tag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post7153446463225148098..comments2024-02-19T01:07:06.277-08:00Comments on Hapa Kwetu: Nadharia ya Uandishi Mbelehttp://www.blogger.com/profile/16077261126944002622noreply@blogger.comBlogger2125tag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post-56631545935939954742015-06-04T21:04:46.759-07:002015-06-04T21:04:46.759-07:00Ndugu Mhango, ni sawa kabisa unavyosema. Uandishi ...Ndugu Mhango, ni sawa kabisa unavyosema. Uandishi wa kweli ni huu unaouelezea kama moto. Siku nyingine, panapo majaliwa, nitaleta mawazo ya Ernest Hemingway ambayo yako katika mkondo huo huo.<br />Nilianzisha mada hii kwa mategemeo kuwa kuna wanaotafiti au kusomea nadharia za fasihi, nikataka wapate mambo ya kuyatafakari. Na kwa kweli, huwa Napata ujumbe mara moja moja kutoka kwa waandishi chipukizi wa Afrika Mashariki wakiulizia hili au lile.<br />Mada hii nilitaka wazingatie hasa wale wanaoandika wakiwa tayari na ndoto ya kuwa maarufu, au duku duku na mategemeo ya kazi zao kuingizwa kwenye mitaala ya masomo. Mtazamo aliouelezea Mario Vargas Llosa unajenga hoja kwamba hili ni tatizo, nami ningeweza kuongezea kuwa ni sehemu ya tatizo ambalo wanafalsafa huliita "alienation." Yaani mtu unafanya shughuli kama mashine, bila nafsi yako kufungamana na shughuli yenyewe.<br />Kinachotakiwa ni kwa uandishi kuwa sehemu ya nafsi ya mwandishi, na uandishi wa aina hiyo unakuwa na uhalisia, kwa ki-Ingereza wanaita "authenticity."Mbelehttps://www.blogger.com/profile/16077261126944002622noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post-36404362480963953352015-06-04T18:36:55.641-07:002015-06-04T18:36:55.641-07:00Mwalimu Mbele nakubaliana nawe. Licha ya uandishi ...Mwalimu Mbele nakubaliana nawe. Licha ya uandishi kuwa tunu ni kama ugonjwa au moto unaowaka kiasi cha kutaka mwenye kuubeba aendelee kuuchochea. Nakumbuka zamani mke wangu alikuwa akinilalamikia nilipokuwa nikiandika makala kali sana. Alikuwa anauliza, "Kwani usipoandika utakufa?" Mara zote nilimjibu ndiyo. Maana nisipofanya hivyo, nguvu inayonisukuma na kuniwezesha kuandika inaweza kuupasua moyo wangu. Kwa machache tu, kuandika si tunu bali moto unaowaka kwenye nafsi na moyo wa mwandishi. Hata akijitahhidi kuupuuzia haumpuuzii. Nakumbuka niliandika kitabu changu cha kwanza Dear Mothers mwaka 1989. Hadi sasa sijawahi kukichapisha na sijui hata mswada wake niliouacha Tanzania kama bado upo salama.Ndugu Nkwazi N Mhangohttps://www.blogger.com/profile/11640087613265490788noreply@blogger.com