Posts

Showing posts from June, 2013

Mganga wa Kienyeji Akamatwa Akijaribu Kuloga Ndani ya Mahakama Kisutu

Image
MGANGA WA KIENYEJI AKAMWATA AKIJARIBU KULOGA NDANI YA MAHAMAKA YA HAKIMU MKAZI KISUTU LEO MGANGA WA KIENYEJI HUYU HAPA PICHANI, RAJABU ZUBERI(30),MKAZI WA Kerege,Muheza Tanga, akiwa chini ya ulinzi wa wanausalama leo saa mbili asubuhi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, baada kifaa maalum cha upekezi kumnasa mganga huyo akiwa na vifaa hivyo vya uganga ambavyo alikuwa amekuja navyo mahakamani hapo kwaajili ya kufanyia mambo ya kishirikina katika kesi moja inayomkabili  mmoja wa washtakiwa mahakamani hapo. Hongereni sana wanausalama kwa kazi nzuri ya kumnasa mtu huyo kwani mmesaidia kuvuruga azma yake.Picha kwa hisani ya Happy Katabazi CHANZO: Jamii Forums

Waraka kwa Rais Obama Kutoka kwa Kamati ya Ulinzi wa Wanahabari

Image
Powered by Translate The Committee to Protect Journalists writes to President @BarackObama ahead of his meeting with President @jmkikwete Imewekwa 26.6.13 The Committee to Protect Journalists wrote to U.S. President Barack Obama ahead of his meetings with Tanzanian President Jakaya Kikwete next week to ask that he bring up the critical importance of press freedom to economic development and democracy. June 25, 2013 His Excellency Barack Obama President of the United States of America White House Via facsimile: +1 202-456-2461 Dear President Obama: Ahead of your first trip to East Africa, we would like to bring to your attention the deteriorating state of press freedom in Tanzania. In your meetings with Tanzanian President Jakaya Kikwete, we ask that you discuss the critical importance of press freedom to economic development and democracy. In the past year, CPJ has documented a rise in threats and attacks against j

Mwanafunzi Ameshindwa Kuja Darasani Ili Kumtunza Mbwa

Jana, mwanafunzi wangu mmoja aliniandikia ujumbe kuwa hangehudhuria darasa. Mbwa wa familia, kule Minneapolis, alikuwa hajisikii vizuri, na hapakuwa na mtu wa kumwangalia. Kwa hivyo, kwa niaba ya familia, ilibidi kijana aende kule kumshughulikia mbwa. Hali ya mbwa ilihitaji apelekwe kwa daktari. Kijana alinipa maelezo hayo. Ila leo amekuja darasani. Kabla ya kipindi kuanza nilimwuliza mbwa anaendeleaje, naye akasema alimpeleka kwa daktari ile jana, na anaendelea vizuri. Ninafahamu kuwa habari hii itawashangaza wa-Tanzania wenzangu na wa-Afrika kwa ujumla. Kwetu mbwa hatumjali kiasi hicho. Ni utamaduni tofauti. Lakini hapa ni Marekani. Kama nilivyoeleza katika kitabu changu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences katika utamaduni huu, mbwa wanamjali utadhani binadamu. Baadhi ya maneno niliyoandika ni haya:   Many Americans keep pets, such as dogs, cats, birds, and fish, lavishing much care and tenderness on them. They let their dogs wander anywhere in their hou

