tag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post5181196269442641329..comments2024-02-19T01:07:06.277-08:00Comments on Hapa Kwetu: Video ya Kumbukumbu ya Miaka Kumi ya KitabuMbelehttp://www.blogger.com/profile/16077261126944002622noreply@blogger.comBlogger2125tag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post-130853165561490952015-03-12T13:46:58.509-07:002015-03-12T13:46:58.509-07:00Shukrani, Dada Yasinta, kwa ujumbe wako. Pamoja na...Shukrani, Dada Yasinta, kwa ujumbe wako. Pamoja na uandishi, huwa najielimisha kuhusu uandishi wa vitabu, kuhusu uchapishaji na uuzaji wa vitabu. Ninanunua na kusoma vitabu vinavyoelimisha kuhusu masuala hayo.

Papo hapo, ninajitahidi kuwanufaisha wengine kwa yale ninayojifunza. Kwa mfano, mara kwa mara huwa naandika makala katika blogu hii, na nimeweka pia makala katika kitabu changu cha CHANGAMOTO: Insha za Jamii, ambamo nawaeleza wengine yale ninayoyafahamu.

Hizi juhudi zangu za kutangaza kitabu change ni mwendelezo wa hayo niliyosema hapa juu. Vitabu nilivyosoma vinasisitiza mengi, na mojawapo ni jukumu la mwandishi kutangaza kitabu chake. Nami nategemea kuwa kwa kuonyesha mfano, waandishi wasiojua suala hilo wataweza kujifunza.

Mimi kama mwalimu, nina wajibu wa kufanya utafiti, kujielimisha, na kuwafundisha wengini. Kuandika Makala na vitabu ni wajibu wangu, na kama ilivyo kwa mwalimu ye yote, kazi yangu ni kuwapa wengine yale ninayoyafahamu. Kwa msingi huu, nina wajibu wa kutangaza vitabu vyangu.

Ninashukuru kuwa wasomaji nao, wanablogu kama wewe Dada, wahakiki, na walimu wenzangu hapa Marekani wamekuwa mstari wa mbele katika kunitangazia kitabu hiki na vitabu vyangu vingine.

Napenda kurudia shukrani zangu kwako.Mbelehttps://www.blogger.com/profile/16077261126944002622noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post-31312339860337814182015-03-12T00:57:54.954-07:002015-03-12T00:57:54.954-07:00Nimependa sana mtindo wako wa kukitangaza kitabu h...Nimependa sana mtindo wako wa kukitangaza kitabu hiki. HONGERA SANA KWA KUMBUKUMBU YA MIAKA KUMI YA KITABU. TUPO PAMOJA.Yasinta Ngonyanihttps://www.blogger.com/profile/09314172793959023532noreply@blogger.com