Posts

Showing posts from December, 2012

Milima Haikutani

Image
Wa-Swahili husema, milima haikutani bali binadamu hukutana. Hayo yalinipata mjini Karatu mwaka 2008 nilipokutana na mzee ambaye anaonekana nami pichani. Siku hiyo ilikuwa siku ya mnada mjini Karatu, siku ambayo hutokea mara moja kwa mwezi. Katika umati mkubwa wa watu, yeye na mimi tulijikuta uso kwa uso. Yeye alinitambua mara moja, akauliza: "Profesa Mbele?" Nilimwambia ndio mimi. Tulifurahi sana, tukaanza michapo. Mzee huyu nilimfahamu mwaka 1996 wakati nafanya utafiti wa masimulizi ya jadi kuhusu shujaa wa wa-Iraqw aitwaye Saygilo Magena. Utafiti huu ulinipeleka kwenye miji na vijijini kama vile Mbulu, Mamaisara, na Karatu. Kati ya watu walionisaidia sana ni huyu mzee ambaye jina lake ni John Qamlali. Baada ya kufahamiana kule Mbulu, tulikutana tena mjini Arusha, tukaongea sana. Anajua sana habari za wa-Iraqw na ameshawasaidia watafiti wengine wa mataifa mbali mbali. Ninazo kanda za maongezi yetu. Kukutana tena mwaka 2008, miaka zaidi ya kumi tangu tulipokutana ma

Maaskofu Watoa Tamko Juu Ya Masuala Mbali Mbali

TANZANIA CHRISTIAN FORUM (TCF) MKUTANO MKUU WA NNE WA JUKWAA LA WAKRISTO TANZANIA (TCF ) TAMKO RASMI “ATUKUZWE MUNGU JUU MBINGUNI, NA DUNIANI IWE AMANI KWA WATU ALIOWARIDHIA” Utangulizi Katika Mkutano Mkuu wa Nne wa Jukwaa la Wakristo Tanzania, Tanzania Christian Forum – TCF, uliofanyika katika Kituo cha Mikutano na Mafunzo cha Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Kurasini jijini Dar es Salaam, tarehe 6 Desemba, 2012; Wajumbe walitafakari kwa undani juu ya kuzorota kwa mahusiano baina ya Dini mbili za Ukristo na Uislamu nchini Tanzania, pamoja na kutathmini juu ya wajibu wa Kanisa na Utume wake wa Kinabii kwa taifa letu. Jukwaa la Wakristo Tanzania (TCF) linajumuisha taasisi kuu za Umoja wa Makanisa nchini kama ifuatavyo;- Jumuiya ya Kikristo Tanzania - CCT Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania - TEC Jumuiya ya Makanisa ya Kipentekoste Tanzania - PCT Kanisa la Waadventisti Wasabato – SDA (observers) Tafakari Tafakari yetu ilianza kwa kujiuliza yafuatayo: 1. Ni mwenend

Shaaban Robert na Nyerere: Waandishi Muhimu kwa Kila m-Tanzania

Image
Kwa miaka michache iliyopita, wakati nimejitosa katika kusoma maandishi ya Shaaban Robert, nimejiwa na mawazo mbali mbali ambayo naona ni muhimu. Kwa bahati nzuri, nimechapisha makala mbili juu ya Shaaban Robert, moja katika Encyclopedia of African Literature , na nyingine katika CHANGAMOTO: Insha za Jamii . Napenda kunukuu machache niliyoandika katika Encyclopedia of African Literature : Shaaban Robert displayed profound awareness of the human condition; he opposed injustice, championed freedom, and extolled the dignity of labour. He was sensitive to the condition of women. He wrote poems celebrating women, and a biography of Siti Binti Saad, the famous female taarab singer, recounting the meteoric rise to fame of this woman from a humble rural background in a male-dominated world which put incredible obstacles in her path. He was proud of his Swahili language and culture, which he understood very well, appropriated, and celebrated in and through his writings. However, he deeply resp

