Posts

Showing posts from April, 2015

Maelezo Zaidi Kuhusu Filamu ya "Papa's Shadow"

Image
Wakati huu ninapoandika makala hii niko na binti zangu Deta na Zawadi, tunaangalia filamu ya Papa's Shadow, iliyotngenezwa na Jimmy Gildea, aliyekuwa mwanafunzi katika kozi niliyofundisha Tanzania Januari, 2013. Nimeshaitaja filamu hii katika blogu hii Maelezo yanayoambatana na filamu ni haya: FEATURING AN EXCLUSIVE TESTIMONY GRANTED BY HIS SON, PATRICK HEMINGWAY, PAPA'S SHADOW DIVES HEAD FIRST INTO AUTHOR ERNEST HEMINGWAY'S HUNTING EXPEDITIONS IN EAST AFRICA AND THEIR DEFINING ROLE IN SHAPING A LEGEND. YOUNG FILMMAKER JIMMY GILDEA DOCUMENTS HIS EXPERIENCE WHILE STUDYING HEMINGWAY UNDER THE INSTRUCTION OF AFRICAN AUTHOR JOSEPH MBELE, JOURNEYING ACROSS MIDWEST AMERICA, THROUGH THE SERENGETI PLAIN AND UP THE STEEP CLIFFS OF MT. KILIMANJARO. HEMINGWAY'S SON PATRICK AND MBELE ENGAGE IN AN INSPIRATIONAL AND REVEALING CONVERSATION REGARDING THE FAMOUS AUTHOR'S FASCINATING RELATIONSHIP WITH EAST AFRICA. THIS PERSONAL AND EMOTIONAL FILM EXPOSES MANY ANSWERS TO QU

Leo Nimeonana na Mtengeneza Filamu ya Hemingway

Image
Leo nimeonana na Jimmy Gildea, mtengenezaji wa filamu ya Papa's Shadow . Jimmy alikuwa mmoja wa wanafunzi wa Chuo cha St. Olaf waliokuja Tanzania, Januari 2013, kwenye kozi yangu Hemingway in East Africa. Filamu yake imetokana na kozi ile, na watakaobahatika kuiangalia watajifunza mengi kutoka kwa Mzee Patrick Hemingway, motto pekee aliyebaki wa Ernest Hemingway aliyebaki,  na mimi, ambao ni wazungumzaji wakuu. Tumeongea kwa saa moja na robo hivi, kuhusu filamu yake na masuala yanayohusika nayo. Tumeongelea mikakati ya kuitangaza filamu hiyo, fursa za kuionyesha katika matamasha, vyuoni, na kadhalika. Tumeongelea safari yetu ya Montana tulipoenda kuongea na Mzee Patrick Hemingway, na jinsi alivyotufanyia wema wa kutueleza mengi juu ya baba yake. Tumejikumbusha jinsi alivyotugusa alipoelezea  hisia zake kuhusu hali ya baba yake iliyotokana na unywaji uliokithiri na pia ajali za ndege nchini Uganda zilizohujumu afya yake kwa miaka yote hadi kifo chake. Niliyafahamu mambo ha

Ushauri kwa Waandishi Chipukizi

Image
Mara kwa mara, ninapata ujumbe kutoka kwa waandishi chipukizi wa- Tanzania wakiniomba ushauri kuhusu masuala ya uandishi, uchapishaji, na uuzaji wa vitabu. Ninafurahi kuwapa ushauri wowote ninaoweza, kutokana na uzoefu wangu. Ninataka wafanikiwe. Kwa mfano, ninajisikia vizuri ninapoona mafanikio ya mwandishi chipukizi Bukola Oriola kutoka Nigeria, ambaye anaonekana nami pichani hapa kushoto. Nilisoma katika gazeti hapa Minnesota kuwa alikuwa na mswada, ila hakujua afenyeje ili kuuchapisha. Niliona ni lazima nimsaidie. Ingawa hatukuwa tunafahamiana, nilimwandikia na kumweleza kuwa nilikuwa tayari kumsaidia kuchapisha kitabu chake, bila usumbufu wala gharama. Tulipanga siku, akaja ofisini kwangu, nikamwelekeza namna ya kutumia tekinolojia ya uchapishaji mtandaoni kwenye tovuti ya lulu. Kitabu alichapisha, Imprisoned: The Travails of a Trafficked Victim , ambacho kimechangia kumpa umaarufu hapa Minnesota. Anaalikuwa kutoa mihadhara; anahojiwa katika televisheni, na anaendesha ki

