Posts

Showing posts from May, 2021

Nimealikwa Kuongelea Kitabu Changu

Image
Nimealikwa kuongelea kitabu changu,  Africans and Americans: Embracing Cultural Differences , katika mkutano mkubwa ujulikanao kama  Trade With Africa Summit  utakaofanyika kutumia mtandao tarehe 31 Mei hadi 4 Juni mwaka huu. Mkutano huu hufanyika mara moja kwa mwaaka. Aliniaalika ni mwanaadji waa mkutano  Toyin Umesiri , mjasiriamali na mhamasishaji maarufu wa biashara baina ya Afrika na nchi zingine, hasa Marekani. Aliamua kunialika baada ya kusoma kitabu changu kisha akanialika kwenye kipindi chake cha Nazaru TV  na kufanya  mahojiano nami . Kwa miezi ya karibuni, mimi mwenyewe nimeanza kujibidisha kutafiti namna tofauti za tamaduni zinavyoathiri biashara. Mawazo yangu tayari yanaonekana katika kitabu changu, lakini ninayaendeleza na kuyafafanua. Mfano ya juhudi zangu ni  makala katika Medium  na  maongezi katika YouTube .