tag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post4941304370792394409..comments2024-02-19T01:07:06.277-08:00Comments on Hapa Kwetu: Vitabu Nilivyojipatia LeoMbelehttp://www.blogger.com/profile/16077261126944002622noreply@blogger.comBlogger3125tag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post-66809306584213992182017-01-20T04:59:21.729-08:002017-01-20T04:59:21.729-08:00Ndugu Mbele umenikumbusha nami vitabu nilivyoacha ...Ndugu Mbele umenikumbusha nami vitabu nilivyoacha nyumbani. Kwa wanaonijua, kila aliyetembelea kwetu alikuwa akiuliza huyu mtu anafanya nini na vitabu vyote ni vya nini? Kwa familia changa ya mtoto mmoja kipindi kile kuwa na sebule iliyoshiba shelf ya vitabu ukuta hadi ukuta chini hadi juu na kushoto kulia halikuwa jambo la kawaida. Huo ndiyo utajiri nilio kuwa nao na wakati wa kuondoka hakuna kilichoniumiza kama kuacha vitabu vyangu ambavyo vingine havichapishwi tena. Ilikuwa sawa na kuwaacha marafiki zangu wapendwa.Ndugu Nkwazi N Mhangohttps://www.blogger.com/profile/11640087613265490788noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post-49910286188924073332017-01-19T19:00:31.177-08:002017-01-19T19:00:31.177-08:00Shukrani kwa ujumbe, ndugu Mhango. Mara nyingi nin...Shukrani kwa ujumbe, ndugu Mhango. Mara nyingi ninajikuta nikiwa na masikitiko kwamba sitaweza kuvisoma vitabu vyangu vyote vilivyoko Tanzania na hapa Marekani. Ni vingi mno, na bado ninapenda kujipatia vitabu sawa na nilivyopenda nilipokuwa kijana mdogo.<br /><br />Dini nyemelezi, kama unavyoziita, zimechanganywa na ukasuku katika bara letu la Afrika, na matokeo yake ni majanga. Waumini wengi wamezipeleka akili zao likizoni.Mbelehttps://www.blogger.com/profile/16077261126944002622noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post-90375923895319154372017-01-18T18:37:26.130-08:002017-01-18T18:37:26.130-08:00Ndugu Mbele hongera kwa kuendeleza utamaduni wa ku...Ndugu Mbele hongera kwa kuendeleza utamaduni wa kuthamini vitabu. Hata mie huwa na tabia hiyo hasa nipitapo kwenye meza zenye vitabu ambavyo yoyote anaweza kuchukua. Hakuna kitu cha thamani kama kupata kitabu tena cha kitaaluma kikiwe hakina price tag.<br />Endelea kukusanya vitabu kwani scripta est manent yaani lililoandikwa ni la milele. Afrika sasa inahangaishwa na kuhujumiwa kwa sababu ya vitabu vya dini vilivyoletwa kueneza mila za hovyo za wengine kama ulivyomalizia kuwa Quran haisemi wanawake wavae nini zaidi ya kujihifadhi. Kuna aya mbili nilizipata jana wakati nikifanya utafiti wa mswaada wangu juu ya Ugaidi na namna Marekani na mataifa ya Ulaya na mengine yenye nguvu yanavyoitumia kuikalia Afrika kijeshi ili kuendelea kuinyonya. Haya hizi ni Qurans (42:7) “Hivyo, tumedhihirisha Korani kwako, ili muweze kuonya mji mkuu na waishio karibu yake...”<br />Na nyingine ni Quran (14:4) “ Hatkutuma mtume yeyote ila kwa lugha ya watu wake ili kufanya mambo kuwa rahisi. Allah humpotosha amtakaye na humuongoza yeyote amtakaye. Tafsiri ni yangu. Pamoja na haya kuwa wazi, wengi hawajui kiasi cha kupwakia kila upuuzi kwa sababu ni wavivu wa kusoma.Ndugu Nkwazi N Mhangohttps://www.blogger.com/profile/11640087613265490788noreply@blogger.com