Posts

Showing posts from September, 2014

Tamko la CHADEMA Kuhusu Migomo na Maandamano ya Amani

Image
TAMKO LA CHAMA JUU YA UTEKELEZAJI WA AZIMIO LA MKUTANO MKUU KUHUSU MIGOMO NA MAANDAMANO YA AMANI NCHI NZIMA Ndugu waandishi wa habari Tunapenda kuanza mkutano huu kwa kutoa salaam za amani kwa Watanzania wote, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Amani Kimataifa, ambayo huadhimiswa Septemba 21, ya kila mwaka. Kauli mbiu ya mwaka huu kama ilivyotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ni ‘The Right Of People’s to Peace’. Tumekutana nanyi hapa siku hii mahsusi ya kuazimisha amani kimataifa, tukiwa na ujumbe maalum kwa Watanzania kuwaeleza namna ambavyo watawala wa Serikali ya CCM, wanavyohatarisha amani ya nchi yetu kwa kuvunja haki za msingi za Watanzania huku pia wakififisha matumaini ya wananchi. Tunataja maneno hayo mawili HAKI na MATUMAINI kwa makusudi kabisa kwa sababu hayo ndiyo ndiyo msingi wa amani na utulivu wa kweli mahali katika taifa ambalo linajali na kuzingatia maendeleo na ustawi wa wananchi wake. Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere katika moja

Maandamano ya CHADEMA, Bunge la Katiba, na Polisi

Image
Kwa muda wa siku kadhaa, tumesikia kuhusu azma ya CHADEMA kufanya maandamano katika nchi nzima kupinga vikao vinavyoendelea Dodoma kwenye Bunge la Katiba. CHADEMA inasema kuwa kuendelea kwa vikao hivi ni ufujaji wa fedha za wananchi. Sehemu mbali mbali za nchi, polisi wamekuwa wakifanya juu chini kuzuia maandamano hayo kwa sababu hii au ile. Walioko kwenye hilo Bunge, polisi, na waziri mkuu Mizengo Pinda, wanaendelea kudai kuwa vikao hivi vya Bunge ni halali kwa mujibu wa sheria. Wazo hili limenifanya nami niandike kifupi mtazamo wangu. Kama raia wa Tanzania, ninayo haki sawa na raia wenzangu, kutoa maoni kuhusu suala hilo na masuala mengine yanayohusu nchi yetu. Wale wanaodhani kuwa kwa vile ninafanya kazi Marekani, na nimekaa huku kwa miaka mingi, basi nimechukua uraia wa Marekani, napenda kuwaambia kuwa dhana hii haina ukweli wowote. Sijawahi kuwazia kuchukua uraia wa Marekani wala nchi nyingine yoyote. Kwa hivi, nina haki sawa na m-Tanzania aishiye Dar es Salaam, Korogwe au T

Jibu Langu kwa "Anonymous" Aliyenikosoa Leo

Image
Hapa naleta maoni ya "anonymous," aliyoyatoa leo kwenye taarifa niliyoleta jana kuhusu dhuluma za polisi dhidi ya waandishi wa habari.  Taarifa niliyoweka hii jana ni hii hapa . Baada ya maoni ya "anonymous", nami nimejaribu kuweka jibu langu chini yake, ikashindikana. Kwa hivi, nimeweka hapa maoni yale ya "anonymous" na jibu langu. Mdau karibu ujisomee: ----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------- Anonymous said... Naona na wewe umejiunga katika kundi la wanaharakati ambao wanajiita waandishi. kwa taarifa yako huyo Isango anafanya kibarua (sio ajira rasmi) gazeti la Tanzania Daima na huyo Badi pia anapeleka picha (si muajiriwa rasmi kwa muda mrefu tu, sababu hazijulikani) na wote walikuwa wanakaidi amri halali ya polisi. Nani kasema uhuru wa habari hauna mipaka? Mbona nyie huko Snowden na wikileaks hamuwaachii wafanye watakalo? Babu usijivunjie heshima yako ndogo uliyonayo Se

Dhuluma za Jeshi la Polisi Tanzania Kwa Waandishi wa Habari

Image
  Askari wa Jeshi la Polisi wa kuzuia ghasia wakiwazuia kwa mbwa Waandishi wa habari kufanya kazi yao. Askari wa Jeshi la Polisi wa kuzuia ghasia wakimpa kipigo cha mbwa mwizi Mwandishi wa habari Bwn.  Josephat Isango Muendelezo wa Jeshi la Polisi nchini kuwanyanyasa, kuwatisha waandishi wa habari na kuwafanya wasitekeleze wajibu wao ipasavyo, ilijidhihirisha wazi jana makao makuu ya jeshi hilo, baada ya waandishi kupigwa, kukimbizwa na mbwa ili wasichukue taarifa za kuhojiwa kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe. Tukio la kupigwa na kudhalilishwa kwa waandishi wa habari lilitokea jana, limetokea ikiwa ni siku moja baada ya Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama nchini kushirikiana na waandishi wa habari katika kufanya kazi kwa ajili ya kulinda amani ya nchi. Waandishi waliyopigwa na Polisi hiyo jana ni Josephat Isango anayeandikia gazeti la Tanzania Daima huku Yusuph Badi ambaye ni m

