tag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post8040718532629283153..comments2024-02-19T01:07:06.277-08:00Comments on Hapa Kwetu: Vitabu Nitakavyoonesha Katika Tamasha la Afrifest, Agosti 2Mbelehttp://www.blogger.com/profile/16077261126944002622noreply@blogger.comBlogger2125tag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post-3608344862187485722014-07-29T12:09:11.901-07:002014-07-29T12:09:11.901-07:00Shukrani, Dada Yasinta. Mimi ni mwalimu ambaye nai...Shukrani, Dada Yasinta. Mimi ni mwalimu ambaye naipenda na kuiheshimu sana kazi yangu. Kuandika makala na vitabu ni sehemu ya ufundishaji.

Pamoja na ugumu wake, ni shughuli ninyoipenda. Kitabu cha "Matengo Folktales," kilinichukua miaka yapata 23 kukiandaa. Lakini nafurahi nilifanya hivyo.

Raha yangu kama mwandishi ni kuona watu wanasoma niliyoandika. Juzi hapo Ndugu Bwaya ametueleza jinsi nakala yake ya "Africans and Americans" ilivyoazimwa na kuzunguka kwa watu mbali mbali hadi kupotelea kusikojulikana hadi leo.

Tukio la aina hii tunaweza kulitafsiri kwa namna mbali mbali, lakini kwa mimi mwandishi ni ishara nzuri. Kwa hiyo, nafurahi kwamba wewe ni mmoja wa wasomaji wangu.

Msomaji ana uhuru kamili wa kuafiki au kupinga ninayoandika, au kuwa na mawazo mengine tofauti. Hiyo ni haki yake na ana uhuru kamili. Ninachosema ni kuwa naona faraja maandishi yangu yakisomwa. Ni hilo tu.

Mbelehttps://www.blogger.com/profile/16077261126944002622noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post-43378396106159755412014-07-29T03:58:51.400-07:002014-07-29T03:58:51.400-07:00Hongera sana kwa kuandika vitabu vingi mie nimesom...Hongera sana kwa kuandika vitabu vingi mie nimesoma viwili tu kati ya hivyo.Yasinta Ngonyanihttps://www.blogger.com/profile/09314172793959023532noreply@blogger.com