Posts

Showing posts from January, 2012

Mwandishi Shafi Adam Shafi

Image
Tanzania tuna waandishi wengi maarufu katika lugha ya ki-Swahili. Mmoja wao ni Shafi Adam Shafi, kutoka Zanzibar, ambaye anaonekana nami pichani hapa kushoto. Tulikuwa New Africa Hotel, Dar es Salaam mwaka 2004 wakati wa tamasha la vitabu. Shafi Adam Shafi anafahamika sana kwa riwaya zake. Riwaya aliyoichapisha kwanza ni Kasri Ya Mwinyi Fuad (Tanzania Publishing House, 1978). Ilikuwa maarufu tangu mwanzo. Sikupata muda wa kuisoma. Halafu, mwaka 1980 niliondoka Tanzania, kuwenda masomoni Marekani, hadi mwaka 1986. Baada ya kukaa Marekani miaka sita hiyo, nilivyorejea Tanzania nilifanya juhudi ya kujipatia vitabu vya ki-Swahili. Nilinunua nakala ya Kasri Ya Mwinyi Fuad tarehe 28 Oktoba, 1987, ikasainiwa na Shafi Adam Shafi tarehe 29. Nina risiti ya kununulia kitabu, kutoka Tanzania Publishing House. Kwa hivyo, nina ushahidi kuwa nimeonana na Shafi Adam Shafi mara mbili. Ingawa mara kwa mara ninapoongelea vitabu katika blogu zangu huwa naandika kuhusu yaliyomo, na uchambuzi w

Africonexion: Kampuni Chipukizi

Image
Mwaka 2002 nilisajili kampuni katika jimbo la Minnesota ambayo niliita Africonexion . Nilichagua aina ya usajili iitwayo "sole proprietorship." Yaani mmiliki na mhusika mkuu ni mimi. Nilianzisha Africonexion kama chombo cha kushughulikia elimu kuhusu tamaduni duniani, kwa kuandika, kuchapisha, na kuuza vitabu, na kutoa mihadhara na ushauri kwa watu binafsi, mashirika, taasisi, makampuni, na kadhalika, kama ninavyoripoti mara kwa mara katika blogu zangu. Africonexion ni kampuni ndogo sana kwa wakati huu, kwa maana kwamba sina timu ya wafanyakazi au washiriki. Lakini nimeitumia vizuri kama fursa ya kujielimisha, kwa kuzingatia kuwa elimu ni mtaji bora kuliko hata fedha. Shughuli zote ninazofanya, iwe ni kuandika au kutoa mihadhara au ushauri kwa watu binafsi, ni kama shule kwangu. Hii picha hapa kushoto ilipigwa wakati wa maonesho fulani Brooklyn Park, Minnesota. Ninataka kuipeleka kampuni hii Tanzania na kwingineko. Nimeshaendesha warsha Dar es Salaam , Zanzibar na Pem

Mfanya usafi akamatwa akimlawiti mtoto msikitini

Habari hii inahuzunisha, nikizingatia jinsi mtoto huyu alivyohujumiwa maisha yake na haki zake za kibinadamu, nikizingatia uchungu wa mama yake, ndugu, jamaa, marafiki na wapenda haki. Habari hii inapaswa kutangazwa, ijulikane, ili angalau iwe faraja kwa mtoto huyu na mama yake, kwamba tuko tunaojali utu na haki, na tuko pamoja nao. Habari hii imetokea msikitini. Hivi juzi, wanafunzi wa ki-Islam walipoandika waraka wakiorodhesha hujuma walizosema wanafanyiwa wa-Islam mashuleni, niliandika ujumbe kuwaunga mkono katika kulaani hujuma hizo. Soma hapa . Nilisukumwa na maadili ya kuzingatia haki, niliyofundishwa katika imani yangu ya u-Katoliki. Sasa basi, ni muhimu wa-Islam, wa-Kristu, na wengine wote tuungane kumpigania mtoto huyu aliyelawitiwa msikitini, na watoto wengine wanaotendewa vitendo hivi, na wengine wote wanaohujumiwa haki zao. Tuungane kukemea maovu yote na kupigania haki za wote. Ni lazima tufanye hivyo, ili angalau kumpunguzia mtoto huyu matatizo ya kisaikolojia ambayo ya

Maandamano ni Mpango wa Makafiri--'Allaamah al-Fawzaan

Image
Video hii imenisisimua akili. Sikujua kuwa maandamano ni mpango wa makafiri na kwamba hakuna maandamano katika u-Islam

