Posts

Showing posts from June, 2016

Masuali Kuhusu Uislam Kutoka Katika Blogu ya Kimbilia

Nimeshaandika mara kwa mara kuwa blogu yangu hii ni uwanja huru wa fikra, mawazo, na mitazamo. Ninakaribisha mijadala, na hoja za kuchangamsha bongo, wala sijali kama zinawatatiza watu. Ninasimamia uhuru wa watu kutoa mawazo. Dini ni mada mojawapo ninayopenda kuona inajadiliwa. Wakati wengi wanaamini kuwa tujiepushe na mijadala ya dini, mimi ninasema kuwa mijadala ya dini ni muhimu. Kwa msingi huo, leo ninaleta mada ya dini kwa staili ya pekee. Siku chache zilizopita, niliona makala juu ya u-Islam katika blogu ya Kimbilia. Ni makala inayoibua masuali mengi juu ya u-Islam. Inastahili kusomwa na kujadiliwa. Kati ya masuala yanayotokana na makala hii ni suala la haki na uhuru wa mtu kuwa na dini, kutokuwa na dini, au kubadili dini. Binafsi, ninatetea uhuru na haki hiyo, kama nilivyotamka katika blogu hii.  Tangazo la kimataifa la haki za binadamu linatambua haki hiyo. Ningependa kujua kwa nini watu waliojitoa katika u-Islam, kama vile Wafa Sultan, mzaliwa wa Syria, na Ayaan Hir

Nilivyokutana na Askofu Yakobo Komba (Yafunani)

Image
Kati ya mambo ninayoyakumbuka sana ya ujana wangu ni jinsi nilivyokutana na Askofu Yakobo Komba, ambaye sasa ni marehemu. Alikuwa anajulikana zaidi kwa jina la Yafunani, ambalo ni jina la baba yake. Nilikutana na kuongea naye mwaka 1970, nilipokuwa mwanafunzi wa kidato cha nne katika seminari ya Likonde, mkoani Ruvuma, Tanzania. Baada ya kusoma shule ya msingi Litembo, 1959-62, nilijiunga na seminari ya Hanga, mkoani Ruvuma, 1963-66, na baadaye seminari ya Likonde, 1967-70. Seminari hizi ni za Kanisa Katoliki. Zilikuwa zinachagua wanafunzi waliojipambanua kimasomo na kitabia katika shule zao. Pamoja na masomo ya kawaida ya shule zingine nchini, tulikuwa tunaandaliwa kuwa mapadri. Kwa miaka yetu ile, ili kuwa padri ilikuwa lazima mtu afaulu masomo ya angalau kidatu cha nne, na baada ya hapo alikwenda kusomea falsafa na teolojia katika seminari kuu, kwa miaka kadhaa. Kanisa Katoliki lilihakikisha kuwa mapadri wana elimu ya shuleni kuizidi jamii waliyokuwa wanaihudumia. Miaka ile,

Ninasoma "A Moveable Feast"

Image
Nina tabia ya kusoma vitu vingi bila mpangilio, na niliwahi kutamka hivyo katika blogu hii. Kwa siku, naweza kusoma kurasa kadhaa za kitabu fulani, kurasa kadhaa za kitabu kingine, makala hii au ile, na kadhalika. Sina nidhamu, na sijui kama kuna umuhimu wa kuwa na nidhamu katika usomaji. Siku kadhaa zilizopita, niliandika katika blogu hii kuhusu vitabu nilivyochukua katika safari yangu ya Boston. Nilisema kuwa kitabu kimojawapo kilikuwa A Moveable Feast cha Ernest Hemingway. Ni kweli, nilikuwa ninakisoma, sambamba na vitabu vingine, makala na kadhalika. Matokeo yake ni kuwa inachukua muda kumaliza kitabu. A Moveable Feast ni kitabu kimojawapo maarufu sana cha Hemingway. Wako wahahiki wanaokiona kuwa kitabu bora kuliko vingine vya Hemingway, ingawa wengine wanataja vitabu tofauti, kama vile A Farewell to Arms ,   For Whom the Bell Tolls , na The Old Man and the Sea . Hemingway alikuwa mwandishi bora kiasi kwamba kila msomaji anaona chaguo lake. Ninavyosoma A Moveable Feast