Utitiri wa Blogu

Siku hizi, wa-Tanzania tuna utitiri wa blogu, blogu za kila aina. Pamoja na hayo, blogu zinaendelea kuibuka, kama uyoga. Mimi mwenyewe nimechangia utitiri huo. Nina blogu mbili: hii ya hapakwetu na nyingine ya ki-Ingereza. Mtu akitaka, anaweza kushinda, na hata kukesha, anazisoma hizi blogu, na hataweza kuzimaliza. Wenye blogu na wadau tunaandika usiku na mchana, kwani tumeenea sehemu mbali mbali za dunia. Inapokuwa usiku Tanzania, huku ughaibuni ndio kwanza tunaamka, au ni mchana, alasiri au jioni, bado tuko kazini kwenye blogu. Mtu atasoma hadi achoke, hali sisi tunaendelea kudunda, kama wasemavyo mitaani. Je, kuna ubaya wowote kuwa na utitiri wa blogu? Ni jambo jema, au ni jambo lisilostahili hata kuzungumzwa? Hili ndilo suali kuu ninalotaka kulitafakari, au kulianzishia mjadala. Kwa upande mmoja, utitiri wa blogu ni jambo jema. Kumiliki blogu kunampa mtu fursa kamili ya kujieleza bila vizuizi ambavyo vinakuwepo kwenye magazeti na vyombo vingine vya habari ambavyo vinatawal

Filamu Inayoongelea Kozi Yangu Ya Hemingway

Image
Leo, Jimmy Gildea, mmoja wa wanafunzi waliofika Tanzania mwezi Januari 2013, kwenye kozi yangu ya Hemingway in East Africa ameniletea nakala ya awali ya Papa's Shadow , filamu ambayo ameitengeneza kutokana na kozi ile. Nimeiangalia leo hii na binti yangu Zawadi, na tumeifurahia. Wakati nilipokuwa nawachagua wanafunzi wa kuwepo katika kozi hii, Jimmy aliomba awemo katika msafara wetu ili akarekodi kumbukumbu ("documentary"). Alikuja na vifaa vyake, akawa anarekodi matukio na sehemu mbali mbali tulizotembelea, kama vile Arusha mjini, hifadhi za Ngorongoro na Serengeti, Karatu, na Longido. Baada ya kozi kwisha, wazazi wa Jimmy, kaka yake na dada yake walifika kumchukua Jimmy wakaenda kupanda Mlima Kilimanjaro. Filamu inaonyesha safari hiyo pia, sambamba na maneno maarufu ya Hemingway aliyoyaweka mwanzoni mwa hadithi yake maarufu,  The Snows of Kilimanjaro : Kilimanjaro is a snow-covered mountain 19,710 feet high, and is said to be the highest mountain in Africa. Its

Misahafu na Balaa Linaloitwa Dini

Image
Si kila kinachoitwa dini ni dini. Katika historia, kumekuwepo na uovu mwingi ambao umefanyika kwa jina la dini. Hadi leo, uovu wa aina hiyo unaendelea kufanyika. Siku nyingine, panapo majaliwa, nitaleta na kuongelea mifano, kwa uwazi na haki. Misahafu imetumika na inaendelea kutumika kuhalalisha uovu. Kwa kiasi fulani hii ni kwa sababu mtu anaweza kuzipata nukuu kutoka katika msahafu ambazo zinapingana au zina utata. Lakini vile vile ni suala la tafsiri. Wataalam wa lugha wanatueleza kuwa matumizi ya lugha yanatoa mwanya wa tafsiri mbali mbali.   Kwa msingi huo, watu waovu wanaweza kutafsiri nukuu za msahafu kwa namna ya kuhalalisha uovu. Katika tamthilia ya Shakespeare, The Merchant of Venice , Antonio anasema, "The devil can cite Scripture for his own purpose." Shetani anaweza kunukuu msahafu kwa faida yake mwenyewe. Historia imethibitisha ukweli huo tena na tena.   Tatizo jingine ni imani miongoni mwa waumini wa dini kwamba kila kilichomo katika misahafu sherti kik

