Posts

Showing posts from January, 2021

Africans and Americans - Embracing Cultural Differences - With Guest Pro...

Image
Image
  Huyu ni Salah Habib-Jama Mohamed kutoka Somalia, akiwa na kitabu changu  Africans and Americans: Embracing Cultural Differences . Alihitimu shahada ya kwanza hapa katika  Chuo cha St. Olaf . Salah aliniambia katikaa maongezi ya simu kuwa aliwahi kuwa na kitabu hiki akakisoma.  Alikipenda sana, ila mtu alikiazima na sasa haijulikani kiko wapi. Nilicheka niliposikia hivyo, kwani nimewasikia waMarekani nao wakilaalamika kuwa nakala zao ziliazimwa na sasa hazijulikani ziliko, kwani waazimaji huwaazimisha wengine, na hivi kitabu kutoweka. Katika ukurasa wake wa Facebook, Salah aliandika kuhusu kitabu hiki kwamba, "It is a great book and a must read allowing us to understand each other better with humor," yaani ni kitabu bora sana na muhimu kusomwa kwa namna kinavyotuwezesha kuelewana huku kikituchekesha. Nafurahi kuwa kitabu kinapendwa na wote ambao wamekisoma. Nafarijika kuwa kinapendwa na waAfrika kutoka bara lote, wanawake kwa wanaume, wa makabila na dini mbali mbali. Nafarij