Nimepata Zawadi Murua ya Krismasi Leo
Wafuatiliaji wa fasihi ya ki-Ingereza wanafahamu kuwa juzuu la pili la barua za Hemingway, limechapishwa mwaka huu. Sawa na juzuu la kwanza, hili ni buku kubwa, kurasa 519. Leo nimepokea kifurushi kutoka Amazon.com. Binti yangu Zawadi aliponiletea nilishangaa, maana sijaagiza kitabu kutoka Amazon kwa miezi kadhaa. Nilipofungua kifurushi sikuamini macho yangu. Ni juzuu hilo nililolitaja. Nimefurahi sana. Nilikuwa natamani kufanya mkakati wa kununua. Lakini Mungu mkubwa, kamwongoza huyu bwana aninunulie hiki hiki ambacho roho yangu ilikuwa inatamani. Bwana aliyeniletea ni David Cooper, mzazi wa mwanafunzi mmojawapo wa wale waliokuja Tanzania mwezi Januari mwaka huu kwenye kozi ya Hemingway. Baba huyu ni msomaji makini wa Hemingway na waandishi wengine. Ni huyu bwana, anayeishi Ohio, alipoambiwa na kijana wake kwamba natamani siku moja kwenda Montana kuongea na Mzee Patrick Hemingway, mtoto pekee wa Ernest Hemingway aliebaki, alisema atatusafirisha kwa ndege yake. Siku ilipofika