Posts

Showing posts from October, 2010

Polisi Wajifunze Nidhamu, Wazingatie Haki

Mara kadhaa, hasa wakati wa kampeni za kisiasa na uchaguzi, tumeshuhudia vitendo vya polisi na vyombo vingine vya dola ambavyo vimechangia kuleta hofu miongoni mwa wananchi na pia kuvuruga amani. Katika uchaguzi wa mwaka huu, vitendo hivi vimejitokeza tena, kama inavyoonekana katika video hii Kwanza namsifu na kumshukuru huyu dada anayeongea katika video hii kwa kutuelezea hayo anayoelezea, kwa uwazi na kwa dhati. Nafikiri ametoa somo la maana sana, na nategemea wahusika watajirekebisha. Kama wahenga walivyosema, kosa si kufanya kosa, bali kurudia kosa. Kwa upande mwingine, ni lazima niseme kuwa, kwa ujumla, kazi ya polisi si rahisi. Katika mazingira kama haya ya kampeni za siasa na uchaguzi, hali inaweza kuwa ngumu pia, kwa sababu ya ushindani mkubwa na pengine uhasama unaoweza kuwepo katika jamii. Kwa hivi, naamini kuwa polisi wanaweza kufanya maamuzi au vitendo kwa lengo la kulinda amani, kumbe ikawa vitendo vyao vikachangia kuharibika kwa amani. Hata hivi, naamini kuwa polisi

Mahojiano: JK na Wanahabari

Jana tangu asubuhi hadi leo mchana nilikuwa Chicago, katika mkutano. JK alifanya mahojiano yake na wanahabari jana hiyo hiyo. Leo nimeona yamewekwa katika blogu maarufu ya wavuti . Nami nimeyaweka hapa kwangu, nikitanguliza shukrani kwa Da Subi.

Mgombea wa CCM Kufanya Mahojiano

Zikiwa zimebaki siku tatu tu hadi uchaguzi ufanyike nchini Tanzania, tumepata habari kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM atafanya mahojiano na vyombo vya habari. Hii ni tofauti na msimamo wa CCM katika kipindi chote cha kampeni, ambapo wagombea wake walikuwa hawashiriki midahalo. Wengi wetu tunafahamu kuwa midahalo, mahojiano, na kadhalika, ni mambo muhimu katika jamii inayothamini elimu. Sasa kwa nini CCM haikutambua hilo kabla? Tena CCM ni chama chenye wanachama milioni kadhaa, wakiwemo "wasomi" wengi. Ni lazima niulize: hao ni wasomi kweli au ni wababaishaji? Ni aibu kuwa hawakuweza kuchangamka kabla na kutambua umuhimu wa midahalo, hadi saa hii ya mwisho, na baada ya Dr. Slaa kuonyesha mfano. Mimi kama mwalimu, na pia raia ambaye si mwanachama wa chama chochote cha siasa, nawajibika kuwashutumu CCM kwa kutoonyesha mfano bora, pale walipotamba kuwa mgombea wao hahitaji kushiriki midahalo. Na pamoja na hayo, wagombea wao wote wakawa hawashiriki midahalo. Sijui kama ilik

Mbumbumbu Waache Kugombea Uongozi

Kitu kimoja kinachonikera ni jinsi wakati wa kugombea uongozi, mbumbumbu wengi wanavyojitokeza kuwania uongozi. Halafu, kwa jinsi wapiga kura wengine walivyo mbumbumbu, wanawapigia kura hao mbumbumbu wenzao na kuwawezesha kushinda. Baada ya hapo, kunakuwa na matatizo mengi. Tatizo moja kubwa ni jinsi hao mbumbumbu wanaoitwa viongozi wanavyojifanya miungu. Hawakubali kukosolewa. Kwa mfano, gazeti likiwakosoa, wanalitishia au wanazuia lisichapishwe. Kama kuna kitabu kimewakosoa, wanakipiga marufuku. Msimamo wangu ni kuwa watu wasiojiamini au wasioheshimu uhuru wa watu kutoa fikra, wasigombee uongozi. Nchi inahitaji viongozi wa kweli, ambao wanatambua kuwa wao si miungu, na ambao hawatetereki kwa kukosolewa. Kibaya zaidi ni kuwa hao mbumbumbu wanadhani kuwa wao ndio nchi. Wakikosolewa, wanasema ni hatari kwa usalama wa taifa. Ni usalama wa taifa au ni usalama wa mbumbumbu? Ni taifa gani ambalo linatetereka kwa sababu ya mbumbumbu kukosolewa? Haya ninayosema nayasema kwa dhati. Mimi