Video ya Mkutano wa CHADEMA Ulioshambuliwa Soweto, Arusha

Image

Pinda Awaagiza Polisi Kuwapiga Wakaidi

Sijawahi kusikia kutoka kwa serikali nchini Tanzania kauli kama hii ya waziri mkuu Pinda, kuwa wanaofanya ukaidi wapigwe, kwani eti nchi inaendeshwa kwa misingi ya sheria. Pinda anawaagiza polisi wawapige watu wa aina hiyo. Hapo naona Pinda anajikanyaga, kwani kama Tanzania inaendeshwa kwa misingi ya sheria, sidhani kama sheria inaruhusu kuwapiga hao anaowaita wakaidi. Vile vile maagizo ya Pinda ni ukiukwaji wa haki za binadamu. Kazi ya polisi ni kuwakamata watuhumiwa na kuwafikisha kwenye sheria. Hao ambao Pinda anawaita wakaidi wana haki ya kuhesabiwa hawana hatia hadi mahakama iamue vingine. Kuna tangazo la kimataifa la haki za binadamu ambalo liko wazi kuhusu suala hilo. Kwa muda wote tangu wanapofanya huo ukaidi hadi wanapofikishwa mahakamani, na hadi mahakama itoe uamuzi, hao watu ni watuhumiwa tu.  Huu ndio utawala wa sheria na ni msingi mojawapo wa haki za binadamu. Kusema wapigwe ni kutetea ukiukwaji wa haki za binadamu.

Wanafunzi Wangu Walipata Mkong'oto Babati

Image
Nilikuwa Tanzania mwezi Januari mwaka huu na wanafunzi wa hapa chuoni St. Olaf katika kozi juu ya mwandishi Ernest Hemingway . Tulikaa siku nne Babati. Siku moja wanafunzi waliniambia wameona kiwanja mjini hapo na wanataka kwenda kucheza kabumbu. Walipofika kiwanjani, waliwakuta vijana wenyeji wamevalia sare za kabumbu, wakapatana kuwa wapimane nguvu. Wanafunzi walitwanga vibaya, ila sikumbuki walitwangwa magoli mangapi. Siku ya pili wanafunzi wakaenda tena. Nadhani walikuwa na ndoto ya kulipiza kisasi. Wapi, ndugu yangu. Waligaragazwa tena. Nadhani siku hiyo Babati ilisisimka sana. Kwanza, sio kawaida kutembelewa na wazungu wengi namna hii. Halafu, huenda waliamini kuwa hao wazungu ni wacheza soka, na kwa maana hiyo, matokeo ya mechi yalikuwa kwamba wa-Marekani wamegaragazwa Babati. Yawezekana kuwa hayo ndio maneno yaliyoenea mitaani. Ukweli ni kuwa hao wanafunzi wangu wala sio timu ya kabumbu. Walijikusanya tu kiholela wakaenda uwanjani. Ila, kwa vile ninapangia kuwapeleka

Mnyika Aeleza Sababu za Nassari Kuhamishwa

Image

CHADEMA: Mlipuaji wa Bomu la Arusha ni Polisi

Image
Baadhi ya kauli za Mheshimiwa Mnyika katika video hii zinaendana na kauli aliyotoa mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete, miezi kadhaa iliyopita, kwamba kuna viongozi katika CCM ambao hutumia polisi kuwahujumu wapinzani. Kwa vile mwenyekiti wa CCM alisema hivyo, nawajibika kusema kuwa ni ukweli. Bila upendeleo, nilivyomwelewa mimi ni kuwa alikuwa na nia ya kuwakanya CCM waache ufedhuli huo. Nasubiri kusikia kauli ya msemaji yeyote wa CCM kuhusu hilo suala. Wakisema kuwa CHADEMA inadanganya, basi waseme pia wazi wazi kuwa mwenyekiti wa CCM naye ni mdanganyifu.

CCM na Wadanganyika

Image
Niliiona picha hii katika mtandao wa Facebook, ikaniacha hoi, mbavu sina. Hatimaye, nimeshindwa kujizuia kuiweka hapa katika blogu yangu. Bahati mbaya sijaweza kuona jina la aliyeiandaa picha hii. Ningemtaja, kwa mujibu wa haki mikili.

