Posts

Showing posts from February, 2012

Wadau Walionitembelea "Danish," Arusha

Image
Mwaka 2007, nilikuwa Tanzania na wanafunzi na mwalimu mmoja kutoka Chuo cha Colorado waliokuja kwenye kozi yangu ya Hemingway in East Africa . Ni kozi ya wiki tatu. Tulifika na kuanzia kozi kwenye kituo cha " Danish ," Arusha, wiki ya mwisho ya Mei. Kama ilivyo kawaida ninapokuwa Tanzania, wadau mbali mbali hunitafuta. Basi hapo Danish alikuja Mama Esther Simba, mwenye gauni jekundu pichani, na rafiki yake, ambaye jina lake limenitoka. Tulikuwa tumewasiliana kwa kitambo, kwa barua pepe. Yeye alikuwa mshauri katika programu ya Cross Cultural Solutions , ambayo inaleta watu wa kujitolea Tanzania. Alikuwa anawapokea na kuwahudumia, pamoja na kuwaelimisha kuhusu maisha na utamaduni wa Tanzania. Mama Simba ni mdau wa kitabu changu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences . Shughuli zetu zinahusiana vizuri, kwani nami huwaelimisha wa-Marekani kuhusu utamaduni wa wa-Afrika, na pia nawaelimisha wa-Afrika kuhusu utamaduni wa wa-Marekani chini ya kampuni ya Afri

Kwa Kuzuia Misa, wa-Kwere Mmechemsha

Nimesoma taarifa kuwa waumini wa Kanisa Katoliki la Lugoba, wamemzuia padri asisome misa, eti kwa vile anawasema vibaya. Napenda kusema machache kuhusu suala hilo. Wakwere mmechemsha, tena mno. Mimi ni mtani wenu, kwa hivyo lazima niwape vidonge vyenu! Mimi pia ni m-Katoliki, na ninafahamu fika kuwa waumini hatuna wadhifa wa kuzuia misa isisomwe. Hapo mmekosea kabisa! Mbali ya hilo kosa lenyewe, tambueni kuwa mmewakwaza hata watoto, ambao tunapaswa kuwalea katika njia ya kuheshimu misa na mamlaka ya Kanisa. Tena bora mwende mkaungame. Kama mlikuwa na malalamiko dhidi ya padri, mngeweza kabisa kukaa naye kikao, au kulalamika kwa askofu, na suluhu ingepatikana. Kuzuia misa ni kitendo kiovu sana. Sijawahi kusikia kitu kama hiki. Inaonekana padri alikuwa anawatolea uvivu kwa yale aliyoyaamini kuwa yanakwamisha maendeleo yenu. Sasa nyinyi badala ya kutafakari ili kubaini kama alikuwa anasema ukweli au la, na kama ilikuwa ni ukweli, badala ya kukiri mnarukia hoja ya kwamba anawakera. Kum

Mapinduzi Bora Nyumbani

Image

Picha za Wadau Wakiwa na Vitabu

Image
Hapa naleta picha niizopiga na wadau mbali mbali wa vitabu vyangu. Kila picha inanikumbusha tukio la kukutana na wadau hao. Kila picha inabeba historia fulani, na ningeweza kuisimulia. Kitu kimoja kinachonifikirisha ni jinsi watu wanavyoshika vitabu wakat wa kupigwa picha. Karibu wote wanaweka kitabu sehemu ya kifuani, karibu na moyoni, na wengine karibu na tumboni. Mtu unaweza kuandika insha kuhusu suala hilo, kuelezea saikolojia inayoandamana na upigaji picha kwa upande wa mpiga picha na mpigwa picha, kama watafiti wengine walivyofanya, halafu ukajikita katika kuwaelezea hao wadau wanaopigwa picha wakiwa wameshika vitabu vyao. Hapa ni mjini Faribault, Minnesota, wakati wa tamasha la tamaduni mbali mbali. Hapa ni Sinza, Dar es Salaam. Huyu mdau ni Gilbert Mahenge, mwanakijiji wa Msoga, Bagamoyo. Huyu ni kati ya wa-Tanzania wachache ambao nawaona wameelimika kiukweli, kwa maana kwamba anatafuta elimu bila kuchoka. Mara ya kwanza kukutana naye, tulikuwa kwenye basi tukitoke

