Nawashauri akina anonymous wanaokikejeli kitabu changu wakati hata hawajakisoma waandike vitabu vya mada ile ile tuone kama wataweza.
Vinginevyo hao ni wapumbavu. Halafu, hakuna chuo kikuu kinachoweza kumtuza mtu cheo cha uprofesa kwa kuandika kitabu kama changu. Sio kitabu cha kitaaluma. Nimeshasema hayo tena na tena katika blogu hii.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Tangazo la Maongezi Yangu Books on Central, Faribault
Kwa miaka mingi, nimeongea na hadhira mbali mbali hasa kuhusu tofauti za tamaduni. Matangazo huandaliwa na kusambazwaa kabla ya mikutano. Ka...
-
Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwangu, ambayo ni tarehe 17 Agosti, 1951. Familia yangu, ndugu, na marafiki wamejumuika nami kushereh...
-
Leo napenda kukitambulisha kwako mdau kitabu muhimu cha ki-Swahili, Tenzi Tatu za Kale . Nilinunua nakala yangu miaka kadhaa iliyopita katik...
-
Kutafsiri kazi ya fasihi ni kazi ngumu ya kuchemsha bongo. Inahitaji ufahamu wa hali ya juu wa lugha husika, na pia hisia makini za kifasih...
26 comments:
Profesa usiwajli hao watu, wanaongea lkn hawajui wanachokiongea.Kama anajiamini, angejitambulisha yeye ni nani
Kwa hakika nakubaliana na emu-three kama yeye/wao ni shujaa kwa nini asisema jina lake? Wala usikonde Peofesa achana nao. Mimi nimevisoma vitabu vyako na nimevipenda na nitaendalea kuvipenda..
emu-three acha ushamba. Kwani wewe si sawa na anonymous? Hapa nadhani mngemshauri profesa awe mstaarabu na aache majivuno yasiyolingana na umri wake na elimu yake. Wote hatuwezi kuwa waandishi wa vitabu wala maprofesa. Kwanini kumkosoa profesa Mbele inakuwa kama dhambi? Si yeye yule yule aliyetwambia kuwa usomi maana yake ni kuchokoza mjadala? emu-three jina lako halisi ni nani? Mbona huweki picha yako?
Pole Profesa Mbele, Naona kidogo hapo umeghadhabika na maoni ya wanaofikiri kupitia tumboni badala kichwani hawa lengo lako wakubadilisha wawe kama wao kwa sababu wewe una-maarifa ziaid yao na pia unatumia kichwa kufikiri na kujifunza maarifa mapya na pia kuwanufaisha wenigne wasiokuwa na ujuzi maarifa kama yako...
Mungu akubarikia Pr. Mblele na endelea kwa moyo wako kujituma kuwasaidia waliopo gizani kimaarifa ni kwa wale tuu wemnye juhudi kufanya hivyo
Anon mwenzangu usimsifu profesa ujinga na upumbavu. Kwani hao unaosema wanafikiri kwa matumbo kuna maslahi gani katika hili kama siyo kushindwa kujua hata unachoandika? Unamridhisha profesa au anajiridhisha mwenye? Akubali kukosolewa. Na hiki ni kitu cha kawaida na cha faida kwa watu wanaopenda kufikiri na kujifunza hata kufundisha.
Naona anno, ni kweli unafikiria kupitia tumboni kama wewe ni hodari andika mawazo yako katika kutunga kitabu siyo kujaribu kupotosha watu kwa kujiona unaandika kitu sahihi wakati huo huo unajificha hii ni kuonesha udhaifu wa kuto-jihamini na upungufu wa maarifa ya ubunifu endelevu...tafadhali acha hayo maelezo yako ovyo ovyo kama inayoendana na namna unavyofikiria kutoka tumboni badala ya kichwani
Chakarika una tofauti gani name anon au emu-three. Kweli nyani haoni kudule. Usimsifie profesa Mbele ujinga na ubabe wa kutotaka kukosolewa. Kwani kuwa profesa ni kujua yote au ni yale yale ya maprofesa wa Kiswahili ambao wengi wao wameua elimu yetu kwa kuendekeza rushwa ya ngono na umungumtu?
