuwa ninayo fursa na mazoea ya kujisomea kazi za watunzi hao na hivyo kuitajirisha akili yangu kwa namna mbali mbali, ikiwemo kuboresha ufahamu wangu wa ki-Swahili.

Wazo lako la kukusanya michango ya wasomi ni wazo bora. Wenzetu katika mataifa mengine wana jadi hiyo tangu zamani. Kuna vitabu vingi ambavyo ni mkusanyo wa maandishi juu ya watunzi maarufu. Sisi tunao watunzi wetu, kama akina Muyaka, Shaaban Robert, Mgeni bin Faqihi, Embrahim Hussein, Haji Gora Haji na Kezilahabi. Wasomi na wahiki wa maandishi ya ki-Swahili bado tuna njia ndefu. Ninafahamu kuwa kazi hapa na pale imefanyika kuhusu waandishi kama Muyaka na Shaaban Robert, lakini haitoshi kabisa.

Labda, kwa kulianzisha na kuliongelea suala hili tutaweza kujizindua na kuwazindua wengine usingizini.Mbelehttps://www.blogger.com/profile/16077261126944002622noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post-77376578837222202932015-12-10T01:59:11.928-08:002015-12-10T01:59:11.928-08:00Ukereketwa wako mpendwa Mbele umeiva sana wala huc...Ukereketwa wako mpendwa Mbele umeiva sana wala huchoki kumtilia pondo HG ambaye naye bila shaka anajua matumizi ya pondo. Juhudi zako zinafaa kabisa ili kulikuza na kulitukuza jina la mshairi mwenzetu. Pengine ingefaa uwe "mfawidhi" na mwasisi katika kazi hiyo ya kukusanya michango ya wasomi mbalimbali, sijui makala kadhaa kuhusu kazi yake, baadhi ya mashairi yake na kadhalika, pamoja na tafsiri zake. Nina uhakika kwamba utapata mwangwi mkubwa, si katika nchi magharibi tu, bali Afrika pia. Pascal Bacuezhttps://www.blogger.com/profile/16276066470099470468noreply@blogger.com