Ualimu Kazi Ngumu

Image
Mimi ni mmoja wa walimu ambao tunapenda ualimu. Moyo wangu daima umekuwa kwenye ualimu, na sijawahi kuwazia kubadili mwelekeo. Walimu wanakumbana na vipingamizi kadhaa, kuanzia sera katika sekta ya elimu, hadi tabia za baadhi ya watoto na wazazi. Namsikitikia mwalimu anayeonekana katika hii katuni. Huenda wizara imeamua kuwa watoto wafundishwe dhana kama istilahi, kutohoa au kifyonzeo kabla ya wakati ufaao. Kila somo lazima liende hatua kwa hatua, kufuatana na umri wa mtoto. Utaratibu huu ukifuatwa, itadhihirika kwamba hakuna somo gumu. (Namshukuru mchoraji wa katuni hii, ingawa nimeshindwa kumtambua na kumtaja ipasavyo).

Dini Inayoenea kwa Kasi Kuliko Zote Tanzania

Mara kwa mara ninawasikia watu wakiongelea suala la dini inayoenea kwa kasi kuliko zote Tanzania, Afrika au duniani kwa ujumla. Kila mtu ana mtazamo wake. Wengine wanatoa pia takwimu, ambazo sijui kama ni za kweli au ndoto. Ni mchezo wa kuringiana nani zaidi kwa kutumia takwimu, wakati dini ni suala la mtu binafsi. Wala hutaingia ahera kwa msingi kuwa dini yako hapa duniani ilikuwa na wafuasi wengi kuliko dini nyingine. Kwa mtazamo wangu, dini inayoenea kwa kasi kuliko zote Tanzania ni ufisadi na ushirikina. Ufisadi na ushirikina huo unaendelea kushamiri kiasi kwamba unajitokeza hata kwenye nyumba za ibada za dini mbali mbali. Hebu tutafakari hilo.

Wabunge Wakipanda Basi Kwenda Dodoma, 1984

Image
Picha hii murua nimeiona kwenye blogu ya wavuti . Namshukuru Da Subi. Picha hii ni kumbukumbu ya mambo yalivyokuwa enzi za Mwalimu Nyerere. Viongozi hawakuwa mbali na wananchi. Wote walikuwa wanafahamika kwa jina moja la "ndugu," ambayo ni kielelezo muhimu cha itikadi iliyokuwa inatawala. Hapakuwa na usultani kama ilivyo leo. Tunapiga ngonjera kuwa sultani aliondolewa Visiwani, wakati usultani unaendelea kushamiri nchini.

Nilivyoanza Kupeleka Wanafunzi Tanzania

Image
Nimetoka mbali, katika suala la kuwapeleka Tanzania wanafunzi wa vyuo vya Marekani. Mara baada ya kuja kufundisha katika Chuo Cha St. Olaf , nilianza kujishughulisha na masuala ya programu zinazowapeleka wanafunzi Afrika. Kama mmoja wa washauri wa programu hizo nilijifunza mengi. Baada ya miaka michache, nilianza kuwapeleka wanafunzi Tanzania. Hapa kushoto niko na wanafunzi kwenye chuo kilichokuwa kinaitwa Danish , eneo la Usa River. Hii ilikuwa ni programu ya vyuo vilivyomo katika mtandao wa LCCT . Nadhani hiyo ilikuwa ni mwaka 1997. Hapo Danish , tulikuwa tunawapa wanafunzi mafunzo kuhusu masuala mbali mbali ya Tanzania, kwa wiki moja na kidogo. Baada ya hapo, kwa mujibu wa programu hii, niliwapeleka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam , kusoma kwa muhula mmoja. Hapa kushoto niko na wanafunzi wale wale katika nyumba niiyokuwa naishi pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam , sehemu iitwayo "Research Flats." Kadiri miaka ilivyopita, nimejijengea uzoefu na ufahamu mkubwa wa programu h

