Posts

Showing posts from March, 2020

Vitabu Nilivyonunua Leo

Image
Ni muda mrefu umepita, nami sijaandika kuhusu vitabu nilivyonunua kama nilivyokuwa naandika miezi iliyopita. Leo nimeona nifanye hivyo. Nilienda Apple Valley kukutana na mkurugenzi wa African Travel Seminars ambaye tunafanya shughuli za kutangaza utalii Afrika. Baada ya kikao, nilienda katika duka la Half Price Books , ambalo nimelitembelea mara nyingi. Kama kawaida, nilikwenda kwanza kuona vitabu vya Hemingway. Nilichagua  Paris Without End: The True Story of Hemingwahy's First Wife na Ernest Hemingway: Artifacts From a Life . Nilichagua Paris Without End kwa sababu nilitaka kujua zaidi juu ya Hadley Richardson, mke wa kwanza wa Hemingway. Nimesoma habari zake hapa na pale, lakini si kwa undani. Ninafahamu jinsi anavyoelezwa na Hemingway katika riwaya ya A Moveable Feast .  Vile vile niliguswa sana na barua alizoandika Hemingway kwa mke wake huyo pale alipokuwa ameanzisha uhusiano na mwanamke mwingine, Pauline. Hemingway anaelezea namna alivyosongwa na mawazo kuhusu tatizo