Mwandishi Lazima Awe Msomaji Sana

Yule mwandishi maarufu sana, Ernest Hemingway, alikuwa na mawazo ya kusisimua kuhusu masuala mbali mbali, likiwemo suala la uandishi. Aliandika sana kuhusu uandishi: mbinu za uandishi, uandishi bora, changamoto za uandishi na namna ya kuzikabili, raha na machungu ya kuandika. Aliongelea kazi za waandishi mbali mbali, na hakuficha hisia na mtazamo wake kuhusu ubora au mapungufu ya waandishi hao. Kuna mengi sana ya kuongelea, kuhusu suala hilo la Hemingway na uandishi. Lakini hapa nataka kutaja jambo moja tu, nalo ni kauli ya Hemingway kwamba mwandishi ana wajibu wa kusoma kazi za waandishi wote waliomtangulia, ili ajue kazi inayomkabili ya kuwafunika hao waandishi. Napenda kunukuu maneno ya Hemingway aliyomjibu kijana kutoka Minnesota aliyemfuata Hemingway umbali mkubwa ili kuuliza masuali kuhusu uandishi. Kiutani, Hemingway alimpa kijana huyo jina la Mice. Mice alimwuliza Hemingway masuali mengi, ila suali ninalotaka kulileta hapa ni, "What books should a writer have to read?

Naikumbuka Matema Beach

Image
Tanzania ina sehemu nyingi zinazopendeza sana, nami nimebahatika kuziona baadhi ya sehemu hizo. Mwaka jana, kwa mfano, nilipata bahati ya kufika Matema Beach, pwani ya kaskazini ya Ziwa Nyasa. Ni sehemu nzuri sana kwa mapumziko. Imetulia na haina msongamano na misuguano kama ya Dar es Salaam. Hapa kushoto naonekana nimetulia kwenye bembea, nikifaidi upepo mwanana. Huyu binti ni mmoja wa wanafunzi wawili niliowaleta hapo kwenye ziara ya kuifahamu nchi. Ukifika ufukweni hapo, unaweza kujikalia mahali chini ya mti, unapiga mbonji, kama wasemavyo watoto wa vijiweni, au ukawa unasoma kitabu, kupiga michapo na wenyeji, au kuangalia Ziwa na mitumbwi ipitayo humo. NImeandika mara kadhaa kuhusu Matema Beach katika blogu zangu, kwa mfano hapa na hapa , na napangia kuendelea kuandika.

Kitabu cha m-Tanzania Kuhusu Usimamizi wa Fedha

Image
Hatimaye, nimejipatia na kusoma nakala ya kitabu kiitwacho Taking Control of Your Money , kilichoandikwa na Juanita Puja Kilasara . Huyu ni binti m-Tanzania ambaye amejipambanua katika fani ya uhasibu na masuala ya fedha kwa ujumla. Habari za kitabu chake hiki niliziona kwanza katika tovuti ya wavuti , kwani kwenye ukurasa wa mbele pana sehemu inayotangaza vitabu vya wa-Tanzania. Kitabu hiki kinaeleza kwa njia rahisi masuala mbali mbali ya kuzalisha fedha na matumizi ya fedha kwa namna ya kumsaidia mtu kuwa mwangalifu na kumfanya asonge mbele kimaisha. Kuna mawaidha mengi ya manufaa, hata katika masuala ya kuanzisha na kuendesha biashara na shughuli zingine za kujipatia kipato. Kwa kuzingatia mabadiliko ya dunia, hasa katika tekinolojia ya mawasiliano, kitabu hiki kinatoa dokezo mbali mbali za kumwezesha mtu kutumia fursa zilizopo mtandaoni. Ingekuwa vijana wa Tanzania wana mazoea ya kusoma vitabu, wakawa wanasoma vitabu kama hiki, hata suala la ajira wangeliangalia kwa upeo tofauti

Kumbukumbu ya Martin Luther King Imefana

Image
Kumbukumbu ya Martin Luther King, Jr. niliyohudhuria leo Chuoni Concordia imefana sana. Watu wengi walihudhuria, wakajaza ukumbi mkubwa sana wa chuoni hapo uitwao Gangelhoff. Kulikuwa na hotuba kadhaa za watu mashuhuri katika jamii na taasisi na serikali. Hapa kushoto anaonekana Askofu William Watson, III, ambaye ndiye alikuwa mtoa mada mkuu. Hotuba zilisisitiza mambo muhimu aliyofanya na kusema Martin Luther King, Jr. Wasemaji walikumbushia wosia wake katika masuala kama haki, usawa, na elimu. Walihudhuria watu wa kila aina: wa rangi na mataifa mbali mbali, watoto, watu wazima, na wazee, wake kwa waume. Hapo mtu ulijionea mwenyewe kuwa kweli Martin Luther King alikuwa mtu wa pekee sana, ambaye katika maisha yake aligusa mioyo ya watu sana na bado anawagusa na ataendelea hivyo kwa vizazi vijavyo. Kulikuwa na vikundi kadhaa vilivyofanya maonesho. Waliburudisha kwa nyimbo, muziki, na staili za kucheza. Hapa kushoto ni kwaya ya watoto wavulana, ambayo ni ya watawa wa-