Soma Misahafu Upate Akili, Halafu Changanya na Zako

Image
Kati ya vitabu vinavyochangamsha na kutajirisha sana akili ni misahafu ya dini mbali mbali. Hayo ni maoni yangu, yanayotokana na uzoefu wangu. Ninayo misahafu ya dini kadhaa. Ninayo Qur'an , kwa miaka zaidi ya thelathini. Kabla ya kuipata Qur'an , nilikuwa na Biblia . Qur'an niliipata kwenye mwaka 1984 nilipokuwa masomoni Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison. Kati ya marafiki zangu walikuwepo wa-Islam, na mmoja wao kutoka Sudan, alinitafutia Qur'an ilivyotafsiriwa kwa ki-Ingereza na Abdullah Yusuf Ali. Uzuri wa tafsiri hii ni kuwa ina maelezo mazuri ya vipengele mbali mbali. Bhagavad Gita , msahafu maarufu wa u-Hindu, nilijipatia miaka ya hivi karibuni, sambamba na vitabu vingine vya dini hii. Kwa nini mimi, ambaye ni m-Kristu (m-Katoliki) niwe na misahafu ya dini zingine? Kwa nini ninasoma, angalau kidogo kidogo, misahafu ya dini mbali mbali? Nina sababu zangu, na Mungu anajua, na ndiye atakayenihukumu. Kwanza, ninatambua wajibu wa kuwaheshimu wanadamu wote. M

Mazungumzo Kufuatia Mhadhara Lands Lutheran Church

Image
Mhadhara wangu jana kwenye mkutano uliofanika katika kanisa la Lands Lutheran mijini Zumbrota, Minnesota, ulienda vizuri. Kulikuwa na mambo kadhaa katika ajenda, kama vile hotuba na ripoti mbali mbali, muziki na nyimbo. Halafu nilitambulishwa, nikatoa hotuba yangu fupi. Mada yangu ilikuwa "The Dilemma of Cultural Differences: Challenges and Opportunites," ambayo inaendana na utafiti, uandishi, na mihadhara ambayo nimekuwa nikitoa sehemu mbali mbali. Niliongelea umuhimu wa kuzingatia athari za tofauti za tamaduni katika ulimwengu wa utandawazi wa leo. Kwa vile nilikuwa naongea katika mkutano wa waumini wa dini, nilisisitiza kuwa utandawazi huu unatuhitaji tutafakari namna ya kuthibitisha imani ya dini yetu, kwani kuwepo kwa tamaduni mbali mbali ni mtihani anaotushushia Mungu. Kwa kuzingatia kuwa wote waliokuwa wananisikiliza ni wazungu, katika eneo la mashambani, na ambao wanajua propaganda zilizopo Marekani kuhusu wageni wanaoendelea kuingia nchini, niliwakumbusha kuwa Y

Mipango ya Mhadhara wa Keshokutwa Imekamilika

Jioni hii, nimepigiwa simu na Marci Irby wa First English Lutheran Church, Faribault, kunipa taarifa kuwa mipango ya mhadhara wangu wa keshokutwa, imekamilika. Mada yangu itakuwa kama ilivyopangwa, "The Dilemma of Cultural Differences: Challenges and Opportunities." Hadi leo, watu 40 wameshajiandikisha kuhudhuria mkutano. Lakini, kama ilivyokuwa miaka iliyopita, wengine hungoja mpaka dakika ya mwisho, na wengine hujisajili hapo hapo kwenye mkutano. Mama Irby kaniuliza aseme nini juu yangu wakati wa kunitambulisha. Nimemwambia kuwa ninapenda kutambulishwa au kujitambulisha kifupi, bila madoido mengi. Itatosha akitaja jina langu, uraia wangu kama m-Tanzania, na kwamba ninafundisha Chuo cha St. Olaf. Anaweza kuongeza kuwa, zaidi ya kufundisha darasani, ninatoa ushauri kuhusu masuala ya utamaduni kwa wa-Marekani wanaoenda Afrika, iwe ni kusoma, kujitolea, au kutalii, na ninatoa ushauri huo kwa wa-Afrika wanaofika au wanaoishi Marekani.  Mkutano utaanza saa tatu asubuhi,

