Posts

Showing posts from October, 2012

Taarifa kwa Umma Kuhusu Hatma ya MwanaHalisi

Image
Leo 28 Oktoba 2012 Mtandao wa Watetezi wa Haki za Bidamu (THRD-Coalition), wadau wanaounda mtandao huu na mwanachama mwanzilishi wa Mtandao likiwa ni shirika lenye majukumu ya ya kutetea uhuru wa habari kusini mwa Afrika (MISA-Tan) tunaendelea kwa pamoja kuonyesha kusikitishwa kwetu kwa kufungiwa kwa gazeti la Mwanahalisi. Kwa mara kadhaa sasa tunawakutanisha tena lengo likiwa ni kuendelea kuishawishi serikali ilifungulie gazeti la Mwanahalisi. Kwa vile hoja yetu ya kutaka kuliona gazeti la Mwanahalisi likiwa mitaani haijatimia basi na sisi kwa upande wetu kazi yetu bado haijatimia. Tunatambua umuhimu wa kuheshimu sheria za nchi, lakini kwa upande mwingine tunaona kwamba ipo haja ya sisi watetezi wa haki za binadamu kupitia kwenye vyombo vya habari na pia kwenye mashirika mengine yanayounda mtandao huu kuishawishi serikali kuachana na sheria gandamizi ambazo ni za kidikteta kama sheria hii ya magazeti ya mwaka 1976 ambayo hukiuka misingi ya haki za binadamu na uta

Mdau Profesa Aliyenihamasisha Kuandika Kitabu

Image
Leo nimekutana na rafiki yangu wa siku nyingi, Profesa John Greenler wa Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison . Alikuja hapa Chuoni St. Olaf na binti yake. Kama umesoma kitabu changu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences , utaona nimemtaja Profesa Greenler kwenye ukurasa wa "Acknowledgements." Profesa huyu tulifahamiana miaka yapata kumi iliyopita kwenye mikutano ya washauri wa programu ya Associated Colleges of the Midwest (ACM) ambayo hupeleka wanafunzi Tanzania. Miaka ile yeye alikuwa anafundisha Chuo cha Beloit . Wakati wa kupanga na kutathmini hali ya program kila mwaka, nachangia kwa namna ya pekee masuala yanayohusu tofauti za tamaduni, ambayo ni changamoto kwa wa-Marekani na wa-Tanzania. Kwenye mikutano yetu hiyo, nilikuwa, na bado niko, mstari wa mbele kufafanua matukio mbali mbali na mambo mengine wanayokumbana nayo wanafunzi katika kuishi na wa-Tanzania. Profesa Greenler alipochukua fursa ya kupeleka wanafunzi Tanzania, aliniomba niandik

Ngoma Nzito Marekani: Tanzania Je?

Image
Pamoja na mapungufu yake yote, siasa Marekani ina mambo kadhaa ya kupigiwa mfano. Kinachonivutia zaidi ni mijadala inyofanyika baina ya wagombea kabla ya uchaguzi. Leo, kwa mfano, tumeshuhudia pambano la tatu baina ya Obama na Romney Mijadala ya namna hii inawapa wapiga kura fursa ya kuwasikiliza wagombea. Vile vile naiona kama namna ya kuwaheshimu wapiga kura. Mfumo wa Marekani unatambua kuwa wapiga kura wana haki ya kuwasikia wagombea wakiongelea masuala kadha wa kadha katika kupambanishwa na wapinzani wao. Ninakerwa ninapokumbuka mambo yalivyo kwetu Tanzania. Ninakerwa nikikumbuka jinsi CCM ilivyotoroka midahalo mwaka 2010. Ni dharau kwa wapiga kura. Tatizo ni jinsi wapiga kura wengi walivyo mbumbumbu, wasitambue kuwa hili lilikuwa dharau. Walipiga kura kama vile hawajadharauliwa. Hebu fikiria mambo yangekuwaje ule mwaka 2010 iwapo Kikwete angepambana na Slaa katika midahalo mitatu hivi, ambayo ingeonekana katika televisheni na kusikika redioni. Lakini tulinyimwa fursa hii,

