Namshukuru Mungu kwa Kunitoa Hospitalini
Tangu tarehe 1 Februari hadi tarehe 20 Machi nililazwa katika hospitali ya Allina Northwestern Minneapolis. Sasa niko nyumbani chini ya usimamizi wa wataalam wa kuimarisha afya ya viungo. Namshukuru Mungu. Nawashukuru ndugu, jamaa, marafiki kutoka sehemu mbali mbali za dunia kwa salamu na sala zao. Nawashukuru madaktari na wauguzi. Inavyoonekana, nitakuwepo tena mitaani baada ya wiki kadhaa, Insha'Allah.