Sunday, November 29, 2020
Hata Balozi wa Japani Kalalamikia Uchaguzi wa Tanzania
Ule unaoitwa uchaguzi ambao ulifanyika Tanzania tarehe 28 mwezi Oktoba umelalamikiwa sana ndani na nje ya nchi. Kilichonishtua zaidi ni kuwa hata Balozi wa Japani nchini Tanzania amelalamika, kwa tamko hili:
I am troubled by the information of widespread irregularities and wrongdoings during the recent election process in this country. I am convinced that sound democracy based upon multiparty system works best to contribute to further development and prosperity of Tanzania.
(GOTO Shinichi, Ambassador of Japan to Tanzania)
Ziko nchi, kama vile Marekani, ambazo tamaduni zao hazina utata juu ya kukosoa, kulalamika, na hata kukemea. Lakini Japan haina jadi hiyo, kwa misingi ya utamaduni wao ambao umejengeka katika dhana kama "saving face." Ukilalamikiwa na Japani, lazima ujitafakari sana, na hapa ndipo mamlaka za Tanzania zimekwama.
Niliwahi kutamka katika ukurasa wangu wa Facebook kuwa mimi kama mtafiti wa tofauti za tamaduni nililichukulia tamko la balozi wa Japani kwa uzito wa pekee kwa mujibu wa utamaduni wao, nikataja kitabu katika maktaba yangu cha utamaduni wa Japani, kilitwacho "Culture and Communication," ambacho kinaonekana pichani.
Baadaye, nilifukua maktaba yangu, nikaona vitabu vingine viwili, vinavyoonekana pia pichani. Katika kuvisoma, nimejithibitishia lile wazo langu kuwa kama hata Japani inalalamika, basi hujuma zilizofanyika katika uchaguzi lazima zilikuwa mbaya kupindukia. Nakaribisha mchango wa yeyote mwenye ujuzi na elimu zaidi, kwani hili ni suala la kitaaluma, na utafiti hauwekewi mipaka.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...
-
Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwangu, ambayo ni tarehe 17 Agosti, 1951. Familia yangu, ndugu, na marafiki wamejumuika nami kushereh...
-
Leo napenda kukitambulisha kwako mdau kitabu muhimu cha ki-Swahili, Tenzi Tatu za Kale . Nilinunua nakala yangu miaka kadhaa iliyopita katik...
-
Kutafsiri kazi ya fasihi ni kazi ngumu ya kuchemsha bongo. Inahitaji ufahamu wa hali ya juu wa lugha husika, na pia hisia makini za kifasih...
No comments:
Post a Comment