Saturday, June 5, 2021
Ms. Vera Moore - Mdau Mpya wa Kitabu Changu
Wiki hii nzima, nimekuwa nikihudhuria mkutano mkuu uitwao Trade With Africa Business Summit. Mkutano umejumlisha wafanya biashara, wanadiplomasia, na wajasiriamali, na wengine kutoka nchi mbali mbali. Mwandaaji wa mkutano, Toyin Umesiri kutoka Nigeria, mjasiriamali na mhamasishaji wa biashara baina ya Afrika na Marekani, alikuwa amenialika kuongelea kitabu changu, "Africans and Americans: Embracing Cultural Differences." Alikipigia debe mkutanoni, na kilitajwa mara kwa mara. Mjumbe mmoja, Vera Moore, mfanyabiashara maarufu wa vipodozi, alitusisimua alipokuwa akiongea, kwa kutuonyesha nakala ya kitabu akisema ameshanunua. Nilishangaa alivyokinunua haraka namna ile. Nafurahi kuwa na mdau maarufu huyu. Wengine wanakuja.
Friday, May 28, 2021
Nimealikwa Kuongelea Kitabu Changu
Nimealikwa kuongelea kitabu changu, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences, katika mkutano mkubwa ujulikanao kama Trade With Africa Summit utakaofanyika kutumia mtandao tarehe 31 Mei hadi 4 Juni mwaka huu. Mkutano huu hufanyika mara moja kwa mwaaka.Aliniaalika ni mwanaadji waa mkutano Toyin Umesiri, mjasiriamali na mhamasishaji maarufu wa biashara baina ya Afrika na nchi zingine, hasa Marekani. Aliamua kunialika baada ya kusoma kitabu changu kisha akanialika kwenye kipindi chake cha Nazaru TV na kufanya mahojiano nami.
Kwa miezi ya karibuni, mimi mwenyewe nimeanza kujibidisha kutafiti namna tofauti za tamaduni zinavyoathiri biashara. Mawazo yangu tayari yanaonekana katika kitabu changu, lakini ninayaendeleza na kuyafafanua. Mfano ya juhudi zangu ni makala katika Medium na maongezi katika YouTube.
Kwa miezi ya karibuni, mimi mwenyewe nimeanza kujibidisha kutafiti namna tofauti za tamaduni zinavyoathiri biashara. Mawazo yangu tayari yanaonekana katika kitabu changu, lakini ninayaendeleza na kuyafafanua. Mfano ya juhudi zangu ni makala katika Medium na maongezi katika YouTube.
Saturday, April 3, 2021
Kitabu Kimetua Abuja, Nigeria
Mwezi Machi 2021 umeisha vizuri kwangu. Kitabu changu, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences, kimetua Nigeria. Nilikuwa nimempelekea Jennifer Chinyelu Ikeaba-Obiasor, aonekanaye pichani, ambaye anaishi Abuja. Huenda hii ni nakala ya kwanza kuingia Nigeria.Jennifer alisoma kitabu akaandika maoni kwa nyakati mbali mbali:
Ni kitabu murua chenyee upeo utakaowasidia waAfrika na waMarekani.
Uzoefu wangu unaendana na karibu kila kipengele kitabuni humu. Na kitawafungua macho watu wa tamaduni zote mbili.
Ninakipendekeza kitabu hiki kwa kila mmoja, akisome kwa sababu kitamgusa.
Jennifer nami tulikutana mtandaoni wiki chache zilizopita tukiwa wafuasi wa Toyin Umesiri, mhamasishaji maarufu wa biashara baina ya Afrika na Marekani, ambaye aliwahi kufanya mahojiano nami kuhusu kitabu changu na kuhusu athari za tamaduni katika biashara baina ya waAfrika na waMarekani. Jennifer ni mjasiriamali, mwanzishi na mkurugenzi mkuu wa Chiblenders Green. Katika juhudi za kueneza shughuli zake kimataifa, anafahamu umuhimu wa kuzielewa tamaduni za wengine. Katika muda mfupi wa kufahamiana naye, amenifundisha mengi na ninamshukuru.
Saturday, March 13, 2021
Monday, March 8, 2021
Saturday, March 6, 2021
Wednesday, February 10, 2021
Subscribe to:
Posts (Atom)
Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...