tag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post867422275062486677..comments2024-02-19T01:07:06.277-08:00Comments on Hapa Kwetu: Mwalimu Nyerere na ElimuMbelehttp://www.blogger.com/profile/16077261126944002622noreply@blogger.comBlogger6125tag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post-26945690417148680282017-11-11T21:13:59.392-08:002017-11-11T21:13:59.392-08:00Ndugu Davis Kiwelu, shukrani kwa suali lako. Sina ...Ndugu Davis Kiwelu, shukrani kwa suali lako. Sina hakika kama nina jawabu, bali nina mtazamo. Ninaona kuwa mbali na suala la kutoa elimu bure, jambo ambalo Mwalimu Nyerere alifanikisha vizuri, tukiangalia suala la elimu ni nini, tutaona kuwa Mwalimu Nyerere alikuwa na upeo sahihi, lakini leo tunakwamisha. Ninamaanisha nini?

Ni kwamba Mwalimu Nyerere alitaka elimu iwe inamfanya mwanafunziv asiwe mtu wa kuitikia au kukariri mambo, bali awe na tabia ya kudadisi mambo, na awe anajitambua na kujiamini. Leo ninaona kuwa tunapotea njia. Watu wanazungumzia miundo mbinu, madawati, na vitu vingine, bila kuangalia suala la elimu ni nini.

Leo, katika Tanzania ya awamu ya tano, utamaduni wa kuhoji unadidimizwa katika jamii na hii inaathiri malezi ya vijana pia. Siamini kama mazingira ya leo yanajenga ujasiri na uthubutu alioongelea Mwalimu Nyerere. Miaka ya Mwalimu Nyerere tulikuwa tunatafakari nadharia za wanafalsafa wa elimu kama Paulo Freire, ambao walihusisha elimu na ukombozi, kuanzia na ukombozi wa fikra hadi ukombozi kwa maana pana ya mapinduzi ya jamii.Mbelehttps://www.blogger.com/profile/16077261126944002622noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post-24673410163599559192017-11-07T09:40:09.888-08:002017-11-07T09:40:09.888-08:00ni kweli uliyo yasema hapo juu.... Nina swali kwak...ni kweli uliyo yasema hapo juu.... Nina swali kwako Mr. Mbele kama Mwalimu wa Chuo Kikuu, unazungumiaje elimu ya sasa inayotolewa mashuleni na kwenye vyuo vikuu kulingana na sera ya Elimu bure naa ukilinganisha na elimu iliyotolewa na Mw. Nyerere zamani hizo.kwetutz24https://www.blogger.com/profile/09526881676019419144noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post-15256795862478358112017-10-16T02:48:48.783-07:002017-10-16T02:48:48.783-07:00Ndugu Aginiwe Mbilinyi, shukrani kwa ujumbe. Kitab...Ndugu Aginiwe Mbilinyi, shukrani kwa ujumbe. Kitabu hiki, "Nyerere on Education/Nyerere Kuhusu Elimu," kilichapishwa na kampuni iitwayo E & D Ltd iliyoko Da es Salaam. Ninaamini kinapatikana katika maduka ya vitabu nchini Tanzania. Vitabu vya makampuni ya uchapishaji mengi ya Afrika vinasambazwa huku ughaibuni na African Books Collective iliyoko Uingereza na Michigan State University Press iliyoko hapa Marekani.