Mtoto atoweka nyumbani na anatafutwa

Image
Mtoto huyu pichani afahamikaye kwa jina la Fatuma katoroka nyumbani kwao maeneo ya Mbweni Masauti jana mchana na hajulikani alipo mpaka sasa. Alikuwa amevaa nguo ya kichwani na ameshika begi dogo jeusi. Kwa yeyote atakayemuona tunaomba awasiliane nasi kwa namba 0713 716 656 au ampeleke kituo chochote cha polisi kilicho karibu yake. Chanzo: Michuzi blog

Kabumbu Mto wa Mbu

Image
Miaka michache iliyopita, nilikuwa Mto wa Mbu na wanafunzi katika kozi kuhusu mwandishi Hemingway. Katika kupitapita mitaani, tulitokezea kwenye kiwanja cha mpira. Kabumbu ikuwa inaendelea kama kawaida. Lakini nilivutiwa kumwona mbuzi mweupe akivinjari hadi ndani ya uwanja. Kabumbu iliendelea bila wasi wasi. Najua kuwa ingekuwa mechi kubwa mjini kama Dar es Salaam, halafu mbuzi atinge uwanjani namna hii, watu wangesema mengi.

Mitaani Arusha

Image
Nimefika Arusha mara kadhaa, na nina picha nyingi za mji huo. Kama nilivyofanya kwa miji mingine, kwa mfano Namanga na Mbinga , naleta picha chache. Hapana shaka kuwa baadhi ya wasomaji wa blogu hii hawajafika Arusha. Nataka wapate fununu fulani. Hapa kushoto ni mtaa wa kati kati ya mji, ambapo pana posta na ofisi za usafiri wa ndege, na hoteli na migahawa. Pana maduka ambamo mtu unaweza kununua vitabu na nguo na kazi za sanaa. Hapa kushoto ni mnara wa kumbukumbu ya Azimio la Arusha. Azimio la Arusha lilitangazwa hapa Arusha, mwaka 1967. Mji huu una historia ya kusisimua. Kati ya waasisi wake ni Kenyon Painter , mwekezaji m-Marekani kutoka Ohio. Alijenga posta, kanisa, hospitali, na majengo mengine muhimu, zaidi ya kufungua mashamba ya kahawa na kituo cha utafiti cha Tengeru. Kwa zaidi ya karne moja, watu wengi maarufu kutoka duniani kote wamefika au kupita Arusha, kuanzia viongozi wa nchi hadi watengeneza filamu na waandishi maarufu kama Ernest Hemingway. Umaa

Sera ya Madini Tanzania: Wizi Mtupu

Image
Nimeguswa na katuni hii ya Kijasti, ambayo nimeiona wavuti . Naamini kuwa sera ya madini Tanzania ni wizi mtupu. Hebu fikiria, kwa mfano: serikali ya CCM inatuambia kuwa inaipitia mikataba mibovu ya madini, ili kuziba mianya inayoliletea Taifa hasara, na ili kuhakikisha kuwa Taifa linafaidika na madini hayo. Hapo nina suali: Je, waliosaini mikataba hii mibovu walikuwa wajinga wasioweza kuelewa kilichoandikwa, au walikuwa wamelewa gongo waliposaini, au walikuwa ni mafisadi? Na je, kwa nini hawawajibishwi? Halafu, kwa kuzingatia kuwa serikali ya CCM bado inawaambia hao wanaoitwa wawekezaji waje nchini, je, imeshaandaa mikataba mipya ambayo inatoa kipaumbele kwa nchi? Kukosekana kwa uwazi katika suala hili la madini kunanipa hisia kuwa serikali ya CCM kwa makusudi inaihujumu nchi. Ni fedheha kwa Tanzania kuonekana kuwa ni nchi maskini, na hata hao tunaowaita viongozi wanasema Tanzania ni nchi maskini, wakati ni nchi tajiri kwa rasilimali mbali mbali. Dhahabu yetu, kwa mfano, inayaneem

