 Matamasha ninayoshiriki ni muhimu. Ni kama shule. Ninabadilishana mawazo na wadau mbali mbali. Kuna ambayo ninawaeleza na kuwaelimisha, na wao kuna ambayo wananieleza na kunielimisha. Kuna masuali na majibu, au angalau maelezo, kwa upande wao na wangu.
Matamasha ninayoshiriki ni muhimu. Ni kama shule. Ninabadilishana mawazo na wadau mbali mbali. Kuna ambayo ninawaeleza na kuwaelimisha, na wao kuna ambayo wananieleza na kunielimisha. Kuna masuali na majibu, au angalau maelezo, kwa upande wao na wangu. Hapa kushoto naonekana niko katika mazungumzo mazito na jamaa mmoja kutoka Liberia, aitwaye Ahmed. Tumefahamiana kwa miaka kadhaa. Hapo tulikuwa katika tamasha la Afrifest, mjini Brooklyn Park.
 Ninapata fursa ya kukutana na watu wa aina aina. Hapa kushoto niko na mama mmoja ambaye alionekana mkimya, lakini alikuwa na dukuduku ya kujua moja mawili. Ilikuwa katika tamasha la Afrifest, mjini Brooklyn Park.
Ninapata fursa ya kukutana na watu wa aina aina. Hapa kushoto niko na mama mmoja ambaye alionekana mkimya, lakini alikuwa na dukuduku ya kujua moja mawili. Ilikuwa katika tamasha la Afrifest, mjini Brooklyn Park.Huyu mwenye kofia alikuwa mtu asiye na papara katika kuzungumza, bali mwenye tafakari nzito. Unaweza kujionea jinsi tunavyomsikiliza kwa makini.
Ninaonekana nikiwahamasisha watoto wa shule kuhusu kufanya bidii shuleni, nikiwapa mfano wangu mwenyewe na hatua niliyofikia maishani. Kuwaambia watoto kama hao kwamba juhudi niliyofanya shuleni imeniwezesha sasa kuwa mwalimu na mwandishi wa vitabu ni namna ya kuwahamasisha wazingatie shule.
 Hapa kushoto niko na jamaa wawili, Diamond Jubilee Hall, Dar es Salaam, katika tamasha la Tripod Media nililotaja hapa juu. Kama unavyoona, tuko katika mazungumzo mazito.
Hapa kushoto niko na jamaa wawili, Diamond Jubilee Hall, Dar es Salaam, katika tamasha la Tripod Media nililotaja hapa juu. Kama unavyoona, tuko katika mazungumzo mazito. Hapa kushoto, katika tamasha la Afrifest, mjini Brooklyn Park, naonekana nikipata mawili matatu kutoka kwa bwana Bolstad, ambaye alizaliwa na kukulia Tanzania, na wazazi wa-Marekani. Ingawa sasa anaishi Marekani, anajisikia kama m-Tanzania, na ki-Swahili anaongea vizuri sana.
Hapa kushoto, katika tamasha la Afrifest, mjini Brooklyn Park, naonekana nikipata mawili matatu kutoka kwa bwana Bolstad, ambaye alizaliwa na kukulia Tanzania, na wazazi wa-Marekani. Ingawa sasa anaishi Marekani, anajisikia kama m-Tanzania, na ki-Swahili anaongea vizuri sana.Yeye nami tumefahamiana kwa miaka mingi kidogo, na naguswa na jinsi anavyokipigia debe kwa watu mbali mbali kitabu changu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences. Watu wa aina yake wanachangia katika kunifanya niwe na ari ya kuandika zaidi, kwa faida ya walimwengu.
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment