tag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post9184017982518720672..comments2024-02-19T01:07:06.277-08:00Comments on Hapa Kwetu: Mteja Nimefurahia HudumaMbelehttp://www.blogger.com/profile/16077261126944002622noreply@blogger.comBlogger2125tag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post-74815744594907420472015-06-21T17:18:42.795-07:002015-06-21T17:18:42.795-07:00Ndugu Mhango, ni kweli usemavyo. Hapa Marekani, uk...Ndugu Mhango, ni kweli usemavyo. Hapa Marekani, ukinunua kitu, una uhuru wa kukirudisha kwa sababu yoyote ile, au hata kama huna sababu. Unachohitaji ni kuonyesha risiti tu, ambayo ulipata uliponunua. Uamuzi ni wako, kwa mfano labda unataka kitu kile kile ila rangi tofauti, au saizi tofauti, au unataka kurudishiwa pesa zako. Wanaheshimu kabisa matakwa ya mteja, na unapoondoka wanakuambia karibu tena.

Tanzania kuna vituko, ambavyo tumeishi navyo tangu zamani. Kwa mfano, kuna risiti nyingi ambamo kumeandikwa wazi kuwa kitu kikishanunuliwa, huwezi kukirudisha. Risiti yenyewe inasema hivyo. Kama umelizwa basi wewe ulie tu.

Unaingia katika maduka mengi Tanzania, au sehemu ya kupatia huduma, hata kama ni ofisi, na unapokelewa kama vile wewe ni kero fulani. Ni nadra kukaribishwa vizuri. Mara kwa mara, nimewakalisha chini mameneja na wahudumu kwenye baa na kuwapa mhadhara kuhusu thamani halisi ya mteja, hata kama ananunua soda moja tu na kwenda zake.
Watawala wetu nao ni sifuri. Mengi wanayaona huku ughaibuni, kwa mfano usafi wa miji, lakini wakisharejea Bongo, wanaidhika wala haiwasumbui kuona mitaro michafu, malundo ya takataka kila mahali, mifuko ya plastiki inapeperushwa na upepo mitaani, migahawa iko pembeni mwa mitaro, na kadhalika na kadhalika.
Huwa nashangaa kwa nini wanaitwa viongozi, wakati hakuna wanachoongoza wala wanayemwongoza. Ni watawala, kama unavyosema. Pamoja kwenda shule, hawatambui hata suala la msingi la umuhimu wa usafi katika mazingira.
Uchafu wa mazingira, kwa mujibu wa wanafalsafa fulani ni kioo cha uchafu wa moyoni. Moyo ya ukatili wa watoa huduma na jamii kwa ujumla ni moyo huo huo unaoleta na kudumisha ukatili dhidi ya mazingira.
Mbelehttps://www.blogger.com/profile/16077261126944002622noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-3497774938071508976.post-84992155217332008172015-06-21T06:58:20.673-07:002015-06-21T06:58:20.673-07:00Kaka una bahati. Ingekuwa Tanzania hiyo huduma ya ...Kaka una bahati. Ingekuwa Tanzania hiyo huduma ya tire rotation ungechajiwa hata kama inatolewa bure. Wenzetu wana ustaarabu wa kupigiwa mfano hasa ukilinganisha na ushenzi unaofanyika nyumbani. Mfano huku ukinunua kitu na kukuta kuwa ima hukihitaji au hakifai au mwenzio alishanunua kingine unamrejeshea aliyekuuzia. Jaribu hilo nyumbani. Hatapokea hiyo bidhaa zaidi ya kukurushia mitusi. Rafiki yangu toka Nigeria alisema kuwa ukirejesha bidhaa dukani kwao utaambulia kipigo. Huwa najiuliza: Ni lini tutafikia kiwango hiki cha utu na huduma bora? Ajabu hata watawala wetu wanapokuja huku wakatendewa hivi hawaendi kurudufu hili. Badala yake sijui huwa wanajifunza nini?Ndugu Nkwazi N Mhangohttps://www.blogger.com/profile/11640087613265490788noreply@blogger.com