Monday, March 24, 2014

Namshukuru Mungu kwa Kunitoa Hospitalini

Tangu tarehe 1 Februari hadi tarehe 20 Machi nililazwa katika hospitali ya Allina Northwestern Minneapolis. Sasa niko nyumbani chini ya usimamizi wa wataalam wa kuimarisha afya ya viungo. Namshukuru Mungu.

Nawashukuru ndugu, jamaa, marafiki kutoka sehemu mbali mbali za dunia kwa salamu na sala zao. Nawashukuru madaktari na wauguzi. Inavyoonekana, nitakuwepo tena mitaani baada ya wiki kadhaa, Insha'Allah.


12 comments:

Subi Nukta said...

Ugua pole Mwalimu.

Anonymous said...

Kila la kherihah

Anonymous said...

Kila la kheri.

Yasinta Ngonyani said...

Akanono! Nga vi, nga kumanya...Ugua pole sana Mwal.

Lyimo said...

Pole Mwalimu, ni wakati huo huo nilikuwa nikijaribu kukupigia simu bila mafanikio

Anonymous said...

Ugua Pole Prof.Mola akupe nguvu.

Anonymous said...

Pole sana Joseph Mbele, nilishangaa mbona umepotea ghafla, kila nikifungua blog yako nakutana na ile post ya kitabu. Pole sana

Rachel siwa Isaac said...

Pole sana,MUNGU azidi kukuinua na Upate kupona upesi.

simba deo said...

Pole sana Prof Mbele. Ugua pole na upone mapema.

Christian Sikapundwa said...

Profesa pole sana,waala sikuwa na taarifa yoyote ya matatizo ya kiafya yaliyokupata.
Hii ni kwa sababu ni muda mrefu sijafungua blog yangu.Lakini umenipa faraja uliposema kuwa afya yako imeanza kuimarika zaidi.
Nakutakia afya njema zaidi,ili uendele kuitumikia DUNIA yetu.

Christian Sikapundwa said...

Na mimi sasa niko nyumbani Dodoma baada ya kustaafu utumishi wa Serikali na nimekuwa mjasiriamali,kama walivyo wengine wanavyo jitahidi hulisukuma gurudumu la Taifa letu.

theophilo severin said...

pole sana Mwalimu