Friday, March 6, 2009

Busara za Kipanya

Kati ya watu maarufu sana Tanzania ya leo ni mchoraji wa vikatuni vya Kipanya. Tovuti yake hii hapa.

Ujumbe wa Kipanya katika katuni inayoonekana hapa unatukumbusha mambo ya msingi. Tunapoongelea masuala ya nchi yetu, au wahusika wanapopanga mipango mbali mbali, walengwa wakuu wanakuwa hao wanaoishi vijijini, ambao ndio asilimia kubwa ya wananchi, au walengwa wanakuwa hao wa mijini, ambao ndio wapangaji wa hiyo mipango?

3 comments:

Simon Kitururu said...

Napenda sana kazi za Kipanya!

Tanzania sasa hivi sio nchi moja kinamna.

Kuna maeneo hata Dar es salaam unaweza kuvuka barabara moja tu na kujikuta unaongea na watu waongeao tofauti kimaisha na hata kifikira. Kuna watakao kuambia bongo tambarare wakati unaona wapandao mlima.

Wapanga mipango wana maisha yao na wapangiwa mipango wana maisha tofauti na mipango.:-(

Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli Tanzania yetu ya zamani sio ile tena Naipenda Tanzania. Na naomba Mungu tuzidi kuendelea kuwa na maendeleo na pia Amani

Christian Bwaya said...

Nakubaliana na Kipanya kwamba lingekuwa jambo la msingi kama hiyo 'dharura' isiyoisha kujadiliwa ingewahusu wa-Tanzania waliowengia wasioufaham muujiza wa umeme.

Vinginevyo, kwa mwenendo huu wa mambo, ni ukweli kwamba tuliko, si mahali salama sana.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...