Posts

Showing posts from April, 2021

Kitabu Kimetua Abuja, Nigeria

Image
Mwezi Machi 2021 umeisha vizuri kwangu. Kitabu changu,  Africans and Americans: Embracing Cultural Differences , kimetua Nigeria. Nilikuwa nimempelekea Jennifer Chinyelu Ikeaba-Obiasor, aonekanaye pichani, ambaye anaishi Abuja. Huenda hii ni nakala ya kwanza kuingia Nigeria. Jennifer alisoma kitabu akaandika maoni kwa nyakati mbali mbali: Ni kitabu murua chenyee upeo utakaowasidia waAfrika na waMarekani. Uzoefu wangu unaendana na karibu kila kipengele kitabuni humu. Na kitawafungua macho watu wa tamaduni zote mbili. Ninakipendekeza kitabu hiki kwa kila mmoja, akisome kwa sababu kitamgusa. Jennifer nami tulikutana mtandaoni wiki chache zilizopita tukiwa wafuasi wa  Toyin Umesiri , mhamasishaji maarufu wa biashara baina ya Afrika na Marekani, ambaye aliwahi kufanya mahojiano nami kuhusu  kitabu changu  na kuhusu athari za tamaduni katika biashara baina ya waAfrika na waMarekani. Jennifer ni mjasiriamali, mwanzishi na mkurugenzi mkuu wa  Chiblenders Green . Katika juhudi za kueneza shughu