Andikeni Vitabu Vyenu, Viwe Bora na Maarufu Kuliko Changu
Nawashauri akina anonymous wanaokikejeli kitabu changu wakati hata hawajakisoma waandike vitabu vya mada ile ile tuone kama wataweza. Vinginevyo hao ni wapumbavu. Halafu, hakuna chuo kikuu kinachoweza kumtuza mtu cheo cha uprofesa kwa kuandika kitabu kama changu. Sio kitabu cha kitaaluma. Nimeshasema hayo tena na tena katika blogu hii.