Mhadhara Ujao, Lands Lutheran Church

Image
Siku zimekwenda kasi. Wiki kadhaa zimepita tangu nilipopata mwaliko wa kwenda kutoa mhadhara katika mkutano wa Sinodi ya Kusini Mashariki ya Minnesota. Mkutano ulipangwa kufanyika mjini Zumbrota, kwenye Kanisa la Lands Lutheran, tarehe 11 Aprili. Mama aliyenialika, kwa niaba ya kamati ya maandalizi, alisema kuwa wangependa niongelee masuala ambayo yameanza kujitokeza katika sharika mbali mbali za sinodi kutokana na kuingia kwa watu kutoka tamaduni mbali mbali. Aliniambia kuwa aliwahi kunisikiliza miaka kadhaa iliyopita katika kanisa lake la First English Lutheran Church , mjini Farbault, nikiongelea masuala hayo, akanunua kitabu changu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences . Wiki zilizofuata, mama huyu nami tuliwasiliana ili kupanga mada ya mhadhara wangu. Nilitoa mapendekezo, naye aliyawasilisha kwenye kamati yao. Pendekezo walilolichagua ni "The Dilemma of Cultural Differences: Challenges and Opportunities." Niliandika taarifa ya mwaliko katika

Bemidji Yamwenzi Mary, Mke wa Hemingway

Image
Jioni ya tarehe 4 Aprili, baada ya kurejea kutoka Leech Lake Tribal College karibu na mji wa Bemidji, niliingia mtandaoni nikiwa na lengo la kuona kama kuna taarifa zozote kuhusu mkutano wetu. Katika ukurasa wa Facebook wa Chuo, niliona taarifa na picha za mkutano ule: Hilo lilinivutia. Lakini niliona pia taarifa nyingine, kuhusu namna mji wa Bemidji unavyomwenzi Mary Welsh, aliyekuwa mke wa nne na wa mwisho wa Ernest Hemingway. Mary Welsh alizaliwa karibu na Bemidji akakulia na kusoma mjini hapo. Kisha alienda kusoma katika Chuo Kikuu cha Northwestern karibu na Chicago. Alikuja kuwa mwandishi katika magazeti hapo Chicago na hatimaye London, akajipambanua kama mwandishi wa habari za vita. Huko ndiko alikokutana na Ernest Hemingway na baadaye wakafunga ndoa. Nilifahamu hayo yote na mengine mengi, kutokana na utafiti wangu wa miaka kadhaa. Nilifahamu tangu zamani kuwa Mary Welsh alizaliwa eneo la Bemidji, na nilikuwa nawazia kwenda kule kufanya utafiti juu yake. Mary Welsh Hemingw

Nimerejea Salama Kutoka Leech Lake Tribal College

Image
Nilirejea jana jioni kutoka Leech Lake Tribal College, kwenye mkutano kuhusu "Narratives of Identity." Nilikuwa mmoja wa wanajopo wanne waliotoa mada, na mada yangu ilikuwa "Being African in America." Niliongelea uzoefu wangu katika miaka mingi ya kuishi na kufundisha hapa Marekani, nikielezea kazi kubwa isiyoisha ya kujitambulisha kama mu-Afrika, ambaye ni tofauti na mu-Amerika Mweusi. Nilielezea jinsi suala hilo linavyosabisha mikanganyiko na kutoelewana baina ya wa-Marekani Weusi na wa-Afrika tuishio Marekani. Nilisema wazi kuwa namna wanavyojiita na kujitambulisha wa-Marekani Weusi ni tofauti na namna tunavyojiita na kujitambulisha sisi wa-Afrika. Nilimnukuu Chimamanda Ngozi Adichie wa Nigeria ambaye katika mahojiano na katika riwaya yake maarufu ya Americanah , ameelezea vizuri suala hilo. Nilimnukuu pia mwandishi Jamaica Kincaid wa Antigua, pande za Caribbean, ambaye pamoja na kuwa ni mweusi pia, hakuwahi kujiita kama wanavyojiita  wa-Marekani Weusi.