Haya sasa makubwa yamefikia matusi ya nguoni tena!!!!!!!!!!
Mimi nilifundisha Chuo Kikuu Dar kuNia mwaka 1976 kwa maad ili yote asili mia 100. Tangu mwaka 1991 nimikuwa nimekuwa nikifundisha Chuo cha St Olaf hapa Marekani. Nimechukizwa na haya majungu kuhusu mambo ya rushwa. Hawezi kujitokeza mwanafunzi tangu ile 1976 awe mwanamke au mwanamke, Muislam au Mkristu, akanihusisha na rushwa au upendeleo wa aina yoyote. Aliyeandika ujumbe hapa juu ni mzushi, aone aibu sana.
Mimi ni mwalimu ambaye daima nimezingatia maadili na uchapa kazi kwa kiwango cha asili mia 100. Wanafunzi niliowafundisha chuo Kikuu Dar ni kati ya mwaka 1976 hadi 1990.
Kweli nimechukia.
Naona watu wametoa ya moyoni, kwa hali hii Prof.nitakitafuta kitabu chako nisome maana hapa siwezi kuchangia lolote mpaka nitumie ile methali ya "Asifuye mvua imemnyea"
ama "Siri ya mtungi aijuaye ni kata"
Mdau-Riyadh255252299
Pole sana Mwalimu,wewe ni Prf na huyo kiumbe anae andika vitu vichafu juu yako msamehe bure tu,hajui atendalo,samehe saba mara sabini
By Theophil Kapinga(Mwanafunzi wako}
theophilo severin hata kama wewe ni mwanafunzi wa Mbele hovyo kabisa. Kwani profesa si mtu kama watu wengine? Mbona hata ulichoongea hakionekani. Si kila profesa ni wa kupigiwa mfano. Mara hii umesahau maprofesa wa hovyo kama vile Mukandala wa UDSM ambao wako pale kutumikia mabwana zao wa kisiasa badala ya taaluma! Mjadala huu si juu ya kuandika vitabu vya kumchafua profesa Mbele bali kumekuwapo na wanaomkosoa. Ni kama umedandia mjadala na kujikomba.
Wewe anononymous aw Februari 9, acha upumbavu wako. Manna moja ya uprofesa wa kweli ni kuwa mtu unayeibua na kuchocheaa mijadala iili kuboresha taaluma. Usilete upumbavu wako hapa wa kuwa eti mimi siipendi wala sikubali kudosolewa. Utakuwa profesaa gani.
Watu ninaowaponda hapa ni walle wanaojitia kuongelea kijitabu ambacho wala hawajakiona, achilia mbali kukisoma . unadhani wajinga hao watachachangia nini. Dhana ya uprofesa naona huijui. Kuchochea na kushirki mijaadala, kukosolewa hoja na kukosoa hoja ndio uhai wa taaluma.
Na kuomba kama unanitaja mimi, sema ukweli kuhusu mimi. Mimi si profesa wa UDSM. Niko kwenye Chuo kimoja huku. Marekani, tangu mwaka 1991. Usinihusishe na wengine. Mimi ni mimi. Kama unanifahamu vizuri, niongelelee. Lakini sio unaleta upumbavu wako hapa. Uone aibu.
Ukisoma mchango wa profesa unashindwa kuona tofauti na hao anaotukanana nao. Uprofesa kweli ni kuchochea mjadala lakini si kila mjadala ni mjadala. Kinachoonekana hapa sana sana ni mashindano ya kuonyesha ujinga iwe kwa wanaokosoa au anayekosolewa. Watu wazima mnapofikia kuitana wapumbavu bila sababu na ushahidi mjue mnatumikia kile ambacho waingereza husema, Don't argue with the fool for people (wise) might not notice" Kama wahusika walionyesha ujuha na ujinga wao, profesa hakuwa na sababu ya kujibu sawa na wao. Mimi napita tu. Maana si sehemu ya mchuano huu wa kuonyeshana ubabe ambao mwisho wake ni kujikuta wote mko uchi asiwepo wa kumcheka mwenzake.