Habari Njema: Kitabu cha "Hemingway and Africa" Kimefika

Image
Leo nina furaha sana. Kisa? Kitabu nilichoagiza, Hemingway and Africa , kimefika leo. Kila ninapojipatia kitabu kipya ninafurahi. Ukizingatia kuwa hadi sasa nina vitabu zaidi ya elfu tatu, utaona kuwa nimekuwa mwenye furaha, tena na tena. Huenda nitaishi miaka kadhaa ya ziada kutokana na hiyo furaha. Pamoja na hayo yote, hiki kitabu cha Hemingway and Africa ni cha pekee. Mwanzo kukiona ni pale nilipokiazima kutoka maktaba ya Chuo Kikuu cha Minnesota, nikakisoma. Kilinigusa kwa namna ya pekee, kwa jinsi kilivyosheheni taarifa na uchambuzi mpya, nikaamua lazima niwe na nakala. Kama unavyoniona pichani, nimekishika kitabu hiki nikiwa nimefurahi sawa na mtu aliyejishindia kreti ya bia. Ninataja bia kwa makusudi. Kitabu hiki, chenye kurasa 398, bei yake ni dola 80 ambayo kwa madafu ni zaidi ya 120,000. Ukienda baa na hela hizo, unapata kreti mbili za bia, kuku mzima, na nauli ya teksi ya kukurudisha kwenu Mbagala. Kama wewe si mtu wa baa, hizo hela ni mchango tosha wa sherehe kama vi

Hongera JWTZ Kwa Kufungua Maktaba

Image
Nimevutiwa sana na taarifa juzi kuwa Rais Kikwete, Amiri Jeshi wa Tanzania, amefungua maktaba ya kisasa kwenye chuo cha mafunzo cha Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Monduli. Ni habari njema kabisa. Mimi ni mdau mkubwa wa maktaba na katika blogu hii ninaziongelea mara kwa mara. Mifano ni maktaba za  Tanga ,  Dar es Salaam ,  Songea ,  Lushoto ,  Moshi ,  Iringa , na  Southdale . Kwa miaka mingi sijawahi kusikia rais au kiongozi mwingine wa kitaifa Tanzania akifungua maktaba, ukiachilia mbali tarehe 9 Desemba, 1967, ambapo Mwalimu Nyerere alifungua Maktaba Kuu ya Taifa, Dar es Salaam. Pita katika maktaba yoyote Tanzania, utaona kuwa maktaba ni kitu ambacho wa-Tanzania hawakithamini sana, isipokuwa labda wanafunzi. Na hao wanafunzi wanaonekana maktabani endapo wamebanwa sana na mwalimu au wanakabiliwa na mitihani. Wakaazi wa Tanga, kwa mfano, wamekuwa na bahati ya kuwa na maktaba tangu mwaka 1958, kabla ya Uhuru. Ingebidi wawe juu kabisa kitaifa kwenye suala la elimu. Lakini wapi

Serikali Yapongeza Kuanzishwa Kitivo cha Udaktari Songea

Image
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Ndugu Said Mwambungu akisalimia wananchi baada ya kuwasili Peramiho. Kushoto kwake ni ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Songea, Norbert Mtega akifuatiwa na Mratibu wa Kitivo cha Udaktari Peramiho Chuo cha Mt Augustino Tawi la Songea Padre Dunstan M. Mbano Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Ndugu Said Mwambungu akikagua maeneo ya kitivo cha udaktari Peramiho. Kushoto kwake ni Joseph Joseph Mkirikiti na kulia kwake ni ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Songea, Norbert Mtega akifuatiwa na Mrati bu wa K itivo cha Udaktari Peramiho Padre Dunstan Mbano Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Ndugu Said Mwambungu akielekezwa jambo na ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Songea, Norbert Mtega . Jengo la utawala ambalo bado halijaanza kutumika Jengo la hosteli ya wanafunzi ambalo bado halijaanza kutumika Jengo la Maa b ara K itivo cha U da ktari Peramiho baada ya ukarabati ambalo bado halijaanza kufanya kazi ku t okana na ukosefu wa vifaa vya kufundishia

Mungu ni Mmoja: Anaitwa Allah, Brahman, Chiuta, Ruwa na Kadhalika

Uzuri wa kuwa na blogu yako ni kuwa hutawaliwi na mtu katika kuamua nini cha kuandika. Uamuzi wote ni wako. Nimesema kabla kuwa katika blogu yangu hii, masuala ambayo yanasemwa kuwa ni nyeti, kama dini, ni ruksa kujadiliwa. Tena sio tu ruksa, bali muhimu kujadiliwa . Leo napenda kutoa hoja kuwa Mungu ni mmoja: anaitwa Allah, Brahman, Chiuta, Ruwa, na kadhalika, kutokana na kuwepo kwa lugha nyingi hapa duniani. Huyu ndiye aliye juu ya yote, mwenye uwezo wote, kama inavyosemwa katika ki-Arabu, "Allahu akbar." Ni dhana ya msingi katika dini zetu. Kama wewe ni mu-Islam, halafu unasema kuwa Allah ni tofauti na Mungu wanayemwabudu wa-Kristu, au Mungu wanayemwabudu wa-Hindu, jichunguze upya, kwani utakuwa unasema kuna miungu zaidi ya mmoja. Utakuwa unaongelea kuwepo kwa mungu mwingine zaidi ya Allah. U-Islam hautambui kuwepo kwa Mungu mwingine zaidi ya Allah. Kama wewe ni m-Kristu, halafu unasema kuwa Mungu unayemwabudu ni tofauti na Allah, basi inabidi ujichunguze, kwa misin