Makala Yangu Kuhusu Hemingway na Afrika

Image
Jana, niliandika makala fupi kuhusu juhudi zangu za kumwelewa Hemingway na kufundisha maandishi na habari zake. Jana hiyo hiyo, niliona kuwa makala yangu kuhusu kozi niliyofundisha Tanzania mwaka huu juu ya Hemingway inachapishwa na African Global Roots . Nategemea kuwa yeyote anayejiuliza kwa nini nahangaika sana na mwandishi huyu atanielewa, angalau kidogo. Studying Hemingway in East Africa–Upcoming Africana Magazine Article 09 Sunday Jun 2013 Posted by AFRICAN GLOBAL ROOTS in AGR Magazine ≈ Leave a Comment by Joseph L. Mbele For the whole month of January, 2013, I was in Tanzania, with 29 students from St. Olaf College. We were studying the African writings of Ernest Hemingway while visiting some of the places he visited and wrote about. Hemingway is a famous writer, world traveler, big game hunter, and fan of bull fighting and boxing. About ten years ago, I discovered that he also greatly loved Africa. I embarked on exploring th

Nimetoka Mbali na Kozi ya Hemingway

Image
Kila siku, nawazia habari za mwandishi Ernest Hemingway. Kila siku nawawazia pia waandishi wengine, kutoka sehemu mbali mbali za dunia. Hakuna siku inayopita nisisome angalau kurasa kadhaa za maandishi yao, au uchambuzi wa maandishi hayo. Kwa hilo, naweza kusema Hemingway ndiye anayetawala mawazo yangu kila siku. Nilifanya utafiti na tafakari ya miaka kama sita hivi, kabla sijaunda kozi ya "Hemingway in East Africa." Kozi hii imeniwezesha kuzifahamu sehemu nyingi za Tanzania kaskazini, na  kufahamiana na watu wengi katika sehemu hizo. Cha zaidi ni kuwa nimefahamiana na wanafunzi wengi wa ki-Marekani, waliokuja Tanzania kwenye kozi hiyo. Katika picha hapa kushoto, ambayo ilipigwa na Profesa Bill Davis wa chuo cha Colorado , ninaonekana nikitoa mhadhara juu ya Hemingway. Wanafunzi walikuwa kutoka chuo hicho. Huo ulikuwa ni mwaka 2008. Mara ya kwanza kufundisha kozi hiyo ilikuwa ni mwaka 2007, na wanafunzi walitoka chuo hicho hicho. Hapo ni katika viwanja vya chuo cha MS

Sikujua Mwandishi Legson Kayira Alifariki

Image
Leo katika kupitapita mtandaoni, nimeona taarifa kuwa mwandishi Legson Kayira alifariki mwaka jana, tarehe 14 Oktoba. Sikuwa nimepata taarifa hii ya kifo chake. Kilichonifanya nikatafuta habari za Kayira ni kuwa siku chache zilizopita, niliongea na mzee mmoja m-Marekani na katika maongezi na mzee mmoja m-Marekani, mzee huyu alikumbushia kuhusu mwandishi fulani, na kutokana na maelezo yake, nikahisi anamwazia Legson Kayira. Nilipomtajia, pamoja na jina la kitabu chake maarufu cha I Will Try , mzee huyu alikubali kuwa ni yeye aliyekuwa anamwazia. Basi leo, katika kuangalia mtandaoni, nimesoma kuwa kumbe mwandishi huyu alifariki mwaka jana, akiwa na miaka 70. Taarifa hii imenikumbusha miaka ya ujana wetu, tulipokuwa sekondari. Tulikipenda sana kitabu cha I Will Try . Habari ya kijana fukara Legson Kayira kuamua kutembea kwa mguu kutoka kijijini kwake Malawi ili akafike Marekani kusoma, ilikuwa ni habari ya kusisimua, iliyotutia hamasa ya kuwa wakakamavu katika kufuatilia malengo bor