You are wasting your time if you expect me to suffer fools gladly.
Nilipita hapa siku nyingi, kumbe ule moto unaendelea.
Ila hatimaye kitaelewaka,kila la kher nyote.
Kama wote tutaandika vitabu wasomaji watatoka wapi au kila mtu asome vitabu vyake? Nadhani prof amekubali amechemsha. Napita tu. Amechemka hadi anasahau kuandika Kiswahili akidhani kiingereza kitawanyamazisha wakosoaji wake. Sijui kama hii idiom yake ya suffer fools gladly ameitumia vibaya. Ikizingatiwa kuwa hata hao anaowaona wapumbavu wanaweza kumuona juha mkubwa kwa vile anajiita profesa lakini mwenye kutoweza kufikiri sawa sawa.
Natamani mwisho wa yote tujue nani kashinda , kwa maana nani alikuwa sahihi Prof ama sie wapita njia.
Hata hivyo kila siku najifunza neno kupitia malumbano hayo.
Kama Prof hatafunga mjadala huu hadi mwisho wa mwezi, mimi binafsi nitatoa hitimisho.
Blogu yangu ni huru. Sifungii mijadala.
Naona ama profesa amechemsha. Maana yale makali na matusi aliyoanza nayo yanaelekea kumuishia kiasi cha kuanza kuongea kama profesa sasa na si mhuni wa kawaida. Natamani mjadala uendelee.
Kesha sema mjadala unaendelea,nanukuu "Sifungii mjadala"
Lakini mkumbuke pia ushauri Prof. Mbele sisi wakosoaji tunandike vitabu ile viwe maarufu sana duniani....siyo kukosoa tuu bila kuonesha uwezu wetu na pia maarifa kuweka katika maandishi shindani. Siyo kupiga kelele kama mayowe bila ushindani wa kiandishi kwa vitendo
Profesa huna haja kubishana na watu, wanasema ukibishana nampumbavu utaonekana na wewe mpumbavu watu wanaanza mabishano Kama sehemu za Baa, Kama mtu hukubali kazi ya mwenzako wachana nayo fanya yako na huna haja kupoteza muda kuja mpaka huku kukosoa kitu cha mtu alichotumia kichwa kwa uwezo na kutaka jamii isome, Professa huna haja ya kuweka history yako endelea na kazi zako na bidi ya kuuwa fikra maskini za watu, Tuanze kujipenda wanadamu tuache tabia mtu akiwa na nyumba nzuri watasema fisadi na wewe Jenga yako hujazuiliwa why uwe na kibovu? Ahmed.
Anon Ahmed. wa mwisho acha kujipendekeza. Usimshauri mwenzio upumbuvu. Huwezi kuita wakosoaji wapumbavu bila kuonyesha upumbavu wao. Nadhani unajisuta bila kujua. Kwa taarifa yako profesa Mbele hapendi anon kwa vile wanaficha majina yao. Ila wakimsifu kama ulivyofanya huwavumilia. Bila kukosoana duniani mambo yasingebadilika. Ni Mungu pekee asiyekosolewa kwa vile hawezi kuja kujibu. Wanadamu tunakosea na kukosoana ndiyo ustaarabu huo. Kwani profesa Mbele ni malaika au binadamu wa kawaida tena dhaifu saa nyingine kuliko hata hao wanaomkosoa?
Profesa Mbele inatumia kodi za wananchi wa marekani huna lolote profesa gani hapendi kukosolewa? Unakosolewa tu ili ujirekebishe uje kivengine vizuri.
Mwacheni Prof. wawatu sasa katulia,anafuatilia tamthilia ya "BUNGE LA KATIBA"
Post a Comment