Baridi Kali Minnesota

Image
Jimbo la Minnesota ni moja ya sehemu zinazopata baridi kali kuliko zote Marekani, wakati wa miezi ya baridi. Jana imeanguka theluji nyingi, kama inavyoonekana pichani, katika eneo la Chuo cha St. Olaf . Wakati kama huo ni hatari kuendesha magari, na ajali huwa nyingi, yaani magari kugongana barabarani, au kuteleza na kutumbukia mitaroni. Baridi hii haizoeleki hata kama mtu umepambana nayo miaka na miaka. Inapokuja, ni bora kubaki nyumbani, kama huna sababu ya lazima ya kwenda nje, na kama unakwenda nje, ni lazima kujizatiti kwa mavazi yatakiwayo. Vinginevyo, baridi hii itakuletea madhara. Kuna watu wanaokufa kutokana na kuwa nje kwenye baridi hii. Katikati ya picha hapa kushoto linaonekana gari maalum ambalo kazi yake ni kusafisha njia na barabara kutokana na kufunikwa na theluji.

Simba wa Tsavo

Image
Leo napenda kuongelea habari ya simba wa Tsavo. Ni habari iliyokuwa inatusisimua sana tulipokuwa shuleni, baina ya darasa la tano na la nane. Kulikuwa na kitabu, Simba wa Tsavo , ambacho kilichapishwa mwaka 1966. Ni tafsiri ya kitabu cha J.H. Patterson kilichoitwa The Man Eaters of Tsavo . Kitabu hiki kilielezea matukio ya kutisha wakati ujenzi wa daraja la reli kwenye mto Tsavo, nchini Kenya, miaka mia na kitu iliyopita. Kilielezea namna simba walivyokuwa wakiwavizia, kuwadaka na kuwaua wafanya kazi kwenye eneo la hili daraja wakawaua watu zaidi ya mia, hadi, hatimaye, Patterson alipofanikiwa kuwaua, mwezi Desemba 1898. Hiyo ndio habari tuliyosoma tukiwa shuleni, miaka hiyo ya sitini na kitu. Lakini, kwa miaka hii ya karibuni, yapata miaka kumi, nimekutana na taarifa nyingine nyingi kuhusu simba wa Tsavo. Je, unajua wale simba waliishia wapi? Katika kusoma habari za mwandishi Ernest Hemingway, ambaye alizaliwa mwaka 1899 eneo la jirani na Chicago, nimegundua kuwa alipokuwa mto

Barua za Ernest Hemingway, 1907-1922

Image
Leo nimekipata kitabu cha barua za Hemingway ambacho nilikitaja katika blogu hii siku chache zilizopita. Kama nilivyoandika, nilikiona kwa mara ya kwanza katika duka la vitabu hapa Chuoni St. Olaf. Lakini nakala ile ilinunuliwa hima, ikabidi niagize. Hemingway alikuwa mwandishi makini wa barua. Hata mwanae, Mzee Patrick Hemingway, amethibitisha hivyo. Kwa ujumla, Hemingway hakutaka wala kutarajia kuwa barua zake zichapishwe. Alikuwa na mazoea ya kuandika barua zake kwa uwazi na hata kutumia lugha ambayo inaonekana kali au yenye kukiuka maadili. Baada ya Hemingway kufariki, mwaka 1961, suala la kuchapisha au kutochapisha maandishi ya Hemingway ambayo alikuwa hajayachapisha lilijitokeza na kuwa kubwa. Maandishi yake mengine alikuwa hajamaliza kuyarekebisha. Barua zake alikuwa hajaazimia zichapishwe. Suala likawa nini kifanyike. Wasomaji wa maandishi ya Hemingway walisukumwa na kiu ya kutaka kusoma maandishi yake yote. Wahariri na watafiti walitaka hivyo pia. Familia yake ilikuwa

