Tarehe 8 Januari, kitabu changu, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences kitajadiliwa katika semina ya maprofesa wa chuo cha St. Olaf Nitaendesha hiyo semina ili kuleta mitazamo mipya juu ya migogoro ambayo waMarekani wana jadi ya kuijadili kama matokeo ya ubaguzi wa rangi. Suala la tofauti za tamaduni hawaliwazii. Semina yangu italenga kuleta dhana hiyo.
Semina hii ni moja ya semina zinazoendeshwa kwa ufadhili wa Institute for Freedom and Community hapa chuoni. Kwa kawaida, semina hizi zinahusu mada za kitaaluma. Lakini hii semina yangu inahusu mahusiano ya watu ya kila siku, bila kupotelea kwenye mawingu ya nadharia. Profesa moja mstaafu, maarufu katika taaluma ya falsafa, baada ya kukisoma kitabu changu aliniambia kuwa tunahitaji kitabu cha aina hii.
Hii ni fursa ya kukitaambulisha kitabu changu rasmi hapa chuoni, ingawa kuna watu ambao wamekuwa wakikisoma.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...
-
Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwangu, ambayo ni tarehe 17 Agosti, 1951. Familia yangu, ndugu, na marafiki wamejumuika nami kushereh...
-
Leo napenda kukitambulisha kwako mdau kitabu muhimu cha ki-Swahili, Tenzi Tatu za Kale . Nilinunua nakala yangu miaka kadhaa iliyopita katik...
-
Kutafsiri kazi ya fasihi ni kazi ngumu ya kuchemsha bongo. Inahitaji ufahamu wa hali ya juu wa lugha husika, na pia hisia makini za kifasih...
No comments:
Post a Comment