Wadau Wangu wa Canada

Image
Mara moja moja, katika blogu zangu, nimekuwa nikiandika kuhusu wadau wangu kama mwandishi wa vitabu. Kwa mfano, nimewahi kuandika kuhusu wadau wa Arusha , na Nebraska . Leo napenda kuwakumbuka wadau wangu wa Canada. Hapa kushoto ni picha iliyopigwa Dar es Salaam mwaka 2004, wakati wa maonesho ya vitabu kwenye viwanja vya kumbukumbu za Taifa. Niko na dada yangu na wadau wa Canada, waliokuwa wanaishi Tanzania. Wakati ule nilikuwa nimechapisha vitabu viwili tu: Matengo Folktales na Notes on Achebe's Things Fall Apart . Hao akina mama walipita kwenye meza yangu, wakaviangalia vitabu, halafu wakasema watapita tena baadaye kununua kitabu cha Matengo Folktales . Baada ya kusema hivyo, waliendelea na mizunguko yao katika vibanda vingine. Kwa kawaida, watu wakipita namna hii, huwa si rahisi kukumbuka kurudi tena. Lakini hao, baada ya muda mrefu, walirudi, wakanunua kitabu na tukapiga hiyo picha. Hapa kushoto ni Jeff Msangi, mmiliki na mwendeshaji wa blogu maarufu ya Bongocelebrity . Ali

Watu Tuliosoma Darasa Moja

Image
Kitu kimoja kinacholburudisha moyo wangu ninapokuwa Tanzania ni kukutana na watu tuliosoma pamoja. Mwaka jana, wakati napita Songea, nilionana na Bwana Alto Kapinga, ambaye anaonekana nami katika picha hapa kushoto. Anatoka Lundumato, katika wilaya ya Mbinga. Tulisoma darasa moja, kuanzia la tano hadi la nane, katika Seminari ya Hanga, 1963 hadi 1966. Hiyo ilikuwa ni shule bora kabisa mkoani Ruvuma. Ingawa tulisoma zamani vile, tumebahatika kukutana ghafla mitaani Songea mara kadhaa katika miaka iliyofuata. Baada ya kupita Songea, nilienda hadi kwetu milimani u-Matengo. Wakati wa kutembelea Maguu, nilikutana na Padri Simon Ndunguru, ambaye anaonekana nami katika picha hapa kushoto. Picha tulipiga kijijini Chicago. Padri Ndunguru, mwenyeji wa Mbinga, tulisoma darasa moja, kuanzia la tisa hadi la kumi na mbili, katika Seminari ya Likonde, 1967-70. Hiyo ilikuwa ni moja ya shule bora kabisa Tanzania kwa kufaulisha wanafunzi. Tunapokutana namna hii, tunamshukuru Mungu kwa kutuweka hai had

Tamasha la Vitabu, Houston

Image
Kila mwaka kunafanyika tamasha la vitabu mjini Houston, liitwalo National Black Book Festival . Ni tamasha linalowajumuisha waandishi, wachapishaji na wauzaji wa vitabu, klabu za wasoma vitabu, wahudumu wa maktaba, na wadau wengine wengi. Wanapata fursa ya kukutana na kufahamiana, kuongelea masuala mbali mbali yanayohusu vitabu. Nimeshiriki tamasha la vitabu Minneapolis kwa miaka kadhaa, kama nilivyoandika hapa na hapa . Mimi hushiriki kama mwandishi wa vitabu hivi hapa . Hili tamasha la Houston nimelifahamu kwa miaka kadhaa, kwa kusoma taarifa zake. Kwa miaka yapata miwili iliyopita, nimekuwa nikiwazia kushiriki tamasha hilo. Sio lazima niende mwenyewe Houston au kila mahali kwenye shughuli kama hizi. Ingekuwa nina washirika, kama nilivyodokeza katika blogu hii , wangeweza kuniwakilisha, kama nilivyowakilishwa na wadau wa utalii Mto wa Mbu katika maonesho ya utalii Arusha. Yote hiyo ni mipango ya kuitafakari na changamoto za kuzifanyia kazi. Penye nia pana njia, wala hakuna wasi w