Mtume Hatetewi kwa Dhulma na Ujinga

Mtume Hatetewi Kwa Dhulma Na Ujinga Uislamu Na Shari'ah Zake Imekusanywa Na: ‘Uthmaan Beecher Imefasiriwa Na: Abu Suhayl Shukrani njema zinamstahili Allaah, rahmah na amani zimuendee Mtume wetu Muhammad, na aali zake na maswahaba zake na Waislamu wote. Ama baada ya hayo Hakuna Muislamu ambaye anaweza kukubaliana na kutukanwa, kudhalilishwa, kudhauruliwa na kusingiziwa mambo mabaya Mtume wetu mpendwa (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Ma-Imaam wa Ahlus-Sunnah kama Imam Maalik, al-Layth, Ahmad, na Ash-Shaafi’iy, wamekubaliana kwa pamoja kwamba yeyote atakayemvunjia heshima, kumtukana au kumdhalilisha au kumtia ila Mtume wetu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) atakuwa amekufuru, na adhabu inayomstahili kwa yule anayeishi katika dola ya Kiislamu na akafanya hivyo ni kifo, adhabu ambayo itakuwa katika mikono ya mtawala wa Kiislamu. Hapana shaka kwamba mashambulizi ya aina hii kwa Mtume wetu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) yatasababisha hasir

Ziara Chuoni Lake Forest

Image
Juzi nilienda chuoni Lake Forest , maili kadhaa kaskazini ya Chicago. Nilishinda pale jana yote. Hapa kushoto ni picha ya Student Center, ambamo wanafunzi hupata chakula na kupumzika. Nilienda na profesa kutoka chuo cha Wheaton, kutathmini programu ya Area Studies . Hii ni programu ambayo inampa mwanafunzi fursa ya kusoma masomo mbali mbali kuhusu sehemu moja ya dunia, kama vile Mashariki ya Kati, Amerika ya Kusini, Afrika, au Asia. Anasoma masomo kama historia, siasa, uchumi, na hata lugha ya sehemu husika. Pia, ikiwezekana, anaenda kusoma katika sehemu hiyo. Utaratibu wa kutathmini programu na idara mbali mbali za masomo ni wa kawaida katika vyuo vya Marekani. Hufanyika baada ya miaka kadhaa; yaweza kuwa saba, au kumi, na kadhalika. Shughuli ya kutathmini programu huhitaji mtu usome taarifa mbali mbali zinazoelezea malengo na utaratibu wa masomo hayo, ratiba za masomo, na tathmini kutoka kwa wanafunzi waliosoma masomo hayo. Pia kuna taarifa kuhusu wafundishaji, elimu yao, masom

Wa-Kristu Tunamwabudu Allah!

Najua kuwa kichwa cha habari hii kitawashtua wengi. Huenda watu watasema nimechanganyikiwa au nimekufuru.  Huenda wako watakaouliza, "Iweje wa-Kristu wawe wanamwabudu Allah?" Kwa siku kadhaa, nimekuwa nikijuliza suali: Je, wa-Arabu ambao ni wa-Kristu wanatumia jina gani kumtaja Mungu? Ninafahamu kuwa kuna mamilioni ya wa-Arabu ambao ni wa-Kristu, huko Mashariki ya Kati na sehemu zingine za dunia. Sasa je, Mungu wanamwitaje kwa ki-Arabu? Nimefanya uchunguzi kidogo nikagundua kuwa jina wanalotumia, ni hilo hilo wanalotumia wa-Islam, yaani Allah. Hili ndilo neno lililopo katika ki-Arabu. Katika Biblia ya ki-Arabu, ambayo huitwa "al-Kitab al- Muqadis" yaani Kitabu Kitakatifu, Mungu anaitwa Allah muda wote. Nilivyogundua hivyo nimetambua jinsi wengi wetu tulivyopotea, kwani tunaamini kuwa Allah ni tofauti na Mungu. Tunalumbana hadi tunatokwa jasho, na povu mdomoni, kwa umbumbumbu wa kutojua lugha. Taarifa iliyonifungua macho ni hii hapa .

