

Nilichukua A Moveable Feast kwa sababu safari yangu ilikuwa ya kwenda kufanya utafiti juu ya Hemingway na pia kwa kuwa kitabu hiki, ambacho nilifahamu habari zake, nilikuwa nimeanza kukisoma miaka michache iliyopita, hata nikanukuu sehemu yake moja katika blogu hii. Niliona kuwa ingekuwa jambo jema kuendelea kukisoma katika safari yangu ya Boston.
Nilichukua kitabu cha Kusadikika, kwa kujiweka tayari endapo ningependa kusoma pia kitabu tofauti. Sioni kama ni lazima nimalize kusoma kitabu nikiwa safarini. Inatosha kusoma kiasi fulani.

Nilivutiwa nilipoona kuwa ni mkusanyo wa makala za wataalam wengi, wakiwemo Theodor Adorno, Gaston Bachelard, Roland Barthes, Georges Bataille, Jean Baudrillard, Walter Benjamin, Ernst Bloch, Helene Cixous, Gilles Deleuze, Jacques Derrida, Umberto Eco, Michel Foucault, Jurgen Habermas, Martin Heidegger, Hans-Georg Gadamer, na Fredrick Jameson,
Majina ya wataalam hao niliowataja tulikuwa tunayasikia na maandishi yao tukiyasoma, nilipokuwa masomoni Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison, miaka ya 1980-86. Nilivutiwa kuona maandishi kama ya Walter Benjamin, "On Some Motifs in Baudelaire;" Gaston Bachelard, "Poetics of Space;" Martin Heidegger, "Building, Dwelling, Thinking;" Roland Barthes, "Semiology and the Urban;" Umberto Eco, "Function and Sign: The Semiotics of Architecture;" Fredrick Jameson, "Is Space Political?" Michel Foucault, "Space, Knowledge and Power (interview conducted with Paul Rabinow).
Kama nilivyogusia, nimevutiwa na juhudi ya mhariri wa Rethinking Architecture: A Reader in Cultural Theory kuzitafuta makala zinazohusu mada moja lakini kwa mitazamo mbali mbali kutoka uwanja mpana wa falsafa. Kwa jinsi ninavyowaheshimu wataalam ambao maandishi yao yamo katika kitabu hiki, nina imani kuwa hiki ni kitabu bora sana.
No comments:
Post a Comment