Mhadhiri wa Algeria Akifurahia Kitabu

Image
Jana, katika ukurasa wangu wa Facebook, mhadhiri wa fasihi ya ki-Afrika katika chuo kikuu kimoja cha Algeria ameandika ujumbe kuhusu mchango wangu katika fasihi na elimu, akataja kijitabu changu, Notes on Achebe's Things Fall Apart . Hatufahamiani, isipokuwa katika Facebook. Yeye ni mfuatiliaji wa kazi zangu za kitaaluma, na niliwahi kumpelekea nakala ya Notes on Achebe's Things Fall Apart . Ameandika: Dear professor Joseph you're one of God's gifts to the world of literature and education. I always keep praying for you when I read you book Notes On Achebe's TFA . I love you so much dear. Greetings from Algeria. Kwangu ujumbe huu ni faraja, hasa kwa kuwa unatoka kwa mhadhiri wa somo ambalo ndilo nililoandikia mwongozo. Ninafurahi kuwa mawazo yangu yanawanufaisha watu Algeria. Kijitabu hiki niliwahi kukiongelea katika blogu hii, nikataja kilivyoteuliwa kama mwongozo kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Cornell. Taarifa za aina hii hazinifanyi nitulie na kuji

Nimepitia Tena Duka la Half Price Books

Image
Leo nilimpeleka profesa mwenzangu Mall of America na halafu St. Paul ambako atakaa siku kadhaa. Wakati wa kurudi, niliamua kupita mjini Apple Valley kwa lengo la kuingia katika  duka la vitabu la Half Price Books  ambalo nimekuwa nikilitaja  katika blogu hii.  Ingawa lengo langu lilikuwa kuona vitabu vya aina mbali mbali, hamu yangu zaidi ilikuwa kuona kama kuna vitabu juu ya Ernest Hemingway ambavyo sijaviona kabla. Niliangalia sehemu vinapowekwa, nikaviona vitabu ambavyo ninavifahamu. Lakini, kuna kimoja ambacho sikuwa ninakifahamu,  Paris Without End: The True Story of Hemingway's First Wife .  kilichotungwa na Gioia Diliberto. Ninafahamu kiasi habari za huyu mke, ambaye jina lake ni Hadley, na nilimtaja siku chache zilizopita katika blogu hii. Niliwazia kukinunua, lakini badala yake niliamua kununua kitabu cha By-Line cha Ernest Hemingway, ingawa nilishanunua nakala miaka kadhaa iliyopita, bali niliiacha Dar es Salaam mwaka 2013. By-Line ni mkusanyo wa makala alizochapi

Maktaba ya John F. Kennedy

Image
Wanasema tembea uone. Siku chache zilizopita, nilikwenda Boston kwenye maktaba ya John F. Kennedy kuendelea na utafiti wangu juu ya mwandishi Ernest Hemingway. Maktaba hii ina hifadhi kubwa kuliko zote duniani za maandishi na kumbukumbu zingine zinazohusiana na mwandishi huyu. Hii ilikuwa mara yangu ya kwanza kuitembelea maktaba hii, ingawa taarifa zake nilikuwa ninazifahamu na picha za jengo hili nilikuwa nimeziona mtandaoni. Nilijisikia vizuri nilipolikaribia jengo hili na kuingia ndani, nikafanya utafiti kama nilivyogusia katika blogu hii. Katika kutafakari ziara hii, nimekuwa nikiwazia tofauti iliyopo baina yetu wa-Tanzania na wenzetu wa-Marekani katika kuwaenzi waandishi wetu maarufu. Je, sisi tumefanya nini kuhifadhi, kwa mfano, kumbukumbu za Shaaban Robert? Tuna mkakati gani wa kutafuta na kukusanya miswada yake. Huenda iko, sehemu mbali mbali. Mfano ni barua zake ambazo zilizohifadhiwa na mdogo wake Yusuf Ulenge, kisha zikachapishwa. Lakini je, tumefanya juhudi gani za k

