tag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post3617455634227881727..comments2024-02-19T01:07:06.277-08:00Comments on Hapa Kwetu: Tembo wa Hifadhi ya Tarangire, TanzaniaMbelehttp://www.blogger.com/profile/16077261126944002622noreply@blogger.comBlogger4125tag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post-84636373236570909942014-05-31T18:53:34.465-07:002014-05-31T18:53:34.465-07:00Ndugu Anonymous, nimeguswa na ujumbe wako. Navutiw...Ndugu Anonymous, nimeguswa na ujumbe wako. Navutiwa na nawaheshimu kwa namna ya pekee watu wanaosoma vitabu, sio kwa sababu ya mitihani bali kujipanua ufahamu wa mambo ya aina mbali mbali.

Nipe anwani yako ya posta, nami naahidi nitakuletea nakala ya kitabu maarufu cha Maya Angelou, "I know Why the Caged Bird Sings." Nitafurahi ukiwa na angalau hiki kimoja.

Unaweza kutumia anwani yangu: info@africonexion.com

Kila la heri.Mbelehttps://www.blogger.com/profile/16077261126944002622noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post-84894191105444066422014-05-31T18:01:28.002-07:002014-05-31T18:01:28.002-07:00Nashukuru kwa ufafanuzi wako mzuri, Nimekuwa nikis...Nashukuru kwa ufafanuzi wako mzuri, Nimekuwa nikisoma habari zake na kusukiliza baadhi ya mahojiano yake radio 4(http://www.bbc.co.uk/programmes/p01zxd06).
Kwa bahati mbaya sijaweza kuona kitabu chake chochote wala kukisoma.
MdauAnonymousnoreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post-28869006688808043072014-05-31T10:12:23.456-07:002014-05-31T10:12:23.456-07:00Ndugu Anonymous, shukrani kwa ujumbe wako. Sijasom...Ndugu Anonymous, shukrani kwa ujumbe wako. Sijasoma maandishi ya Maya Angelou, labda mashairi mawili matatu. Sina utaalam wowote juu yake, ingawa najua kiasi habari zake.

Nilimsikiliza siku moja, miaka mingi kidogo iliyopita, akitoa mhadhara katika chuo cha jirani cha Carleton. Pia, siku nyingine, nilimsikiliza kwenye mahojiano katika TV.

Kwa miaka, nimekuwa na baadhi ya vitabu vyake, lakini sijavisoma, labda kwa kugusia gusia tu. Sina ufahamu wa kuweza kuandika makala juu yake.

Kuna mamia ya waandishi ambao kazi zao sijazisoma, na hakuna anayeweza kuzisoma zote. Wengi wa waandishi hao wameshinda tuzo kubwa kubwa, kama vile tuzo ya Nobel, lakini mtu hata kama ni profesa wa "Literature" kama mimi, huwezi kuwasoma wote.

Nakumbuka niliwahi kuelezea tatizo hili, au ukweli huu, katika blogu yangu hii. Siku hiyo, kama sikosei, nilimtaja mwandishi Orhan Pamuk wa Uturuki, ambaye alikuwa ameitwaa tuzo ya Nobel, nami ingawa nilikuwa, na bado nina vitabu vyake viwili vitatu, sijavisoma bado.

Inasikitisha, kwamba ningependa kuwa na ufahamu wa kutosha wa waandishi wote maarufu, lakini haiwezekani.Mbelehttps://www.blogger.com/profile/16077261126944002622noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post-59245074158204869122014-05-30T23:16:47.889-07:002014-05-30T23:16:47.889-07:00Ndugu, Ningependa kusoma andiko lako lolote kuhusu...Ndugu, Ningependa kusoma andiko lako lolote kuhusu Maya AngelouAnonymousnoreply@blogger.com