Mwalimu Nyerere Aliiogopa CCM

(Katika kumkumbuka Mwalimu Nyerere, naileta makala yangu, "Mwalimu Nyerere Aliiogopa CCM," ambayo nimeshaichapisha katika hii blogu yangu mara kadhaa) Ingawa alikuwa mwanzilishi wa CCM, kwa nia njema ya kuendeleza mapinduzi katika nchi yetu, miaka ilivyozidi kwenda Mwalimu Nyerere alishuhudia jinsi CCM ilivyobadilika na kuwa mzigo kwake na pia tishio kwa usalama wa Taifa. Mwaka 1993 Mwalimu alichapisha kitabu kiitwacho Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania (Harare: Zimbabwe Publishing House, 1993). Pamoja na mambo mengine katika kitabu hiki, Mwalimu alisema kuwa kuna kansa katika uongozi wa CCM. Nanukuu baadhi ya maneno yake: Chama cha Mapinduzi, kwa sababu ya uzito wa historia yake, hadhi ya jina lake, mfumo wa wavu wake, mazoea ya watu, na ubovu wa Vyama vya Upinzani, kinaweza kuchaguliwa na Watanzania, pamoja na kansa ya uongozi wake. Au watu wanaweza wakachoka, wakasema, "potelea mbali:" wakachagua Chama cho chote, ilimradi tu watokane na kansa ya uongozi wa

Leo Nimehudhuria Tamasha la Vitabu Twin Cities

Image
Leo nilikuwa mjini St. Paul, kushiriki Twin Cities Book Festival. Kama nilivyowahi kuelezea, maonesho haya hufanyika kila mwaka, wakati kama huu. Nililipia ushiriki wangu nikitumia jina la "Africonexion" ambalo ni jina la kikampuni changu ambacho nimekuwa nikikijenga pole pole. Tofauti na miaka iliyopita, maonesho ya leo yalifanyika sehemu iitwayo State Fairgraounds. Miaka iliyopita maonesho haya yalikuwa yakifanyika Minneapolis Community and Technical College, mjini Minneapolis. Miji ya St. Paul na Minneapolis inagusana, na mgeni huwezi kujua mpaka ni wapi. Kama kawaida, watu walikuwa wengi, tangu kuanza kwa maonesho hadi kumalizika. Kama ambavyo nimesema tena na tena, inavutia kuona jinsi wa-Marekani wanavyothamini matamasha ya vitabu. Wanaanza kufika hata kabla milango haijafunguliwa. Vijana, wazee, wake kwa waume wanahudhuria. Pia wako wanaokuja na watoto. Nimeongea na watoto kadhaa waliofika na wazazi wao kwenye meza yangu. Baba m

Mwandishi Mo Yan Apata Tuzo ya Nobel

Image
Nimesoma taarifa mtandaoni sasa hivi kuwa mwandishi Mo Yan wa China ameikwaa tuzo ya Nobel katika fasihi kwa mwaka huu. Sikuwahi kusikia jina la mwandishi huyu. Hili si jambo la kujivunia. Ni kweli kuwa kuna waandishi wengi sana maarufu hapa duniani. Sio rahisi kwa mtu kuwa amesoma au anasoma maandishi ya wale wote wanaopata tuzo ya Nobel. Kwa mfano, mwaka 2006 tuzo ya Nobel katika fasihi aliitwaa Orhan Pamuz wa u-Turuki. Sidhani kama niliwahi kusikia hata jina lake kabla. Nilijisika vibaya kuwa sina hata ufahamu wa mwandishi huyu. Hatimaye nilijikakamua nikanunua kitabu chake kimojawapo. Nadhani kwa sasa ninavyo viwili, ila bado sijapata wasaa wa kuvisoma. Inapotokea habari ya mwandishi kupata tuzo kama hii ya Nobel, nchi zingine hufanya hima kutafsiri maandishi ya washindi hao, iwapo lugha yao ni tofauti. Watatafsiri maandishi ya Mo Yan katika lugha zao. Tanzania hatuna utamaduni huo. Tunadanganyana kuwa sisi ni mabingwa wa ki-Swahili, ambacho kwa kweli hatukitumii kwa nidh

Taarifa ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Juu ya Kifo cha Daudi Mwangosi