Januari 16, Kumbukumbu ya Martin Luther King,Tukutane St. Paul

Tarehe 16 Januari ni kumbukumbu ya Martin Luther King hapa Marekani. Zitafanyika shamrashamra nyingi sehemu mbali mbali. Kwenye miji kama Minneapolis na St. Paul, Minnesota, itakuwa vigumu hata kuamua wapi kwa kwenda. Lakini mimi nilishajisajili kama mshiriki wa maonesho yatakayofanyika Chuoni Concordia , mjini St. Paul. Pamoja na waandishi wengine, tutakuwa pale na vitabu vyetu, tukikutana na wadau na kubadilishana mawazo, kuanzia saa 3:30 asubuhi hadi saa 9 alasiri. Nafurahi kwamba miaka ya karibuni nimefanya juhudi ya kusoma habari za Martin Luther King na baadhi ya maandishi yake, hadi kufahamu jinsi alivyothamini elimu, sawa na Mwalimu Nyerere, na jinsi alivyotufundisha kujali usawa na haki za binadamu wote. Wala hakuwa upande wa watu weusi tu, kama wengi wanavyoamini. Nimegundua kuwa wengi, hata hao wa-Marekani Weusi ambao wanapenda sana kumtaja na kumpigia mfano, hawamwelewi vizuri Martin Luther King. Nangojea kwa hamu kubadilishana mawazo na hata kulumbana na umati wa watu

Nimerudi kutoka Chuoni Gustavus Adolphus

Image
Leo nilienda Chuoni Gustavus Adolphus kutoa mhadhara katika darasa la Profesa Paschal Kyoore. Niliandika kuhusu habari hii hapa . Somo wanalosoma ni "African Tricksters." Wakati huu wanasoma kitabu changu cha Matengo Folktales , na niliona wanazo nakala. Katika mhadhara wangu, uliodumu dakika 50, nilijikita katika kufafanua dhana mbali mbali zinazotumika katika utafiti na uchambuzi wa somo hili, ambazo chimbuko lake ni katika utafiti uliofanywa Ulaya, na jinsi dhana hizi zilivyopachikwa katika masimulizi ya sehemu zingine za dunia, kama vile Afrika. Nilihoji uhalali wa jambo hilo, ambalo tumelirithi na tunaliendeza. Baada ya mhadhara wangu, tulikuwa na kipindi cha masuali, kilichodumu yapata dakika 40.

Kitabu Kinapatikana Chuoni Saint Benedict, Minnesota

Image
Nimeona taarifa leo kuwa kitabu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences kinapatikana katika duka la vitabu la Chuo cha Saint Benedict , Minnesota. Nakumbuka kuwa niliwahi kutoa mihadhara miwili katika chuo hiki, kuhusu vitabu vyangu viwili. Mhadhara mmoja niliuelezea hapa . Mwanafunzi mmoja aliuongelea mhadhara wangu mwingine, kuhusu hiki kitabu cha Africans and Americans katika blogu yake .

Nimeenda Maktaba ya Southdale, Edina.

Image
Leo nilienda mjini Edina, kwenye maktaba ya Southdale . Nilikwenda kukutana na mama mmoja m-Marekani Mweusi, ambaye ninamsaidia kuchapisha kitabu chake kwa kutumia tekinolojia ya uchapishaji mtandaoni, kama ninavyochapisha vitabu vyangu . Niliposogea kwenye jengo hilo, niliona magari mengi yamepaki. Ni kama inavyokuwa kwenye sherehe nchini Tanzania. Niliona watu wakiingia na kutoka, wakiwemo wazee. Hii ni kawaida hapa Marekani. Hapo mlangoni, nilipishana na wazee wawili wakitoka, mwanamme na mwanamke, wazee sana, na huyu mwanamme alikuwa anatembelea mkongojo. Pamoja na uzee wote huu, wanaona umuhimu wa kwenda maktaba. Humo ndani, kama kawaida, kulikuwa na watu wengi wakisoma, kuazima au kurudisha vitabu, na wengine kwenye kompyuta na kwenye sehemu za kusikilizia vitabu, maana siku hizi vitabu vinapatikana vikiwa vimerekodiwa katika kanda. Ukiangalia maelezo ya maktaba hii Southdale , utaona kuwa wanavyoitumia maktaba hii inaendana vizuri na yale aliyoyawazia na kuyatamka Mwalimu Ny

