Posts

Showing posts from February, 2017

Mahojiano: Beca Lewis na Joseph Mbele

Miezi michache iliyopita, jirani yangu mmoja, mama Mmarekani, aitwaye Merrilyn, ambaye ni mpiga debe wa maandishi na shughuli zangu za uelimishaji, alimwelezea habari zangu rafiki yake aishiye Ohio. Halafu alimpelekea kitabu changu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences . Wakati huo huo, alituunganisha kupitia mtandao wa Facebook. Beca Lewis, nilikuja kufahamu, ni mwandishi, mwelimishaji, na mmiliki na mwendeshaji wa kituo cha mawasiliano kiitwacho The Shift. Kutokana na alivyomsikia rafiki yake Merrilyn na kutokana na kusoma kitabu changu, Beca Lewis aliniuliza kama ningekubali kufanya mahojiano naye. Nilivyokubali, tulipanga siku, tukafanya mahojiano tarehe 14 Februari, saa tano asubuhi. Leo, Beca Lewis ameyaweka mahojiano yetu hewani, nami nayaleta hapa katika blogu yangu: http://theshift.com/podcast/every-culture-is-weird-and-wonderful/

Mpiga Debe Wangu Kutoka Liberia

Image
Nina jadi ya kuwatambulisha wasomaji na wapiga debe maarufu wa vitabu vyangu katika blogu hii. Ninafanya hivyo ili kuwashukuru, nikizingatia kuwa wanachangia mafanikio yangu kwa jinsi wanavyoupokea mchango wangu. Leo ninapenda kumtambulisha Charles Chanda Dennis, raia wa Liberia ambaye anaishi hapa Marekani, jimbo la Minnesota. Huyu ni mtu maarufu, hasa katika jamii ya wa-Afrika na wa-Marekani Weusi. Ni mtangazaji na mwendeshaji wa kipindi kiitwacho African Roots Connection katika KMOJ Radio. Sikumbuki ni lini nilifahamiana na Charles, lakini nadhani ni miaka karibu kumi iliyopita. Aliwahi kunialika kama mgeni katika kipindi chake tukahojiana juu ya kitabu changu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences . Wiki chache zilizopita, alinialika tena, tukafanya mahojiano marefu na ya kina ambayo unaweza kuyasikiliza hapa: https://www.dropbox.com/home?preview=Story+Telling.mp3 Miaka yapata mitano iliyopita, Charles alialikwa na wanafunzi hapa chuoni St. Olaf kuto

Tafsiri Yangu ya "A Time to Talk" (Robert Frost)

Image
Leo nimetafsiri shairi fupi la Robert Frost, "A Time to Talk." Hili ni shairi nililolisoma kwa mara ya kwanza miaka mitatu iliyopita, baada ya binti yangu Zawadi kuninunulia kitabu cha mashairi ya Frost, Robert Frost: Selected Poems . Kama nilivyoelezea katika blogu hii, nilikuwa nimelazwa hospitalini mjini Minneapolis, na binti yangu, kwa kujua ninavyopenda vitabu, alininunulia hiki kitabu kinisaidie kukabili hali niliyokuwemo. Shairi hili la "A Time to Talk" lina mawaidha mazito kuhusu maisha. Linatukumbusha umuhimu wa uungwana na ukarimu katika mahusiano yetu binadamu. Tuache fikra ya kwamba hatuna muda wa kujumuika na wenzetu, kujuliana hali, na kadhalika. Robert Frost anavyoelezea mambo katika shairi hili ananikumbusha maisha ya vijijini, ambayo niliishi tangu utotoni. Kusalimiana ni wajibu, na watu hutumia muda kujuliana hali. Bila shaka, Frost anaukosoa utamaduni wa ubinafsi, na utamaduni wa kila mtu na maisha yake. Anaikosoa hali ambayo wanafalsafa ka

Ninafurahia Kusoma "Eugene Onegin"

Image
Siku chache zilizopita, niliandika kuwa utungo wa Pushkin, Eugene Onegin ,   ni mtihani.  Madhumuni ya kuandika taarifa ile ilikuwa ni kujiwekea kumbukumbu ya usomaji wangu, sio kufanya uchambuzi au tathmini ya utungo. Nilivyotaja dhana ya mtihani, nilimaanisha kuwa utungo huo unahitaji tafakari ya dhati kuelewa vizuri. Wazo hilo lilijengeka akili mwangu wakati nasoma sura ya kwanza ya Eugene Onegin . Lakini lazima nikiri pia kuwa kuna beti ambazo hazihitaji juhudi kubwa kuzielewa. Kwa kuwa ninasoma tafsiri, siwezi kujua kama ugumu unatokana na utungo wa asili au tafsiri. Kwa pamoja, ingawa ni tafsiri, hizi beti zote zinavutia kwa ukwasi wa sanaa. Mfano ni beti mbili za mwanzo wa sura ya pili ya Eugene Onegin: They bored Onegin past all measure These woodlands, though a charming spot. A friend of innocent, sweet pleasure Might well thank Heaven for this plot. The lonely manor found protection From wind in hills, and in reflection It danced upon the brook below. The distant m

