Sunday, October 4, 2009

Diwani--"KWANZA JAMII Limefika Roya!"

(Taarifa hii imechapishwa katika blogu ya Mjengwa tarehe 4 Oktoba, 2009. Nikiwa ni mwandishi mmojawapo wa KWANZA JAMII, nafurahi jinsi gazeti hili linavyojitahidi kuingia vijijini. Hata kijijini kwangu, Wilaya ya Mbinga, linafahamika)

Mchana huu Diwani wa Kata ya Roya Bw. Emmanuel Kigodi amempigia simu mwandishi wa KWANZA JAMII Victor Makinda kumjulisha kuwa nakala nne za KWANZA JAMII zimemfikia. Gazeti hilo limebeba habari kubwa ukurasa wa mbele yenye kuhusiana na ujambazi uliotokea kwenye kata hiyo hivi karibuni. Kwa mujibu wa Diwani Kigodi, gazeti hilo la KWANZA JAMII sasa limekuwa gumzo kijijini Roya na linazunguka kwa wanakijiji wenye hamu ya kusoma habari zake!

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kwa kweli ni furaha sana kusikia hili. Safi sana kwani ni mara chache sana magazeti kama haya kufika hadi kijijini.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kumbe ndo maana akaendaaaa!

Sisulu said...

bahati ya mtende kwa wapenda habari muhimu, adimu na sufufu nawatakia heri kuntu wana rorya-wasaaalam.

Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault

Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...