Nimemshukuru Mzee Patrick Hemingway

Image
Leo baada ya kurejea kutoka Boston, nimempigia simu Mzee Patrick Hemingway kumweleza angalau kifupi kwamba ziara yangu kwenye maktaba ya John F. Kennedy imefanikiwa sana. Nimejionea menyewe utajiri wa kumbukumbu zilizomo katika Ernest Hemingway Collection, kuanzia maandishi hadi picha. Nimemwambia kuwa wahusika walinikaribisha vizuri sana na kunisaidia kwa ukarimu mkubwa. Nimemwambia kuwa nimejifunza mengi na nimemshukuru kwa kunitambulisha kwao. Amefurahi kusikia hayo. Ameniuliza iwapo niliwaachia nakala ya kitabu changu, yaani Africans and Americans: Embracing Cultural Differences . Nilijisikia vibaya kuwa sikuwa nimefanya hivyo, nikamwahidi kuwa nitawapelekea. Ni furaha kwangu kuona jinsi mzee huyu anavyokipenda kitabu changu, kama nilivyowahi kuelezea katika blogu hii. Jambo mojawapo nililomweleza ni namna nilivyoshtuka kuona jinsi Hemingway alivyokuwa mwandishi makini, aliyeandika sana, kama hifadhi inavyodhihirisha. Mzee Patrick Hemingway alikumbushia habari ambayo nil

Vitabu Nilivyochukua Safarini

Image
Ninaposafiri kwa basi au ndege, ninapenda kuchukua kitabu au vitabu. Kwa kuwa si mimi ninayeendesha hilo basi au ndege, ninakuwa na muda mwingi wa kujisomea. Siku tatu zilizopita, tarehe 12 Juni, nilisafiri kwenda Boston, nikiwa na kitabu cha A Moveable Feast cha Ernest Hemingway, na Kusadikika cha Shaaban Robert. Nilichukua A Moveable Feast kwa sababu safari yangu ilikuwa ya kwenda kufanya utafiti juu ya Hemingway na pia kwa kuwa kitabu hiki, ambacho nilifahamu habari zake, nilikuwa nimeanza kukisoma miaka michache iliyopita, hata nikanukuu sehemu yake moja katika blogu hii. Niliona kuwa ingekuwa jambo jema kuendelea kukisoma katika safari yangu ya Boston. Nilichukua kitabu cha Kusadikika , kwa kujiweka tayari endapo ningependa kusoma pia kitabu tofauti. Sioni kama ni lazima nimalize kusoma kitabu nikiwa safarini. Inatosha kusoma kiasi fulani. Jana, nikiwa bado mjini Boston, nilitembelea sehemu iitwayo Harvard Square, ambayo niliifahamu zamani kuwa ni sehemu yenye maduka ya

Ziarani Maktaba ya John F. Kennedy

Image
Jana nimefika hapa Boston kwa lengo la kutembelea maktaba ya John F. Kennedy na kuangalia kumbukumbu za mwandishi Ernest Hemingway. Nilijua kwa muda mrefu kuwa maktaba hii inahifadhi idadi kubwa ya kumbukumbu, kama vile miswada, picha, na vitu vingine, kuliko maktaba nyingine yoyote duniani. Leo nimeshinda katika kuangalia hifadhi hii.  Nilianzia na maonesho maalum "Hemingway Between Two Wars," yaliyomo katika maktaba kwa wakati huu, na yatadumu kwa miezi kadhaa. Nimefurahi kuona picha na dondoo muhimu kutoka katika maandishi ya Hemingway baina ya vita kuu ya kwanza na vita kuu ya pili. Uchaguzi wa picha hizi na dondoo umefanywa kwa umakini. Zimewekwa kumbukumbu hizo kutoka kwenye vitabu kama A Moveable Feast ,   The Sun Also Rises ,   Death in the Afternoon ,   A Farewell to Arms ,   Green Hills of Africa , na picha za Hemingway akiwa mwanafunzi, akiwa majeruhi wa vita, akiwa katika mchezo wa "bull fighting" nchini Hispania, akiwa na watoto wake wavulana wa

