Sunday, March 1, 2009

Ushauri kwa Viongozi wa Serikali - Awamu ya Nne

Nimesoma makala, ambayo imeandikwa na H.S. Kasori, nikavutiwa sana na anayosema kuhusu Mwalimu Nyerere. Miaka yote tangu nilipoanza kuyafahamu masuala ya siasa, nimemwona Mwalimu Nyerere kuwa mtu wa aina hiyo anayoongelea Kasori. Pamoja na masuala mengine yote katika blogu yangu hii, ninajitahidi kutaja na kujadili mchango wa Mwalimu Nyerere. Ni muhimu tuendelee kufanya hivyo, kwani mchango wa Mwalimu Nyerere kwa Taifa letu na dunia ni mkubwa sana.

Kuna upotoshaji mwingi kuhusu Mwalimu Nyerere. Naamini kuna pia juhudi inafanywa nchini Tanzania kuzimisha na kufifisha fikra za Mwalimu Nyerere. Hayo nitaendelea kuyaongelea katika blogu hii.

Mimi ni Mtanzania ambaye si mwanachama wa chama chochote. Msimamo wangu kuhusu vyama vya siasa Tanzania ninautoa katika baadhi ya makala zangu ndani ya blogu hii. Naileta hapa makala ya Kasori kwa vile nimevutiwa na yale anayosema kuhusu Mwalimu Nyerere.

Nawakaribisha kusoma makala ya Kasori, "Ushauri kwa Viongozi wa Serikali - Awamu ya Nne".

3 comments:

Simon Kitururu said...

Asante sana kwa kuiunganisha hii makala Prof.

Yasinta Ngonyani said...

Nimepita tu kukusalimia nitarudi siku yake

Mbele said...

Ndugu Kitururu, nafurahi unafuatilia masuala haya. Dada Yasinta, shukrani kwa kutembelea hapa kwetu. Mimi natembelea blogu yako kila siku, kufuatilia picha na masuala ya kwetu.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...