Posts

Showing posts from November, 2020

Kitabu Kujadiliwa Chuoni St. Olaf

Image
Tarehe 8 Januari, kitabu changu, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences kitajadiliwa katika semina ya maprofesa wa chuo cha St. Olaf Nitaendesha hiyo semina ili kuleta mitazamo mipya juu ya migogoro ambayo waMarekani wana jadi ya kuijadili kama matokeo ya ubaguzi wa rangi. Suala la tofauti za tamaduni hawaliwazii. Semina yangu italenga kuleta dhana hiyo. Semina hii ni moja ya semina zinazoendeshwa kwa ufadhili wa Institute for Freedom and Community hapa chuoni. Kwa kawaida, semina hizi zinahusu mada za kitaaluma. Lakini hii semina yangu inahusu mahusiano ya watu ya kila siku, bila kupotelea kwenye mawingu ya nadharia. Profesa moja mstaafu, maarufu katika taaluma ya falsafa, baada ya kukisoma kitabu changu aliniambia kuwa tunahitaji kitabu cha aina hii. Hii ni fursa ya kukitaambulisha kitabu changu rasmi hapa chuoni, ingawa kuna watu ambao wamekuwa wakikisoma.

Alex Trebek wa "Jeopardy" Afariki

Image
Alex Trebek, mwendeshaji wa kipindi cha televisheni cha "Jeopardy" amefariki, akiwa na miaka 80.  Kwa hapa Marekani, "Jeopardy" ni kipindi maarufu sana, ila mimi sikuwa najua. Nilikuja kuzinduka tarehe 23 Novemba, 2017. Kumbe siku hiyo Trebek alikitaja kitabu changu Matengo Folktales  katika kipindi chake. Watu mbali mbali walioshuhudia walianza kupeana na taarifa na mimi nikazipata. Pongezi zilifika kwa wingi, na ndipo nami nikafahaamu maana ya kutajwa kwenye kipindi hicho.