Maskat: Mbunifu wa Mitindo

Image
Katika pita pita zangu mtandaoni, nilikumbana na taarifa kwenye blogu ya Swahili na Waswahili kuhusu mwanamitindo Maskat, m-Tanzania ambaye jina lake jingine ni Hayakuhusu. Nilivutiwa na taarifa hiyo, nikaifuatiliza zaidi, nikaona jinsi dada huyu alivyo mjasiriamali makini. Sio tu anajibidisha katika fani hii ya mitindo, bali anazitumia vilivyo tekinolojia za mawasiliano ya kisasa. Utamkuta sehemu kama Youtube , Facebook na blogu yake . Anwani yake ni maskatdehaan@hotmail.com. Napenda kusoma habari za watu wa aina hii na pia kuzitangaza katika blogu yangu, kwani ni changamoto kwa wengine, hasa watoto na vjiana wetu. Wanasema kuwa picha inajeleza sawa na maneno elfu. Kwa kuangalia picha za Dada Maskat, napata hisia kuwa ni dada anayejipenda na kujiamini, anayejua anachofanya na anakoelekea. Hili ni fundisho muhimu kwa watoto wetu, na sisi wenye mabinti tuna sababu ya ziada ya kuuenzi mfano wa dada Maskat.

Mitaani Mbinga, 2011

Image
Mwaka jana, tarehe 2 Agosti, nilipita Mbinga, mji mkuu wa wilaya yangu, nikapiga picha kadhaa. Hapa kushoto ni kituo cha mabasi. Hapo ndipo unapandia mabasi ya kwenda Mbamba Bay na Songea. Hapo pia unapanda mabasi au magari mengine yanayoenda vijijini katika wilaya hiyo. Hapa kushoto ni mtaa mojawapo wa pembeni, karibu na kituo cha mabasi, upande wa barabara iendayo Songea. Hapo ni mtaa mwingine, sehemu ya bondeni kutoka kituo cha mabasi. Huo nao ni mtaa wa pembeni. Udongo wa Mbinga ni kama inavyoonekana pichani, sawa na ilivyo katika eneo lote kuanzia Songea hadi karibu na Mbamba Bay . Kahawa inastawi katika udongo huo, na hapa Mbinga kuna kiwanda cha kusindikia kahawa . Siku zijazo ninapangia kuleta picha za mashamba ya kahawa, ngano, na kadhalika, ambayo yanazipendezesha sehemu za vijijini katika wilaya ya Mbinga. Huo ni mtaa mwingine upande wa chini kutoka kituo cha mabasi. Mbinga ya leo sio kama ya miaka kumi au ishirini iliyopita. Ingawa nafika h

Iringa: Ofisini kwa Mwenyekiti Mjengwa

Image
Katika mizunguko yangu mwaka jana nchini Tanzania, pamoja na wanafunzi wangu wawili, nilikaa siku kadhaa mjini Iringa. Hapo nilimtafuta Mwenyekiti Mjengwa, mmiliki na mwendeshaji wa Mjengwablog . Tulienda ofisini kwake katika Akiba House. Tulikaribishwa vizuri, tukaelezwa shughuli za ofisi hii. Hatukukaa sana hapa ofisini. Tuliulizia mahali pa kupata chakula cha mchana na Mwenyekiti akatupeleka Neema Craft. Tulipata fursa ya kuongea naye kuhusu mambo kadhaa, yakiwemo ya utaratibu wa vyuo vingi vya Marekani wa kupeleka wanafunzi kwenye masomo nchi za nje na pia kuhusu mawasiliano ya kijamii kama vile blogu. Baada ya hapo tulipanda dala dala tukaenda Kalenga . Natumia dala dala kwa sababu ni njia nzuri ya wanafunzi wangu kufahamiana na wa-Tanzania.

