Tamasha la Kimataifa Faribault, Minnesota

Jana, tarehe 10, nilishiriki tamasha la kimatafifa mjini Faribault, Minnesota. Tamasha hilo huandaliwa kila mwaka na Faribault Diversity Coalition. Miaka iliyopita, nilikuwa mjumbe wa bodi wa hiyo Coalition.

Tamasha hujumuisha maonesho ya tamaduni za watu wa mataifa mbali mbali waishio Faribault na maeneo ya jirani. Nimeshiriki tamasha hili Miaka iliyopita, na daima, inakuwa ni fursa nzuri ya kukutana na watu na kubadilishana uzoefu na mawazo kuhusu mambo mbali mbali ya dunia yetu ya utandawazi wa leo. Ninashiriki kama mwandishi na mtoa ushauri katika masuala ya taamaduni. Ninaonesha vitabu vyangu. Hii jana nilionesha pia vitabu via Bukola Oriola na mtoto wake wa miaka kumi na tatu Samuel Jacobs.

Comments

Popular posts from this blog

Kumbukumbu ya Kuzaliwa

Tenzi Tatu za Kale

Pesa za Majini