Kitabu Nilichonunua Leo: "The Fundamentals of Tawheed"

Image
Leo nilikuwa mjini Minneapolis. Baada ya shughuli zangu, niliamua kwenda kwenye duka la vitabu vya dini ya Uislam liitwalo Akmal Bookstore. Niliwahi kulitembelea duka hilo, kama nilivyoandika katika blogu hii. Kama nilivyoona mara ya kwanza, duka hili lina vitabu vingi vya Uislam. Leo nilitumia muda kuvipitia. Hatimaye niliamua kununua The Fundamentals of Tawheed: Islamic Monotheism , cha Dr. Abu Ameenah Bilal Philips. Huyu nilifahamu habari zake tangu miaka kadhaa iliyopita. Alizaliwa Jamaica, lakini alikulia Canada, ambako alisilimu mwaka 1972. Nimesikiliza hotuba zake mtandaoni. Ni mmoja wa watu wanaosifika kwa ufahamu wao wa dini ya Uislam. Kama nilivyowahi kuandika tena na tena katika blogu hii, ninasoma vitabu vya Uislam na dini zingine kwa ajili ya kujielimisha, sio kwa ajili ya kubadili dini. Nina dini yangu, na nitabaki hivyo. Ninaiheshimu dini yangu, na ninaziheshimu dini za wengine. Ninategemea wengine nao wafanye hivyo, vinginevyo sisiti kuwakabili kwa hoja. Vile v

Utungo wa Pushkin, "Eugene Onegin," Ni Mtihani

Image
Siku chache zilizopita, niliandika katika blogu hii kuwa nilikuwa ninajiandaa kusoma Eugene Onegin , utungo maarufu wa Alexander Pushkin. Nilianza hima, na sasa ninaendelea. Nilifahamu tangu zamani kuwa Pushkin alikuwa ameandika tungo zingine pia. Nilifahamu kuwa Eugene Onegin ndio utungo wake maarufu kuliko zingine. Nilifahamu kuwa utungo huo ni riwaya iliyoandikwa kwa mtindo wa kishairi. Nilidhani kuwa ningesoma Eugene Onegin bila matatizo, kama ninavyosoma kazi za waandishi wengi. Baada ya kuanza kuusoma, na ninavyoendelea kusoma, ninajikuta kama vile niko katika mtihani. Eugene Onegin si rahisi kama nilivyodhani. Pushkin ameusuka utungo wake kwa umahiri mkubwa, akitumia mbinu mbali mbali za kisanii, na pia taarifa za wasanii wa mataifa mbali mbali, kuanzia zama za kale, hadi zama zake. Humo kuna majina ya watunzi wa mataifa mbali mbali, kama vile Theocritus, Juvenal, Ovid, Racine, Chateaubriand, Lord Byron, pamoja na waandishi na waigizaji kadha wa kadha wa u-Rusi, wa wa

Mahojiano Radio KMOJ: Charles Dennis na Joseph L. Mbele

Image
Tarehe 4 Februari, 2017, nilikuwa mgeni katika programu ya African Roots Connection ya Radio KMOJ, Minnesota. Mwendesha kipindi Charles Dennis alifanya mahojiano nami juu ya masuala mbali mbali yanayohusu historia na utamaduni wa watu wenye asili ya Afrika. Unaweza kuyasikiliza mahojiano hayo hapa: https://www.dropbox.com/home?preview=Story+Telling.mp3 (mpiga picha Zawadi Mbele)

Umuhimu wa Kuzifahamu Tamaduni za Wengine

Image
Mada ya tofauti za tamaduni na athari zake duniani ninaishughulikia sana. Kwa mfano, nimeandika kitabu, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences . Nimeongelea suala hilo pia katika kitabu changu kiitwacho CHANGAMOTO: Insha za Jamii .  Vile vile ninaliongelea mara kwa mara katika blogu hii na blogu ya ki-Ingereza. Umuhimu wa kuzifahamu tofauti za tamaduni unaonekana wazi wazi wakati tunapokumbana na matatizo katika mahusiano yetu na watu wa tamaduni ambazo si zetu. Tusijidanganye kwamba jambo hilo ni la kinadharia tu na kwamba halituhusu. Miaka michache iliyopita, wafanya biashara wa Tanzania walikwenda Oman kushiriki maonesho ya biashara. Walipata shida kutokana na kutojua utamaduni wa watu wa Oman. Taarifa hiyo iliandikwa katika blogu ya Michuzi. Suala hili haliwahusu wafanya bashara tu, bali wengine pia, kama vile wanafunzi wanaokwenda nchi za nje, wanadiplomasia, watu wanaokwenda mikutanoni, na kadhalika. Kwa kuzingatia hayo, na kwa kuwa nimekuwa nikifanya utafit

