tag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post8239579946024832005..comments2024-02-19T01:07:06.277-08:00Comments on Hapa Kwetu: Mwandishi Seenaa Aongelea Kitabu Chake Mjini MinneapolisMbelehttp://www.blogger.com/profile/16077261126944002622noreply@blogger.comBlogger2125tag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post-14183242935578872482015-08-08T20:06:34.277-07:002015-08-08T20:06:34.277-07:00Ndugu Mandela Pallangyo,
Shukrani kwa ujumbe wako...Ndugu Mandela Pallangyo,

Shukrani kwa ujumbe wako. Ninajisikia vizuri kuongea na waandishi chipukizi na kuwapa yale ambayo nayafahamu, kama nilivyowahi kuandika katika blogu hii. Huyu dada Seenaa niliyemwongelea hapa alifurahi sana kukutana nami ile siku tulipokusanyika kusikiliza maongezi juu ya kitabu chake. Alikuwa ameambiwa na yule Peter wa Chicago habari zangu.

Siku ya pili yake, yaani tarehe 5, Seenaa nami tulikutana tena, tukaongea kirefu. Nilipata wasaa wa kumhamasisha kwa hili na lile, hasa kwa vile nilishaanza kusoma kitabu chake. Baadaye, yeye, dada mwingine, na mimi tulienda kuangalia mechi ya kabumbu kati ya timu za wa-Oromo. Tulizungumza kirefu zaidi.

Kwa mawazo yangu, Seenaa atakuja kuwa maarufu katika uandishi na katika harakati za ukombozi, hasa ukombozi wa wanawake. Ni jasiri. Anatoka katika familia ya ki-Islam, lakini amekuwa akipambana na mila desturi ambazo zinadaiwa kuwa ni za ki-Islam, lakini yeye anaziona ni kipingamizi kwa haki za wanawake.Mbelehttps://www.blogger.com/profile/16077261126944002622noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post-70678143744113675302015-08-08T16:06:52.270-07:002015-08-08T16:06:52.270-07:00napenda sana mwaalimu anavyoshirikisha mawazo. nap...napenda sana mwaalimu anavyoshirikisha mawazo. napenda sana unapokuwa karibu na waandishi wengine. inatupa hamasa. napenda sana kuandika lakini naona siku za karibuni nitaachana na fani hii kisha niendelee kuchimba madinimandela pallangyohttp://www.mandelapallangyo.comnoreply@blogger.com