Posts

Showing posts from August, 2020

Tundu Lissu, Serikali ya CCM, na Ushoga

Kwa kuzingatia kuwa kuna upotoshaji mwingi kuhusu msimamo wa Tundu Lissu juu ya ushoga, napenda kusema kuwa msimamo wake unafanana na msimamo wa serikali ya CCM kuhusu ushoga. Katika mahojiano kwenye kipindi cha "Hard Talk," yaliyotumia lugha ya kiIngereza, ambacho waTanzania wengi hawakijui, Tundu Lissu aliulizwa msimamo atakaochukua kuhusu ushoga endapo atakuwa na mamlaka. Alijibu kuwa hatajishughulisha na kupekua nini kinaendelea vyumbani mwa watu. Alimaanisha ataheshimu haki ya "privacy." Ikumbukwe kuwa haki hiyo imo katika katiba ya Tanzania pia. Kwa upande wa serikali, baada ya kushambuliwa sana kutoka ndani na nje ya nchi kufuatia kauli za Makonda, wizara ya mambo ya nje ilitoa ufafanuzi kwamba kauli za Makonda si msimamo wa serikali ya Tanzania. Wizara ilisema kuwa Tanzania inaheshimu mikataba yote ya kimataifa iliyosaini juu ya haki za binadamu. Tamko hilo lilitosha kuzimisha mashambulizi. Nami nilitamka na bado ninatamka kuwa serikali ilifanya busara kutoa

Duka Jipya la Vitabu Vyangu

Image
Vitabu vyangu viwili, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences  na Matengo Folktales  sasa vinapatikana katika duka la taasisi iitwayo  Planting People Growing Justice . Mwanzilishi na mwendeshaji wa taasisi hiyo, Dr. Artika Tyner, ni profesa wa sheria katika Chuo Kikuu cha St. Thomas  hapa Minnesota. Aliniuliza iwapo nitaridhia vitabu vyangu kuuzwa na taasisi hiyo. Alianza kukifahamu kitabu changu mwaka juzi, baada ya kununua nakala kadhaa kwa ajili ya watu aliowapeleka Ghana katika safari ya kielimu akishirikiana na Monica Habia,  mwanazuoni mwenzake kutoka Ghana. Baada ya safari hiyo, Monica alinielezea jinsi kitabu kilivyowasaidia waMarekani kuyaelewa mambo waliyokutana nayo Ghana. Unaweza kutembelea tovuti ya Planting People Growing Justice . Vitabu hivi viwili vinapatikana Tanzania, katika maduka ya Soma Book Cafe  na  A Novel Idea .