Zawadi Baada ya Mhadhara Finland

Bado nina mengi ya kusema kuhusu safari yangu ya wiki iliyopita nchini Finland, kwenye mkutano. Nina kumbukumbu nyingi, na kama nilivyowahi kusema zamani, blogu yangu ni mahali ninapojiwekea mambo yangu binafsi. Kama nilivyotamka , nilialikwa kutoa mhadhara maalum, ambao hapa Marekani huitwa "keynote address." Mada yangu ilikuwa "The Epic as a Discourse on National Identity." Baada ya kutoa mhadhara, mtoa mhadhara alikuwa anakabidhiwa ua. Ua hilo ni shukrani ya waandaaji wa mkutano. Hapa kushoto anaonekana Profesa Pekka Hakamies, mwenyekiti wa kamati ya maandilizi, ambaye aliniletea mwaliko. Tulioalikwa kutoa hiyo mihadhara maalum tulikuwa watano, kila mtu akatoa mhadhara wake kwa wakati tofauti. Mhadhara wa aina hiyo hutolewa mbele ya washiriki wote wa mkutano, na unategemewa kuweka msingi au changamoto za kujadiliwa na washiriki katika vikao mbali mbali ambamo mada mbali mbali hutolewa. Katika kuhudhuria hivyo vikao vya baadaye, nilifurahi kuw