Mijadala Kuhusu Vitabu Katika Maktaba ya Bemidji, Minnesota

Ni usiku saa saba kasoro, nami nimo chumbani mwangu katika Hampton Inn hapa mjini Bemidji. Ninasoma gazeti la hapa liitwalo "The Bemidji Pioneer" la jana, yaani tarehe 2. Nimevutiwa sana na habari kuhusu utaratibu walio nao katika mji huu wa kukusanyika katika maktaba yao na kufanya mijadala kuhusu vitabu. Nanukuu habari nzima, ambayo iko ukurasa wa 2: Public Library book discussion set BEMIDJI--The Bemidji Public Library offers a monthly book discussion program--the next session will take place at noon April  13. The program will run for approximately an hour. The book for discussion will be "The Devil in the White City: Murder, Magic and Madness at the Fair that Changed America" by Eric Larson. Nimejikuta nawazia mengi. Je, utaratibu wa aina unawezekana katika miji ya Tanzania? Kuna maktaba katika miji kama Dar es Salaam, Arusha, Tanga, Mwanza, Iringa, Songea, Lushoto, Mbinga, Karatu, na Mbulu. Hizo nimeziona mwenyewe, sio za kusikia. Je utaratibu wa

Nimewasili Bemidji, Minnesota

Image
Alasiri hii, nimewasili mjini Bemidji, nikiwa njiani na wenzangu watatu, ambao tumesafiri pamoja kutoka Minneapolis. Tutalala hapa, na kesho asubuhi tunakwenda Leech Lake Tribal College kwenye mkutano  kuhusu "Narratives of Identity." Mimi ni mmoja wa watoa mada wanne. Mada yangu itakuwa "Being African in America." Tulipokuwa tunakuja, tulisimama kidogo katika mji uitwao Akeley, ili kuona sanamu ya Paul Bunyan, mhusika maarufu katika masimulizi ya jadi ya sehemu hii ya Minnesota, ambaye anajulikana sana pia Marekani na ulimwenguni. Sanamu hii inamwonyesha akiwa ameshika shoka lake. Ili kujionea jinsi sanamu hii ilivyo kubwa, ifananishe na sisi watatu ambao tumesimama hapo Mbele yake. Tulipoingia Bemidji, tulikwenda moja kwa moja kwenye sanamu nyingine ya Paul Bunyan, ambayo inamwonyesha akiwa na fahali wake wa buluu ambaye ni sehemu muhimu ya masimulizi kuhusu mhusika huyu. Sanamu hiyo, sawa na ile ya Akeley, ni kubwa sana. Kwa mujibu ya masimulizi, Paul Bu

Tunahitaji Demokrasia, Lakini Tunahitaji Vyama vya Siasa?

Bila shaka tutakubaliana kuwa tunahitaji demokrasia, yaani mfumo wa utawala ambao ni wa umma, unaendeshwa na umma, kwa maslahi ya umma. Kwa ki-Ingereza wanasema "rule of the people, by the people and for the people." Hii ndio maana na tafsiri ya demokrasia. Lakini je, tunahitaji chama cha siasa? Tunahitaji vyama vya siasa? Ni lini wa-Tanzania walikaa na kulitafakari suali hili? Kwa kweli hawajawahi kufanya tafakari hii. Badala yake wamekurupuka na wazo la chama au vyama, kikasuku tu. Hata wale tunaowaita wasomi wetu nao wameshindwa kuhoji hali hii. Wameshindwa kujinasua kutokana na mtazamo huu, badala ya kufanya kile kinachoitwa kwa ki-Ingereza "thinking outside the box." Nimeelezea zaidi huu ukurupukaji, mkanganyiko, na ukasuku wa wa-Tanzania katika kitabu changu cha CHANGAMOTO: Insha za Jamii.