Matangazo ya Biashara

Image
Wengi tumeshaliona tangazo hilo hapa kushoto, kwani limetokea sana mitandaoni. Linachekesha na kuvutia. Linatosha kumfanya mtu atafute mgahawa huu ili akashuhudie mwenyewe huduma za huyu Hassan. Mtangazaji ametumia ubunifu wa kuwateka watu kisaikolojia. Anatafuta biashara, lakini anafanya ucheshi pia. Hiyo ni mbinu ya aina yake. Kuna biashara za namna mbali mbali. Ziko zinazouza bidhaa na nyingine zinauza huduma. Kwa vyovyote vile, ubora wa kinachouzwa ni msingi wa mafanikio kwa mfanyabiashara. Lakini, pamoja na ubora wa kinachouzwa, ni muhimu kwa mfanyabiashara kuielewa saikolojia ya wateja. Mteja ajisikie amekaribishwa vizuri, sio tu auziwe alichokitafuta. Ajisikie amethaminiwa. Kumvumilia na kumjibu vizuri mteja mkorofi ni muhimu. Kumshukuru mteja ni muhimu. Mfanya biashara daima ajiulize mteja wake anajisikiaje wakati wa kuhudumiwa na baada ya kuhudumiwa. Mteja asiyeridhika, au aliyeudhika ni balaa. Atakwenda kuwaambia wengine maudhi yaliyomfika, nao hawataenda mahali hapo, lab

Mfanya Usafi Anajivunia Kitabu Hiki

Image
Jioni hiii, hapa chuoni St. Olaf , nikiwa katika jengo kubwa ambamo kuna mgahawa, posta, na vyumba vya mikutano, amenizukia mzee moja ambaye ni mfanya usafi. Nimefahamiana naye miaka kadhaa. Alivyoniona tu, kwa mbali kidogo, alinipungia mkono akiniita, "Come, come, come!," kama vile kuna dharura. Sikujua kuna nini, bali nikamfuata. Alitangulia kuelekea kwenye sehemu alipokuwa anafanya usafi. Wakati ametangulia, akienda kwa kasi, aliniambia kuwa anataka nisaini kitabu. Alitokomea ndani kisha akaibuka na nakala ya Matengo Folktales . Niliguswa sana, nikasaini, naye akafurahi sana, kama vile amepata tuzo fulani. Mzee huyu, ambaye jina lake ni Maurice, alishaniambia miezi mingi ilyopita kuwa anasoma kitabu changu. Sikushangaa kwa jinsi ninavyowafahamu wa-Marekani. Mtu aliyelelewa katika utamaduni usiothamini vitabu atashangaa inakuwaje mzee achape kibarua cha kusafisha majengo, halafu atumie dola nyingi kununulia kitabu. Kwa jinsi ninavyowafahamu hao wa-Marekani, kwenye sual

Buriani: Mwandishi Faraji Katalambula

Image
Jana tumepata habari kuwa mwandishi Faraji Katalambula, amefariki Dar es Salaam. Nilipokuwa mwanafunzi Mkwawa High School, 1971-72, Faraji Katalambula alikuwa anavuma kuliko waandishi wote wa ki-Swahili waliokuwa hai wakati ule. Picha ya Faraji Katalambula hapa kushoto nimeipata Hiluka Filmz . Nakumbuka jinsi riwaya yake ya Simu ya Kifo ilivyoleta msisimko kwa wafuatiliaji wa riwaya za upelelezi. Laiti ningesoma maandishi yake tangu miaka ile. Leo ningeweza kuelezea hili au lile kwa kujiamini. Lakini miaka ile mimi nilikuwa sijishughulishi sana na ki-Swahili. Nilizama katika maandishi ya ki-Ingereza. Vijana wenzangu waliopenda riwaya za ki-Ingereza walikuwa wanapenda sana riwaya kama za Ian Fleming na James Hadley Chase. Mimi sikuwahi kuzisoma hizo. Nikirudi kwenye uandishi wa ki-Swahili, napenda kusema kuwa nashukuru kuwa miaka iliyofuata, nilijirudi, kama ninavyoelezea katika kitabu cha CHANGAMOTO: Insha za Jamii . Nami sasa nimejiunga na wasomaji wanaowaenzi waandishi wet