Image
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA(THBUB) YATOA TAARIFA YAKE YA KIFO CHA DAUDI MWANGOSI Mwenyekiti wa Tume Ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora Jaji Kiongozi (Mstaafu) Amiri Ramadhan Manento (katikati) akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani jijini Dar es Salaam Oktoba 10,2012 wakati akitoa muhtasari wa taarifa ya Uchunguzi wa Tume yake kuhusu tukio lililopelekea kifo cha Daudi Mwangosi kilichokea Septemba 2, 2012 kijijini Nyololo. Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mahfoudha.A. Hamid na kulia ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka Tume hiyo Florida Kazora. Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Jaji Kiongozi (Mstaafu) Amiri Ramadhan Manento akionyesha taarifa kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu Muhtasari wa wa Taarifa ya tume yake ya Uchunguzi wa tukio lililopelekea kifo cha Mwandishi wa habari

Programu za Kupeleka Wanafunzi Nje

Image
Leo hapa chuoni St. Olaf, tumefanya shughuli ya kutangaza programu zinazowapeleka wanafunzi kwenye masomo nje ya chuo hapa Marekani na nchi za nje. Ni shughuli ambayo tunafanya kila mwaka, wakati kama huu. Tunawapa wanafunzi fursa ya kuzifahamu programu hizi. Mimi ni mshauri wa program ya ACM Tanzania , ACM Botswana , na Lutheran Colleges Consortium for Tanzania (LCCT) . Chuo cha St. Olaf kinaendesha programu nyingi sehemu mbali mbali duniani. Pia kinashiriki katika programu za vyuo na taasisi nyingine, kwa maana kwamba wanafunzi wa chuo hiki wanayo fursa ya kujiunga na programu zile. Kuna programu za mwezi mmoja, muhula mmoja, na hata mwaka. Chuo cha St. Olaf ni maarufu hapa Marekani kwa programu zake hizi za kupeleka wanafunzi nje. Wanafunzi wengi huja kusoma hapa kwa sababu ya fursa hizo. Nami kama mdau mkubwa wa masuala ya kujenga mahusiano baina ya mataifa na tamaduni mbali mbali nimejizatiti sana katika shughuli ya ushauri wa programu hizi. Mara

Nimejipatia iPad

Image
Pamoja na kuwa mimi ni mmoja wa wale watu wa zamani tuliozaliwa na kukulia kijijini na ambao tunababaishwa na hizi tekinolojia zinazofumuka kwa kasi, nimejipatia kifaa kiitwacho iPad siku chache zilizopita. Nimenunua iPad Wi-Fi+3G. Nilishinikizwa na binti yangu Zawadi. Ndiye anayenisukuma niende na wakati. Tangu ninunue kifaa hiki, yapata wiki mbili zilizopita, nimekuwa katika kujifunza namna ya kukitumia, maana kina mambo mengi sana. Angalau naweza kutembelea mitandao, kutuma na kupokea barua pepe, na kupiga picha na kisha kuziangalia. Hata video najua namna ya kupiga. Kitu ninachotaka kukifanya hima ni kuingiza vitabu pepe kwenye hii iPad, nikianzia na kitabu changu kiitwacho Africans and Americans: Embracing Cultural Difference s , ambacho wadau wanakipata mtandaoni, pamoja na vitabu vyangu vingine , kwa njia hiyo. Kidogo najisikia vibaya kwamba nilikiweka kitabu hiki katika muundo wa kitabu pepe na wadau wanakinunua, wakati mimi mwenyewe sikuwa na kifaa cha kuingizia v

Unaweza Kushindwa Mtihani wa Dini Yako

Siku za hivi karibuni kumekuwa na zogo kubwa Tanzania kutokana na wanafunzi kushindwa mtihani wa dini yao. Sikufuatilia vizuri undani wa kisa hicho na siwezi kukiongelea. Badala yake, napenda tu kuongelea suala la kinadharia la mtu kushindwa mtihani kuhusu dini yake. Tunapokuwa kanisani au msikitini, kwenye mihadhara ya dini au madrassa ya dini, tunafundishwa dini yetu kwa maana ya kwamba tunaelekezwa tuelewe dini inasema nini ili tuwe waumini bora. Suala ni kutujenga kiimani na kimaisha kwa mujibu wa dini yetu, kutokana na yale anayofundisha padri, imam au sheikh. Mambo ni tofauti tunapokuwa shuleni au chuoni. Mimi ni mwalimu, na ingawa sifundishi dini, napenda kusema kuwa darasani hatufundishi kwa lengo la kujenga imani ya watu kwenye dini yao. Labda kabla sijaenda mbali, nifafanue kuwa naongelea kiwango cha chuo. Kwenye madarasa ya mwanzo, ambako tunawafundisha watoto, naamini tunategemewa kuwafundisha dini kwa lengo la kuwafanya wawe waumini bora. Lakini, lengo langu hapa ni

