Posts

Showing posts from July, 2020

Kitabu Muhimu kwa Wageni Marekani

Image
Tarehe 11 mwezi huu, nilipata ujumbe kutoka kwa jamaa aishiye eneo la kati la jimbo hili la Minnesota. Anasema kuwa wana jumuia yao ambayo inawakaribisha na kuwasaidia wahamiaji na wakimbizi kimaisha.  Anasema kuwa wanatumia kitabu changu, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences , na wanakiona ni bora sana kwa malengo yao. Kauli kama hizi si ngeni kwangu. Nimezisikia tangu mwaka 2005 nilipochapisha kitabu. Sehemu ya ujumbe ni hii hapa: I  have been involved with a local organization in St. Joe that works to help refugees and immigrants adjust to and succeed in central Minnesota. Our group is called Cultural Bridges.  I have been sharing your book, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences, with members of our group. Everyone who has read it has really enjoyed it and we see it as an excellent resource as we work to fulfill our mission as an organization.

Yatokanayo na Picha ya Msomaji Nami

Image
Picha hii ilipigwa tarehe 27 Julai, 2019, Soma Book Cafe, Dar es Salaam. Wadau wa vitabu, yaani waandishi, wachapishaji, wauzaji, na wasomaji wa vitabu, tulikusanyika kuongelea masuala yanayotuunganisha. Huyu ninayeonekana naye pichani ni Chiombola Joseph ambaye nilimfahamu siku hiyo. Nilikuwa nimetoa mhadhara kuhusu "Writing About Americans," naye akawa mmoja wa wale walionunua vitabu vyangu vilivyokuwa vikiuzwa na Soma Book Cafe. Napenda kusema neno juu ya hilo na mengine yatokanayo. Uamuzi wa kununua kitabu si wa kawaida na si rahisi katika jamii yetu waTanzania. Huyu ndugu alinunua viwili. Sikumbuki wanauzaje, lakini lazima nusu laki au zaidi ilimtoka. Zingatia kuwa vitabu vyangu si udaku na haviko katika orodha ya vitabu vinavyofundshwa mashuleni na vyuoni nchini. Anayeamua kununua vitabu vyangu Tanzania ninamwona kama mtu wa pekee. Najiuliza, ni nini kinachomtuma kufanya hivyo? Bila shaka ni hamu tu ya kutaka kujua mambo. Mimi mwenyewe niko hivyo. Sichoki kununua

Sasa Nimesoma "The Comedy of Errors" (Shakespeare)

Image
Jana nilimaliza kusoma "The Comedy of Errors," tamthilia mojawapo ya Shakespeare, ambaye alliandika tamthilia 37, na labda zaidi kidogo. Katika ulimwengu wa fasihi, Shakespeare ni kinara. Wanafasihi wanaweza kuhoji kwa nini ninatumia neno fasihi kuziongelea tamthilia. Malumbano huenda yasiishe. "The Comedy of Errors" ni tamthilia inayoelezea matatizo na mikanganyiko itokanayo na uwepo wa watu kadhaa katika jamii ambao wanafanana maumbile na sura kiasi kwamba ukikutana na mmoja, halafu baadaye ukakutane na mwingine, hutajua hata kidogo kuwa ni mwingine. Tamthilia hii inaonyesha migogoro, kutoelewana, na magomvi kwa sababu hiyo. Kusoma maandishi ya Shakespeare kunahitaji mwendo wa taratibu. KiIngereza chake ni cha zamani, miaka mia tano iliyopita, na utamaduni ni vile vile. Ni chemsha bongo kwa sisi watu wa leo, sawa na kusoma tungo za zamani za kiSwahili kama vile "Al Inkishafi" au "Utenzi wa Rasi 'lGhuli." Kwa mtazamo wangu, chemsha bongo

Tunasoma Fasihi ya Afrika

Image
Baada ya muhula wa masomo kwisha hapa chuoni St. Olaf, mwezi Mei, sasa ninafundisha kozi maalum ya fasihi ya Afrika. Kwa miaka, nimefundisha kozi hiyo. Ni fursa kwa watu kuufahamu mchango wa waAfrika katika kutafakari masuala ya maisha ya binadamu (kwa maana ya kifalsafa ya "the human experience" na "the human condition") kwa njia ya fasihi. Ninapofundisha fasihi ya Afrika, ninaanza kwa kuielezea Afrika kama chimbuko la binadamu, tekinolojia, lugha, fasihi, falsafa, na yengine yite ambayo binadamu anahusika nayo. Safari hii ninafundisha Changes: A Love Story , Maru , Season of Migration to the North , na Woman of the Ashes. Nimesoma baadhi ya vitabu vya waandishi wote wanne na caribou vyote nilivyovisoma nilivbsoma katika kufundisha. Naweza kusema ninafahamu zaidi kazi za Ama Ata Aidoo na Mia Couto. Hata hivyo, vitabu hivi ninavyofundisha sikuwahi kuvisoma. Kila mara ninapofundisha kozi hii, au nyingine yoyote ya fasihi, nina jadi hiyo ya kufundisha angalau baadhi y