Kumbukumbu ya Kuzaliwa Charles Dickens

Image
Leo ni kumbukumbu ya kuzaliwa Charles Dickens yule mwandishi maarufu sana wa riwaya katika lugha ya ki-Ingereza. Alizaliwa February 2, 1812, Landport, maeneo ya Portsea, Uingereza. Sisi tuliosoma shule zamani, tulibahatika kusoma maandishi ya Dickens. Mimi nilianza darasa la kwanza mwaka 1959. Tulianza kujifunza ki-Ingereza darasa la tatu, na miaka michache tu baadaye tulikuwa tunaweza kusoma maandish ya ki-Ingereza na kuongea ki-Ingereza. Dickens ni mmoja wa waandishi waliotupa motisha kubwa ya kusoma maandishi ya ki-Ingereza Tulipokuwa sekondari, tulikuwa tunasoma maandishi ya waandishi mashuhuri kama Shakespeare, Jules Verne, Robert Louis Stevenson, Chinua Achebe, Daniel Defoe na Charles Dickens. Nani atasahau tulivyovutiwa na riwaya ya Dickens ya Oliver Twist ? Ni nani anayeweza kuwasahau wahusika wake wakuu, kama vile Oliver Twist, The Artful Dodger, na m-Yahudi Fagin? Katika riwaya hii, Dickens alielezea, kwa namna isiyosahaulika, matatizo ya watoto wa shule miaka yake, ikiwa

Mwalimu Nyerere Aliiogopa CCM

(Makala hii nilishaichapisha katika blogu yangu. Ninaichapisha tena, wakati huu CCM inapoazimisha miaka 35 ya kuwepo kwake) -------------------------------------------------------------------------------------------------------- Ingawa alikuwa mwanzilishi wa CCM, kwa nia njema ya kuendeleza mapinduzi katika nchi yetu, miaka ilivyozidi kwenda Mwalimu Nyerere alishuhudia jinsi CCM ilivyobadilika na kuwa mzigo kwake na pia tishio kwa usalama wa Taifa. Mwaka 1993 Mwalimu alichapisha kitabu kiitwacho Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania (Harare: Zimbabwe Publishing House, 1993). Pamoja na mambo mengine katika kitabu hiki, Mwalimu alisema kuwa kuna kansa katika uongozi wa CCM. Nanukuu baadhi ya maneno yake: Chama cha Mapinduzi, kwa sababu ya uzito wa historia yake, hadhi ya jina lake, mfumo wa wavu wake, mazoea ya watu, na ubovu wa Vyama vya Upinzani, kinaweza kuchaguliwa na Watanzania, pamoja na kansa ya uongozi wake. Au watu wanaweza wakachoka, wakasema, "potelea mbali:" wakach

Wanafunzi Walioenda Tanzania Wameongea Leo

Image
Mwaka jana, niliandika katika blogu zangu kuhusu mizunguko yangu Tanzania na wanafunzi katika programu ya LCCT . Baadhi ya taarifa ni hii hapa na hii hapa . Baada ya kuwa nao Tanzania kwa wiki tatu, niliwaacha Chuo Kikuu Dar es Salaam , ambapo walisoma kwa muhula moja, kwa mujibu wa programu. Wakisharejea Marekani, wanapata fursa ya kuongelea safari yao, masomo waliyosoma, na maisha yao Tanzania kwa ujumla. Shughuli hiyo imefanyika leo, Chuoni St. Olaf . Kwa vile wanafunzi hao wanasoma kwenye vyuo hapa Marekani, wanakuwa na upeo wa kufananisha mambo ya Chuo Kikuu Dar na vyuo vyao, kuanzia maisha ya wanafunzi, viwango vya ufundishaji, na kadhalika. Wanapokuwa Chuo Kikuu Dar , wanafunzi hao wa LCCT wanapata fursa ya kujitolea kama waalimu wasaidizi katika shule ya msingi ya Mlimani. Mwezi Agosti mwaka jana, nilipoenda hapo shule ya msingi kutoa taarifa kuhusu ujio wa wanafunzi hao, walimu walisema mpango huu wa wanafunzi wa ki-Marekani kujitolea pale una manufaa. Kwa mfano,