Kitabu Kinapendwa

Tangu nichapishe vitabu vyangu mtandaoni, ninaweza kufuatilia mauzo kila siku. Nimefungua duka mtandaoni , na nimetoa ushauri kwa waandishi wengine, hasa wa-Tanzania, kuhusu uzuri na ubora wa tekinolojia hii. Ushauri wangu nimeutoa katika kitabu kiitwacho CHANGAMOTO: Insha za Jamii . Lakini inaeleweka kuwa ukiwa na wazo ukaliweka kitabuni, usitegemee kama wa-Tanzania wataliona. Huu ni ukweli ambao umesemwa tena na tena. Nami sidhani kama nina la kuongeza. Papo hapo, falsafa yangu ni kuwa ukiwa na jambo la manufaa, waeleze wengine. Kitabu changu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences ndicho chenye mauzo kuliko vingine vyote. Kila ninapoona kimenunuliwa, najiuliza ni nani huyu aliyenunua. Pengine inakuwa ni nakala moja, lakini pengine ni nakala za kutosheleza darasa. Nami sijui ni nani kaagiza. Hiki kitendawili kinanifanya niwe na dukuduku, na nafahamu kuwa sitapata jawabu. Kuna wakati zinapita siku nyingi kidogo bila mtu kukinunua, lakini wakati mwingine hali