Nashawishika kuongeza jambo. Hii kampuni ya E & D Ltd ilianzishwa na inaendeshwa na akina mama wawili: Elieshi Lema na Demere Kitunga, ambao walikuwa wanafunzi wangu wa "Literature," Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Wana mtazamo wa kimaendeleo kuhusu uchapishaji, vitabu, na elimu kwa ujumla, na wanahamasisha usomaji wa vitabu kwa rika zote. Fuatilia shughuli zao, utajionea mwenyewe. Nakutakia kila la heri.Mbelehttps://www.blogger.com/profile/16077261126944002622noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post-3035064813454385692017-10-13T23:39:24.691-07:002017-10-13T23:39:24.691-07:00Nashukuru kwa naelezo haya Ninauhitaji na kitabu h...Nashukuru kwa naelezo haya Ninauhitaji na kitabu hicho nimeshindwa kukipata hapoMbilinyi mwinamahttps://www.blogger.com/profile/08777727910159738464noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post-37398168932467187942008-12-07T13:31:00.000-08:002008-12-07T13:31:00.000-08:00Shukrani sana kwa mchango wako. Ni kweli usemavyo,...Shukrani sana kwa mchango wako. Ni kweli usemavyo, kuhusu maarifa. Sehemu mbali mbali duniani watu wanatambua kuwa uchumi wa dunia ya leo unatawaliwa na maarifa kuliko kitu kingine chochote. Fundisho hili bado halijaingia vichwani mwa Watanzania wengi, na hivyo tunajichimbia kaburi. Lazima tujenge utamaduni wa kutafuta elimu na maarifa, utamaduni wa kusoma vitabu, kuhudhuria mafunzo ya aina mbali mbali. Tunatakiwa tuamke kimawazo na kutambua kuwa kununua vitabu na kuvisoma, au kulipia semina ni sawa na kugharamia pembejeo katika kilimo au kitendea kazi chochote. Kama tunafanya biashara, kwa mfano, tutambue kuwa kuna vitabu ambavyo vina nadharia, mbinu, na mawaidha muhimu. Kuna mambo madogo kama kumjali mteja. Siri moja ya mafanikio katika biashara ni kumjali na kumhudumia vizuri mteja. Inasikitisha kuwa hata jambo dogo kama hili wengi hawalitambui. Matokeo yake ni kuwa biashara yao ikizorota, wanasema wamelogwa. Narudia, shukrani kwa mchango wako. Katika kufuatilia habari zako mtandaoni leo, nimeona kuwa umeandika kitabu, _E-Commerce for Development: eTourism as a Showcase_. Nitakitafuta.Mbelehttps://www.blogger.com/profile/16077261126944002622noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post-70644585980842633862008-12-07T06:16:00.000-08:002008-12-07T06:16:00.000-08:00Hakika, bila utamaduni wa kusaka maarifa kwa njia ...Hakika, bila utamaduni wa kusaka maarifa kwa njia mbalimbali hasa kujisomea, taifa letu tutazidi kubaki nyuma. Kwa vile pande nyingine za dunia wanatumia muda na rasrimali nyingine kujielimisha kwa muda wote, jamii ambazo hazifanyi hivyo ziko mashakani kuendelea.

Kwa vile sasa uchumi unatawaliwa na maarifa zaidi kuliko rasrimali nyingine kama ardhi, madini, misitu, nk, haishangazi jinsi jamii zetu tunavyozidi kutegemea watu wengine watutengenezee vifaa vilivyojaa maarifa. Katika jamii zetu karibu kila kitu cha kutegemea maarifa sana kimetengenezwa njee. Hii ni hatari kwa usalama na maendeleo.

Ili tuendelee tunabidi na sisi tuuze bidhaa zilizotengenezwa kwa kuongezewa thamani ya maarifa na tuagize bidhaa kama hizo kutegemea na mahitaji ya walaji (product differentiation). Mfano mzuri ni kwamba hata nchi zinazotengeneza tuseme magari bado zinaagiza magari toka nchi nyingine. Utaratibu huu unaitwa "intra-industry trade" katika Uchumi.

Katika kuyasaka maarifa inapaswa kufika kipindi cha kutakiwa kuachia ("unlearn") baadhi ya vitu tunavyovifahamu kwa sasa. Hii inatokana na ukweli kwamba kadri mtu anavyopata ukweli sahihi, mambo mengine aliyodhani hapo zamani kuwa ni kweli inabidi aachane nayo. Labda hii ya kuutafuta ukweli sahihi inaweza ikawatisha baadhi ya watu kujisomea zaidi. Maana inasemekana kuwa "ujinga una raha zake" yaani ignorance is bliss! Kwa uhakika hakuna raha yeyote kwenye "ujinga" kwa vile dunia haibadiriki eti mtu anaiangalia kwa mtazamo usio sahihi.

Ka-mchango kangu katika uzi (thread) huu wa maana sana.kamuzohttps://www.blogger.com/profile/03911631365251631886noreply@blogger.com