Mkutano wa Cheetah Development

Image
Jana jioni nilihudhuria shughuli ya Cheetah Development mjini St. Paul. Cheetah Development ni mtandao wa watu wanaojishughulisha na miradi ya maendeleo Afrika Mashariki, hasa Tanzania. Nilijulishwa kuhusu mtandao huu na rafiki yangu Mzee Paul Bolstad, ambaye anaonekana kushoto kabisa hapa pichani. Yeye na huyu mwingine ni marafiki wa tangu zamani. Wote ni wapenzi wakubwa wa Tanzania. Mzee Bolstad alizaliwa na kukulia Tanzania, na huyu mwenzake walikuwa wote katika programu ya Peace Corps Tanzania walipokuwa vijana. Walihudhuria watu wengi Kulikuwa na hotuba na maonesho ya shughuli mbali mbali za Cheetah Development. Kikundi cha kwaya kiitwacho imuka , kutoka Bukoba, ambacho kiko katika ziara hapa Marekani, kilitoa burudani. Tulikutana wa-Tanzania kadhaa, tukabadilisha mawazo na kupiga michapo.

Museum Africa, Johannesburg

Image
Nilipokuwa Johannesburg, mwezi Juni, nilitembelea sehemu kadhaa za jiji hilo. Hiyo ilikuwa ni tarehe 17. Kwenye kitongoji cha Newton niliweza kuona taasisi kadhaa, mojawapo ikiwa Museum Africa . Hili ni jumba la makumbusho ambamo wamehifadhi vitu vingi vya kihistoria. Kwa mfano, kuna picha nyingi sana na maelezo kuhusu siku za mwanzo kabisa za Johannesburg, kwa mfano usafiri ulivyokuwa, simu, nyumba ya mwanzo ya ibada, na idara ya mwanzo kabisa ya zimamoto, ambayo haikuwa na vifaa tunavyovijua leo. Ni kumbukumbu murua sana kwa yeyote anayeithamini historia. Museum Africa sio kumbukumbu pekee eneo hili la Newton. Ziko nyingine pia. Ukiingia humo ukakaa saa moja, mbili, au zaidi ukiangalia na kusoma yaliyomo, utatoka ukiwa umeelimika sana. Insh'Allah nitaleta taarifa zaidi.

Vitabu Nilivyonunua Leo

Image
Leo baada ya mizunguko kwenye mji wa Apple Valley, niliingia katika duka la vitabu la Half Price Books, ambalo nimeshaliongelea kabla . Kama ilivyo kawaida hapa Marekani, kwenye duka la vitabu, hawakosekani wateja, na mara kwa mara kunakuwa na msongamano. Leo nilinunua vitabu vitano. Kimoja ni Three Plays cha Sean O'Casey. Huyu ni mwanatamthilia maarufu wa Ireland. Nilipokuwa nasoma Chuo Kikuu Dar es Salaam, 1973-76, tulisoma tamthilia yake mojawapo iitwayo Purple Dust . Ilituvutia sana. Ingawa nahisi kitabu cha Three Plays ninacho katika shehena ya vitabu vyangu vilivyopo Tanzania, nimeona ni vema nikawa na nakala nyingine. Sean Ocasey alikuwa mtu wa ajabu, kwa jinsi ambavyo alivyokuwa mtoto maskini wa mitaani, akajielimisha mwenyewe hadi kufikia hadhi ya kuwa mwandishi anayeheshimiwa sana duniani. Kitabu kingine nilichonunua ni Reality, Man and Existence: Essential Works of Existentialism , kilichohaririwa na H.J. Blackham. Kitabu hiki kina maandishi ya Kierkegaard, S