Tunaanza Kusoma "Midnight's Children, Kitabu cha Salman Rushdie

Image
Wiki kadhaa zilizopita, niliezea katika blogu hii azma yangu ya kufundisha kitabu cha Salman Rushdie kiitwacho Midnight's Children . Sasa wakati wa kufanya hivyo umefika. Leo ni siku ya kwanza ya muhula wa kipindi cha joto. Ni siku ya kwanza ya somo langu la Post-colonial Literature. Leo nimejitambulisha kwa wanafunzi na kuitambulisha kozi. Nimeongelea maana ya Post-olonial literature na utata uliopo katika dhana hiyo, malumbano yanayoligubika dhana hiyo. Nimetoa utangulizi kuhusu India, historia ya utamaduni wake na fasihi yake, nikianzia na tungo za kale za Mahabharata na Ramayana , nikalipitisha darasa hadi kwenye uandishi wa watu kama Kalidasa, Tagore, Raja Rao, Mulk Raj Anand, na R.K. Narayan. Niliwaelezea jinsi, kwenye miaka ya sitini hadi leo, wanawake wamejitokeza katika uandishi wa India na wanatoa mchango mkubwa. Hayo yote yalikuwa ni sehemu ya  matayarisho ya kusoma na kujadili Midnight's Children . Nimewaelezea kiasi habari za mwandishi Salman Rushdie, m

Nimehudhuria Ibada ya Ki-Swahili, Minneapolis

Image
 Leo, baada ya kukosekana kwa miezi mingi, nilienda kuhudhuria ibada ya ki-Swahili Minneapolis. Ni ibada ya madhehebu ya ki-Luteri, ambayo hufanyika katika kanisa la Holy Trinity Lutheran Church . Ibada iliendeshwa na mchungaji Dr. Mwalilino. Kwaya iliendeshwa na ndugu Smart Baitani, mwanzilishi na mkurugenzi wa COSAD . Nilipopata fursa ya kuongea na Baitani, ambaye tumefahamiana kwa zaidi ya miaka ishirini, nilimtania kuwa sikutegemea kumwona Minneapolis wakati huu, kwani nilidhani yuko Muleba (Bukoba). Kwenda kwangu leo kulitokana na mwaliko wa rafiki yangu, Mzee Paul Bolstad, anayeonekana wa pili kutoka kulia hapo pichani. Aliniambia kuwa leo angekuwepo mchungaji mgeni, Herb Hafermann, ambaye anaonekana kushoto kabisa. Mchungaji huyu anaifahamu sana Tanzania, na ameishi kule miaka mingi. Mara yake ya kwanza kuja Tanzania ni mwaka 1963, na bado yuko kule. Alitoa mahubiri leo, kwa ki-Swahili. Anaongea ki-Swahili sawa na wa-Swahili, na michapo juu. Wakati huu mchungaji huyu yu

Mama wa Mwanafunzi wa Kozi ya Hemingway Kanitembelea

Image
Leo nimepata bahati ya kuonana na mama wa mwanafunzi mojawapo wa kozi ya Hemingway, ambayo niliifundisha Tanzania mwezi Januari. Mama huyu, mtoto wake, na mimi tunaonekana pichani hapa kushoto. Mama kaja kutoka kwao Connecticut kujumuika na wahitimu wenzake wa chuo cha St. Olaf . Ni utaratibu wanaouita "reunion." Wanakuwepo chuoni kwa siku mbili tatu, wakiongelea masuala mbali mbali, pamoja na kujikumbusha miaka waliyosoma hapa. Laiti tungekuwa na utamaduni huu Tanzania. Mama huyu alikuwa ameleta taarifa kabla, kupitia kwa mtoto wake, kwamba atapenda tuonane. Alisema ana nakala za kitabu changu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences , ambazo alitaka nizisaini. Ndivyo ilivyokuwa leo. Tulikutana, akanielezea jinsi mwanae alivyofaidi na kufurahia kozi ya Hemingway na fursa ya kuwepo Tanzania. Kisha ilisaini nakala zake tatu za hicho kitabu. Kitabu hiki ni kati ya vile ambavyo wanafunzi walitakiwa kusoma kwa maandalizi ya safari ya Tanzania. Nimeshakut