Mara moja moja, katika miaka kadhaa iliyopita, nimekuwa nikiwazia kufanya mpango wa kutafsiriwa kitabu changu, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences , kwa kiSomali. Niliwazia lugha hiyo kwa kuwafikiria waSomali waishio Marekani. Hapa kuna waSomali wengi kuliko sehemu yoyote duniani ukiachilia mbali Somalia yenyewe. Jimbo hili la Minnesota ninapoishi linaongoza kwa kuwa na waSomali wengi. Nimekuwa na mahusiano ya miaka mingi na waSomali wa Minnesota, hasa katika miji ya Faribault na Minneapolis. Nimehusika katika kuwashauri kuhusu maisha ya hapa Marekani, mifano ikiwa ni mihadhara yangu Mankato na Faribault. WaSomali ambao wamesoma kitabu changu wanakipenda sana na wananikumbusha tunapokutana. Mmoja wao ni rafiki yangu Mohamed Dini. Huyu ndiye tumekubaliana akitafsiri kitabu hicho. Yeye ni mmoja wa waSomali wachache sana wanaotambulika katika fani hiyo hapa Minnesota. Kazi hiyo itaanza mwezi huu. Ni faraja kubwa kwangu kwamba tafsiri hii itakapochapishwa itap