Mabepari wa Venisi: Tafsiri ya Julius Nyerere

Image
Wiki kadhaa zilizopita, mawazo yangu yalitekwa sana na kumbukumbu za tafsiri za tamthilia za Shakespeare zilizofanywa na Julius Nyerere. Nilipata hamu ya kuziangalia na kuzisoma. Kwa kuanzia, niliagiza nakala ya Mabepari wa Venisi . Kama nakumbuka sawa sawa, tulisoma The Merchant of Venice tulipokuwa kidatu cha nne. Tulikuwa tunafahamu ki-Ingereza kiasi cha kuweza kusoma na kuelewa maandishi hayo ya Shakespeare. Ni tofauti na leo, ambapo uvivu na uzembe vimesababisha ufahamu wa ki-Ingereza udidimie sana na hata kutoweka. Uvivu huo unajitokeza pia katika ufahamu wa ki-Swahili. Nyerere aliichapisha tafsiri yake mwaka 1969, muda mfupi tu baada ya Azimio la Arusha. Kwa hivi, tafsiri yake ilikuwa na mvuto wa pekee miongoni mwetu, kwani tulikuwa tunavutiwa na nadharia za ujamaa. Hata neno mabepari lilikuwa likitumika sana, sambamba na maneno kama mabwanyenye. Ilikuwa rahisi kuelewa kwa nini Nyerere aliamua kuitafsiri tamthilia hii ya Shakespeare. Kwa kutumia tabia, fikra, na kauli za

Mtu Anapobadili Dini

Blogu yangu hii iinashughulika na masuala ya aina aina, likiwemo suala la dini. Leo napenda kuongelea suala la watu kubadili dini. Watu wengi wanabadili dini. Nikitoa mfano wa wa-Islam na wa-Kristu, wa-Kristu kwa maelfu wanabadili dini na kuwa wa-Islam, na wa-Islam kwa maelfu wanabadili dini na kuwa wa-Kristu. Kuna taarifa nyingi za watu hao mtandaoni. Katika mtandao wa YouTube, unaweza kuwasikiliza watu wa aina hiyo wakijieleza. Kwa mfano, unawasikia watu wakielezea jinsi dini ya u-Islam ilivyoshindwa kukidhi mahitaji yao ya kiroho na kadhalika. Na unawasikia wengine wakielezea jinsi dini ya u-Kristo ilivyoshindwa kukidhi mahitaji yao ya kiroho na kadhalika. Nimewasikiliza baadhi kutoka pande zote, na nimeona jinsi wanavyoongea kwa masikitiko na hata jazba kuhusu dini walizozihama. Watu hao wanajisikia kuwa kubadili dini kumewapa mwanga na amani moyoni. Kama nilivyosema, taarifa hizi zimezagaa mtandaoni. Sijui unajisikiaje endapo mtu wa dini yako akihamia dini nyingine. Wa-Islam wa

Maongezi na Wanafunzi wa Gustavus Adolphus

Image
Leo nimeongea na wanafunzi wa Chuo cha Gustavus Adolphus ambao wanaenda Tanzania wiki hii kujifunza masuala ya afya na matibabu katika utamaduni tofauti na ule wa Marekani. Kama nilivyoelezea katika blogu hii , nilialikwa na Profesa Barbara Zust, nikaongee na wanafunzi hao kuhusu masuala ninayoongelea katika kitabu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences " . Pichani kushoto, Profesa Zust ni kati ya waliosimama, wa nne kutoka kulia. Profesa Zust ni mmoja wa walimu hapa Marekani ambao wanakipenda na kukitegemea kitabu hiki. Nami nashukuru kwa jinsi kinavyowasaidia walimu na wanafunzi wao. Mimi mwenyewe kama mwalimu siwezi kukaa na kutulia, bali natambua na kuzingatia wajibu wa kuendelea kutafiti na kuandika. Leo, nilianza kwa kujitambulisha kwa kuelezea maisha yangu kwa ufupi hadi nilivyosoma Marekani na nikazingatia zaidi mchakato ulionifikisha kwenye kuandika kitabu hiki. Wale waliokisoma watakumbuka kuwa nimeelezea kiasi mchakato huo mwanzoni mwa kitabu.