Alex Trebek wa "Jeopardy" Afariki

Alex Trebek, mwendeshaji wa kipindi cha televisheni cha "Jeopardy" amefariki, akiwa na miaka 80.  Kwa hapa Marekani, "Jeopardy" ni kipindi maarufu sana, ila mimi sikuwa najua. Nilikuja kuzinduka tarehe 23 Novemba, 2017.

Kumbe siku hiyo Trebek alikitaja kitabu changu Matengo Folktales katika kipindi chake. Watu mbali mbali walioshuhudia walianza kupeana na taarifa na mimi nikazipata. Pongezi zilifika kwa wingi, na ndipo nami nikafahaamu maana ya kutajwa kwenye kipindi hicho.

Comments

Popular posts from this blog

Tenzi Tatu za Kale

Filamu ya "Papa's Shadow:" Fursa ya Kuitangaza Tanzania

Pesa za Majini