Wa-Kenya Walitia Fora Tamasha la Afrifest

Image
Tarehe 2 Agosti, lilifanyika tamasha la Afrifest , katika mji wa Brooklyn Park, Minnesota. Tamasha hili hufanyika kila mwaka, likijumuisha wa-Afrika na watu wenye asili ya Afrika waishio Marekani, visiwa vya Caribbean, America ya Kati na Kusini, na sehemu zingine, na pia watu wasio wa-Afrika au wa asili ya Afrika. Wote hao hushiriki, kwa lengo la kufahamiana, kuelimishana, na burudani. Tamasha huanzia siku moja kabla, jioni, kwa burudani ya muziki, maonesho ya mavazi na kadhalika. Hivyo ndivyo ilivyokuwa tarehe 1 Agosti. Siku inayofuata, tamasha hufanyika nje uwanjani. Kunakuwepo na mabanda ya wafanya biashara, pia watoa huduma mbali mbali. Kunakuwepo muziki, michezo ya watoto, na mechi ya soka. Ndivyo ilivyokuwa mwaka huu kule Brooklyn Park. Mwaka huu, wa-Kenya walijitokeza kwa wingi kuliko wa-Afrika wa nchi nyingine yoyote. Palikuwa na meza ambapo paliwekwa bidhaa na vitu mbali mbali kutoka Kenya. Bendera ya Kenya ilipepea siku nzima. Ilifurahisha kuona wenzetu walivyoonyesha u

Kitabu Kimeingia Katika Chuo Kikuu cha Cincinnati, Marekani

Image
Pamoja na mengine yote, blogu hii ni mahali ninapohifadhi kumbukumbu za shughuli zangu mbali mbali, hasa zile ninazofanya katika jamii, nje ya chuo ninapofundisha . Kumbukumbu hizi ni pamoja na taarifa kuhusu namna vitabu vyangu vinavyotumika katika jamii. Miezi kadhaa iliyopita, niliona taarifa mpya, ila sikupata fursa ya kuiweka katika blogu hii. Taarifa yenyewe ni kuwa kitabu changu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences kimependekezwa kwa wanafunzi katika chuo cha matibabu cha Chuo Kikuu cha Cincinnati kilichopo katika jimbo la Ohio, hapa Marekani. Profesa wa programu ya kupeleka wanafunzi Ghana, Dr. Jason Blackard, ambaye picha yake nimeiweka hapa kushoto, ndiye aliyekipendekeza kitabu hiki--pamoja na vingine vitatu--akiwataka wanafunzi kuwa kila mmoja achague kitabu kimojawapo, akisome, halafu aandike ripoti fupi kielezea aliyojifunza. Taarifa hizi zimo katika "syllabus" yake ya programu hiyo ya Ghana. Simfahamu profesa huyu, na wala hat

Viongozi wa Afrifest Foundation

Image
Kama wewe ni mtembeleaji wa blogu yangu hii ya hapakwetu au ile ya ki-Ingereza , utakuwa umesoma taarifa zangu kuhusu Afrifest , taasisi iliyoanzishwa hapa Minnesota, Marekani, na makao yake ni hapa hapa. Hapa kushoto tunaonekana baadhi ya viongozi tunaoendesha Afrifest . Kulia kabisa ni Nathan White, kutoka Liberia, ambaye nikatibu mtendaji wa Afrifest , na ndiye ambaye alianzisha wazo zima la Afrifest , kama anavyoelezea hapa . Katikati naonekana mimi, m-Tanzania, ambaye ni mwenyekiti wa bodi ya Afrifest . Nimekuwa mshiriki wa Nathan White tangu mwanzo, pamoja tukapanga na kuendesha tamasha la kwanza la Afrifest , mwaka 2007. Tulipopiga picha hii, afya yangu ilikuwa dhaifu kuliko sasa. Sikumbuki kama maishani mwangu nimewahi kupigwa picha inayonionyesha nikicheka namna hii. Kusohto kabisa ni Wycliff Chakua, kutoka Kenya. Yeye alijiunga na Afrifest miaka michache iliyopita. Ndiye mweka hazina wa Afrifest. Tulipiga picha hii tarehe 2 Agosti, wakati wa tamasha la Afrifest lil

Ninasoma "Shalimar the Clown," Riwaya ya Salman Rushdie.