Kitabu Andika Kwa Ajili Yako

Image
Mara kwa mara ninapata ujumbe kutoka kwa watu wanaohitaji ushauri kuhusu uandishi wa vitabu. Baadhi wanakuwa wameshaandika miswada na wanatafuta ushauri kuhusu kuchapisha vitabu. Wengine, baada ya kupata ushauri wangu ambao kwa kawaida unahusu uchapishaji wa mtandaoni, wanaulizia utaratibu wa malipo. Yaani wanataka kujua watalipwaje kutokana na mauzo ya vitabu vyao. Ninakaribisha maulizo kuhusu masuala haya ya uandishi, uchapishaji, na uuzaji wa vitabu, kama ninavyothibitisha katika blogu hii. Hapa ninapenda kusema neno la jumla kwa watu hao, hasa wanaowazia mauzo na malipo: kitabu andika kwa ajili yako. Nimeona kuwa watu wana kiherehere cha kuchapisha vitabu na kuviuza, wajipatie fedha. Wanaamini kuwa wakishachapisha kitabu, kuna utitiri wa watu watakaonunua, na wao waandishi watajipatia fedha, na labda fedha nyingi. Kwa ujumla, hii ni ndoto. Kwanza, ni waandishi wachache sana duniani wanaopata fedha kutokana na vitabu vyao za kutosha hata kumudu gharama za kawaida za maisha

Nimempigia Simu Mzee Patrick Hemingway

Leo, saa 12.52 jioni, nimempigia simu Mzee Patrick Hemingway, kumwarifu kuwa nimeshawasiliana na wahusika wa maktaba ya J.F. Kennedy kuhusu safari yangu ya kwenda kufanya utafiti. Nimemwambia kuwa nimepata majibu kutoka kwa wahusika sehemu zote mbili za hifadhi ya Hemingway.  Wote wameniletea maelezo ya taratibu za kufuata nitakapofika katika maktaba ile. Nimemwambia kuwa nimefurahishwa na ukaribisho wao, na nimemshukuru kwa kunitia moyo katika azma yangu ya kwenda kwenye maktaba ile. Nimemwambia kuwa nimesoma taarifa ya yaliyomo katika maktaba ile, nikizingatia yanayohusiana na utafiti wangu, ambao ni juu ya Hemingway na Afrika. Nimemkumbusha alivyoniambia kuhusu simba aliyehifadhiwa katika maktaba ya J.F. Kennedy, na kuwa ninangojea kwa hamu kumwona simba huyu ambaye amesimuliwa na Hemingway katika Under Kilimanjaro kama "Mary's lion." Mzee Patrick ameniambia kuwa simba huyu aliye maoneshoni si yule wa Mary, bali aliuawa na Clara Spiegel, na kwamba Sara Spiegel

Tafsiri ya Ubeti wa Kwanza wa "Kibwangai"

Niliandika katika blogu hii kwamba ninatafsiri kwa ki-Ingereza shairi la Haji Gora Haji liitwalo "Kibwangai." Baada ya kukabiliana na matatizo katika kila ubeti, nimeshatafsiri beti zote kumi na moja, na leo nimeona nioneshe nilivyojaribu kutafsiri ubeti wa kwanza. Ubeti huo unasema hivi: Kuna hadithi ya kale, kwa babu nimepokeya Kwa manyani zama zile, mkasa ulotokeya Nilikuwa mwanakele, hayo nikazingatiya Leo nawadokezeya, kwa nilivyoyafahamu Mstari wa kwanza una sehemu mbili, kama ilivyo mistari mingine yote katika ubeti huu. Niliutafsiri mstari wa kwanza namna hii: "There is an age-old story, I got from grandfather." Katika hizo sehemu mbili, sehemu ya kwanza haikunipa tatizo. Tatizo lilikuwa katika sehemu ya pili,  "kwa babu nimepokeya." Mtu ukitaka kuhifadhi mpangilio wa sentensi kama ulivyo, unaweza, na tafsiri inaweza kuwa "from grandfather I received," au "from grandfather I got," au "from my grandfather I receiv