Wa-Kristu Wasilimu; Wa-Islam Waingia u-Kristu

Image
Dini ni moja ya mada ambazo nazizungumzia sana katika blogu yangu. Leo napenda kugusia tena mada ya mtu kubadili dini. Niliwahi kuandika kuhusu mada hiyo, nikatamka kuwa kubadili dini ni haki ya mtu, kwa mujibu wa dhamiri yake. Soma hapa .  Dini ni safari ambayo binadamu anasafiri. Kwa wengine ni safari ngumu yenye vikwazo vingi. Kwa wengine ni safari nyepesi, kwa maana kwamba wametulia kabisa katika imani yao. Namshukuru Muumba kwamba mimi ni mmoja wa hao waliotulia, ingawa nilipokuwa kijana nilihangaika na kutetereka kiasi fulani. Ukiangalia mtandaoni, kama vile YouTube, utaona taarifa nyingi za watu wanaobadili dini, kutoka u-Islam kuingia u-Kristu, kutoka u-Kristu kuingia u-Islam, na kadhalika. Maelfu ya watu wanafanya hivyo muda wote. Katika YouTube utawaona wengi wakitoa ushuhuda kuhusu walivyohamia dini nyingine na nini kiliwafanya wahame.  Kwa mtazamo wangu, hayo ni mambo yao binafsi, baina yao na Muumba. Hayaongezi wala kuteteresha imani yangu. Hapa chini ni taarifa ya w

Nimekutana na Kobina Aidoo

Image
Siku chache zilizopita, Kobina Aidoo kutoka Ghana alitembelea hapa Chuoni St Olaf kutoa mhadhara kama sehemu ya maazimisho ya Africa Weeks. Maazimisho hayo huandaliwa kila mwaka na jumuia ya wanafunzi iitwayo Karibu. Sikuwa nimesikia jina la Kobina Aidoo, ila nilihudhuria mhadhara wake. Ni kijana mwenye kipaji anayeinukia katika nyanja za filamu na uanaharakati katika kuelimisha jamii. Aliongelea suala la nani ni mw-Amerika Mweusi, akaleta changamoto nyingi zinazowakabili watu weusi wanaoishi hapa Marekani katika kujitambua na kujitambulisha. Baada ya kusema machache, alituonyesha DVD yake ambayo imajaa kauli na mitazamo ya watu weusi wanaoishi Marekani, wakiwa wametokea nchi mbali mbali za Afrika na bara la Marekani. Ni mitazamo inayofikirisha na kuchangamsha akili. Inatupanua mawazo kuhusu utata wa suala hilo la nani ni m-Marekani Mweusi, na kwa ambaye hakufahamu, inashtua kuona migogoro baina ya waMarekani weusi wa asili na watu weusi ambao ni wahamiaji wa miaka ya karibu

Naiwazia Songea

Image
Nyumbani ni nyumbani. Leo nimeikumbuka Songea, nikaamua kuleta picha mbili tatu nilizopiga mwaka huu. Hapa kushoto ni barabara itokayo stendi kuu kuelekea bomani, hatua chache tu kutoka duka la vitabu la Kanisa Katoliki. Nyuma ya haya majengo ndipo kilipo Chuo Kikuu cha Kanisa Katoliki . Hapa ni taswira ya uwanja wa Maji Maji, kutoka juu. Nilipiga picha hii kutoka ghorofa ya tatu ya hoteli niliyofikia, ng'ambo ya barabara kutoka kituo kikuu cha polisi. Kule ng'ambo ni kitongoji cha Lizaboni, njiani kuelekea Peramiho , Mbinga , na Mbamba Bay . Hapa kushoto ni stendi kuu nikiwa na dada yangu na mdogo wangu.

Mwandishi Hemingway: Vitabu Vipya

Image
Ernest Hemingway ni kati ya waandishi maarufu kabisa duniani. Alizaliwa mwaka 1899 karibu na mji wa Chicago, akafa kwa kujipiga risasi nyumbani kwake kwenye jimbo la Idaho mwaka 1961. Katika maisha yake, aliandika sana, akianzia kama ripota wa gazeti la Kansas City Star. Maandishi yake ni pamoja na riwaya, hadithi fupi, insha, masimulizi ya safari zake, barua magazetini, mashairi, na maelfu ya barua. Tangu wakati wa uhai wake hadi leo, watu wengi sana wamechambua maandishi yake na kuelezea maisha yake. Vitabu kumhusu Hemingway vinaendelea kuchapishwa. Miezi ya karibuni, vimechapishwa vitabu kama Hemingway and Africa , Hemingway's Boat , na The Letters of Ernest Hemingway: Volume 1,1907-1922 . Kitabu cha The Letters of Ernest Hemingway: Volume 1, 1907-1922 nilikiona kwa mara ya kwanza miezi michache iliyopita katika duka la vitabu la Chuo cha St. Olaf. Ni kitabu muhimu sana kwa jinsi kinavyojumlisha kila barua ya Hemingway inayojulikana kwa kipindi cha miaka iliyotajwa. Nin