Image
Salman Rushdie ni mmoja wa waandishi maarufu kabisa wanaoandika katika ki-Ingereza. Kwa uandishi wake, amepata tuzo zinazoheshimika sana, kama vile "Booker Prize." Mimi ni mwalimu wa fasihi ya ki-Ingereza. Mara moja moja ninafundisha kozi ya "South Asian Literature," yaani fasihi ya Asia ya Kusini. Katika kozi hii, ninafundisha maandishi ya watu kama Rabindranath Tagore, R. K. Narayan, Raja Rao, Mulk Raj Anand, Anita Desai, Michael Ondaatje, na Salman Rushdie. Haiwezekani kusoma au kufundisha maandishi yote. Vile vile, kazi mpya za fasihi zinaendelea kuchapishwa. Kwa hivi, kila ninapofundisha kozi ya namna hii, najua kuwa katika orodha yangu kuna waandishi ambao hawamo. Kuna kazi muhimu za fasihi ambazo hazimo. Huu ndio ukweli, ingawa haupendezi. Uchaguzi wowote wa waandishi au maandishi ambao ninafanya kwa kufundishia katika muhula fulani wa masomo una utata na unazua masuali. Nilipofundisha kozi ya "South Asian Literature" kwa mara ya kwanza, Salma

Leo Nimeanza Tena Kufundisha

Image
Baada ya kuumwa kwa miezi mingi, na kuwa katika likizo ya matibabu, leo nimeanza tena kufundisha. Hali yangu inaendelea kuimarika, na ingawa naendelea na matibabu kidogo kidogo, madaktari wameridhia ombi langu kuwa nirudi darasani. Wameniwekea sharti kuwa nisibebe mzigo mkubwa wa kozi za kufundisha, na nisihusishwe na shughuli nyingine ambazo walimu huzifanya, kama vile ushiriki katika kamati mbali mbali na mikutano. Hiyo picha hapa kushoto nimejipiga mwenyewe leo, baada ya kutoka darasani. Hali itakuwa hiyo kwa muhula mzima, ambao umeanza leo, na utamalizika katikati ya mwezi Desemba. Ninafundisha kozi mbili, ya kwanza ni "South Asian Literature," na ya pili ni "Writing." Katika hiyo kozi ya kwanza, ambayo niliitunga miaka michache iliyopita, nafundisha riwaya kutoka India, Pakistan, na Sri Lanka. Riwaya hizo ni, Untouchable , iliyoandikwa na Mulk Raj Anand (India); Twilight in Delhi , iliyoandikwa na Ahmed Ali (India); The Crow Eaters , iliyoandikwa na Bapsi Si

Matamasha Ninayoshiriki ni Kama Shule

Image
Matamasha ninayoshiriki ni muhimu. Ni kama shule. Ninabadilishana mawazo na wadau mbali mbali. Kuna ambayo ninawaeleza na kuwaelimisha, na wao kuna ambayo wananieleza na kunielimisha. Kuna masuali na majibu, au angalau maelezo, kwa upande wao na wangu. Hapa kushoto naonekana niko katika mazungumzo mazito na jamaa mmoja kutoka Liberia, aitwaye Ahmed. Tumefahamiana kwa miaka kadhaa. Hapo tulikuwa katika tamasha la Afrifest , mjini Brooklyn Park. Ninapata fursa ya kukutana na watu wa aina aina. Hapa kushoto niko na mama mmoja ambaye alionekana mkimya, lakini alikuwa na dukuduku ya kujua moja mawili. Ilikuwa katika tamasha la Afrifest , mjini Brooklyn Park. Hapa kushoto nilikuwa katika mji wa Brooklyn Park, na wa-Marekani Weusi wawili. Huyu aliyekaa pembeni yangu tulikuwa tunafahamiana, lakini huyu mwenye kofia ilikuwa ni mara ya kwanza kukutana. Ilikuwa katika tamasha fulani lililoandaliwa na taasisi ya wa-Afrika, inayoshughulikia masuala ya afya. Huyu mwenye kofia aliku

Tamko la Jukwaa la Wakristo Tanzania Kuhusu Katiba Mpya

Tamko la Jukwaa la Wakristo Tanzania kuhusu Katiba Mpya JUKWAA LA WAKRISTO TANZANIA TAMKO LA JUKWAA LA WAKRISTO TANZANIA KUHUSU MCHAKATO WA KATIBA Sisi, wajumbe wa Jukwaa la Wakristo Tanzania, tuliokutana tarehe 27 hadi 28 Agosti, 2014, Dar es salaam , tumepata fursa ya kutafakari, kujadili na kujielimisha kwa kina yaliyomo katika Rasimu ya pili ya Katiba na mjadala unaoendelea katika Bunge Maalum la Katiba. Baada ya mjadala wa kina, tunatoa tamko letu kama ifuatavyo: Tunaipongeza Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo ilikusanya Maoni ya WANANCHI kuhusu mabadiliko hayo na kutuletea Rasimu yenye maoni mengi ya Watanzania bila kujali dini zao, upande wa Muungano walikotoka, hali zao za kimaisha, jinsi na kabila. Pia tunaipongeza Tume kwa kuandaa nyaraka na kumbukumbu mbalimbali kama Randama, Nyaraka zenye maoni ya wananchi, picha, tafiti mbalimbali na hata orodha ya watu walioshiriki kutoa maoni katika Tume. Tume pia iliweza kuandaa Tovuti iliyokuwa na kumbukumbu za Tume