tag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post2761353286826180801..comments2024-02-19T01:07:06.277-08:00Comments on Hapa Kwetu: Vitabu Nilivyonunua LeoMbelehttp://www.blogger.com/profile/16077261126944002622noreply@blogger.comBlogger2125tag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post-86655458136875103432017-08-22T23:27:10.622-07:002017-08-22T23:27:10.622-07:00Ndugu Emmanuel Kachele, shukrani kwa ujumbe. Pole ...Ndugu Emmanuel Kachele, shukrani kwa ujumbe. Pole kwa tatizo la kukosekana vitabu. Lakini ninasikia kuwa kuna uwezekano wa watu huko Tanzania kununua vitabu pepe mtandaoni. Ninafahamu kuwa viko vingi vinavyopatikana kwa mtindo huo, vingi vya bure. Sijui kama njia hii inawezekana mahali ulipo.

Kuhusu kusaidia nchi, binafsi, niliwahi kujiwekea utaratibu wa kukusanya na kupeleka vitabu Tanzania, nikafanya hivyo kwa vyuo kadhaa. Hatimaye, wa-Tanzania wanadiaspora wa jumuia ya mtandao wa Tanzanet walinichangia dola 500, kusaidia usafirishaji wa hivi vitabu, kwani kabla nilikuwa ninajitolea mwenyewe. Vile vile, kila ninapofika Tanzania ninabeba vitabu angalau vichache kwa ajili ya taasisi mbali mbali.
Mbelehttps://www.blogger.com/profile/16077261126944002622noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post-34972492804915680152017-08-22T12:18:25.442-07:002017-08-22T12:18:25.442-07:00Safi sana Profesa Mbele. Ni mara nyingi sana huwa ...Safi sana Profesa Mbele. Ni mara nyingi sana huwa nasoma hizi post zako kuhusu kununua vitabu. Sio siri unanitamanisha sana. Niko Mkoa wa Pembezoni kabisa mwa Tanzania, na kila nikisoma hizo post huwa nawaza sana kama na jamiii yetu ingekuwa na mazingira rahisi ya upatikanaji wa vitabu kama ulio nao huko. Ninatamani sana tena sana.
Lakini labda unaweza kuwa na njia fulani ya kuisaidia nchi yetu na jamii yetu kwa ujumla ili iweze kupata vitabu hadi vijijini kama huku niliko.

Asante sana Profeso.Emmanuel Kachelehttps://www.blogger.com/profile/05939034064386827696noreply@blogger.com