Interview: Bukola Oriola and Joseph Mbele

Image

Nimemaliza Kusoma The Highly Paid Expert

Image
Leo nimemaliza kusoma The Highly Paid Expert , kitabu kilichotungwa na Debbie Allen, ambacho nilikitaja katika blogu hii. Nimekifurahia kitabu hiki, kwa jinsi kilivyoelezea misingi na mbinu za kumwezesha mtu kuwa mtoa ushauri mwenye mafanikio kwake na kwa wateja. Mambo anayoelezea mwandishi Debbie Allen yananihusu moja kwa moja katika ya kampuni yangu ya Africonexion: Cultural Consultants. Kwa hivi, kitabu hiki kimekuwa na mvuto wa pekee kwangu. Nimevutiwa na namna mwandishi anavyoelezea mbinu za mtu kujijenga katika uwanja wake hadi kufikia kileleni. Anaelezea mategemeo ya wateja na namna ya kushughulika nao. Anaelezea umuhimu wa kujifunza kutoka kwa wataalam wengine, matumizi ya tekinolojia katika kuwasiliana na wateja, kuendesha mikutano, na kujitangaza. Vile vile anasisitiza uaminifu na uwajibikaji. Ameelezea vizuri namna wengi wetu tunavyoshindwa kujitangaza na tunavyoshindwa au kusita kutambua umaarufu na umuhimu wetu na thamani ya ujuzi wetu, jambo ambalo linatufanya tusi

Ninamwazia Mwandishi Alexander Pushkin

Image
Kwa wiki yapata mbili, nimekuwa nikimwazia sana Alexander Pushkin, mwandishi maarufu wa u-Rusi. Nimefahamu tangu ujana wangu kuwa wa-Rusi wanamwenzi kama baba wa fasihi ya u-Rusi. Miaka ya baadaye, nilikuja kufahamu kuwa Pushkin alikuwa na asili ya Afrika, na kwamba hata katika baadhi ya maandishi yake aliongelea suala hilo. Nilisoma makala za profesa moja wa Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison, nikafahamu zaidi suala hilo. Katika kufuatilia zaidi, niliguswa na mengi, hasa maelezo juu ya kipaji cha Pushkin cha ajabu katika matumizi ya lugha ya ki-Rusi na ubunifu wake, na pia jinsi alivyokufa. Aliuawa katika ugomvi akiwa na umri wa miaka 37 tu. Siku kadhaa zilizopita, nilitoa mhadhara katika darasa la Nu Skool, kuhusu umuhimu wa Afrika na wa-Afrika katika historia ya ulimwengu. Kati ya watu maarufu wenye asili ya Afrika ambao niliwataja kwa mchango wao ni Antar bin Shaddad wa Saudi Arabia na Pushkin. Antar bin Shaddad ni mshairi aliyeishi kabla ya Mtume Muhammad, na ambaye tungo z

Miaka 50 ya Azimio la Arusha

Image
Tarehe 5 Februari, mwaka huu, itakuwa ni siku ya maadhimisho ya miaka 50 tangu "Azimio la Arusha" litangazwe, tarehe 5 Februari, 1967. Watu wa rika langu na wale wa umri mkubwa zaidi wanakumbuka jinsi "Azimio la Arusha" lilivyotangazwa na kupokelewa nchini. Wanakumbuka msisimko wa furaha na matumaini ulioigubika nchi kutokana na Azimio hilo. Azma ya kuondoa unyonyaji, kuweka njia kuu za uchumi katika mikono ya wakulima na wafanyakazi, kujenga usawa, kuhakikisha kila mtu mwenye uwezo anafanya kazi na anapata malipo halali ya kazi yake, na kujenga nchi yenye kujitegemea, yote hayo yaliisisimua nchi nzima. "Azimio la Arusha" lilielezea kuwa tumekosea kwa imani yetu kuwa pesa ndio msingi wa maendeleo. Lilitufundisha kuwa msingi wa maendeleo ni watu wenyewe, sio pesa. Na huo ni ukweli hata katika mazingira ya leo. Msingi wa maendeleo ni watu kutumia nguvu yao, akili, maarifa, ubunifu, na uthubutu, bila kutetereka. Maendeleo yanatokana na watu, ni maamuzi