Video za Mdahalo wa Dr Slaa, ITV

Zimepatikana video za mdahalo wa Dr. Slaa katika ITV. Ni wazi kuwa Dr. Slaa ni mtu anayejua anachoongea, anayeijua nchi, anayewaheshimu wananchi, na anaipenda sana nchi yetu. Anafahamu vizuri nini anachotaka kifanyike ili kuinusuru na kuiendeleza nchi yetu. Ni muhimu kuwa na mtu wa aina hii, hata kama mnapishana mawazo. Nyerere alikuwa mtu wa aina hii hata kama baadhi walipishana naye mawazo. Mimi kama msomi nimevutiwa sana na jinsi Dr. Slaa anavyoongea kwa kujiamini. Kwa hilo nalo amenikumbusha ya Mwalimu Nyerere, ambaye wakati mwingine alikuwa anatumbukia pale Chuo Kikuu Dar es Salaam ili kujibizana na wasomi masuali ya papo kwa papo. Nami nilikuwepo, kwanza kama mwanafunzi, na kisha kama mhadhiri. Mtu wa namna hii ananivutia sana.

Mdahalo, ITV, Dr. Slaa

Mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA, Dr. Slaa, amefanya mdahalo ITV, kama ilivyotangazwa kwa siku kadhaa. Mimi kama mwalimu naiheshimu sana midahalo, kwani ni njia madhubuti ya kuelimishana, na katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi, ni njia madhubuti ya kuwaelewa wagombea. Namsifu Dr. Slaa kwa kujitokeza mbele ya umma namna hii, na nawashutumu wale wote ambao wamekataa kushiriki midahalo. Sikiliza mdahalo huu wa ITV na Dr. Slaa hapa: This browser does not show iframe content. Check this out on Chirbit Mdahalo huu unaweza kuufuatilia pia na kupata taarifa nyingi zaidi hapa .

Mazungumzo Mjini Faribault Kuhusu Tamaduni, Oktoba 21

Image
Jana jioni, kama nilikuwa mjini Faribault, kuongelea kitabu changu cha Africans and Americans , kama nilivyoandika juzi katika blogu hii . Matangazo yalikuwa yamewekwa sehemu mbali mbali, kama vile gazeti la Faribault Daily New na ukumbi wa Facebook. Wahudhuriaji walikuja kutoka Faribault na miji ya karibu. Wengine, ambao tumefahamiana Facebook, walikuja kutoka Minneapolis. Nilianza kwa kuelezea kifupi, nilivyokuja Marekani mara ya kwanza, kusomea shahada ya uzamifu katika chuo kikuu cha Wisconsin-Madison , 1980-86, ndipo nikapata uzoefu wa kuishi katika utamaduni tofauti na wangu, na nikaanza kupata ufahamu wa yale niliyokuja baadaye kuyaandika katika kitabu cha Africans and Americans na kadhalika. Niliongelea jinsi tunavyojengeka katika utamaduni wetu na kuona utamaduni wetu ndio sahihi na wenye mantiki bora. Kumbe, tukienda kwenye utamaduni wa wengine, tunaona mambo tofauti, na hii inaweza kuwa chanzo cha matatizo katika mahusiano yetu na watu wa utamaduni ule. Nilitaja mifano

Nataongelea Kitabu Changu Faribault, Minnesota, Oktoba 21

Image
Tarehe 21 Oktoba nitakwenda Faribault, Minnesota, kuongelea kitabu changu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences . Nimealikwa na uongozi wa Maktaba ya Faribault kwa kushirikiana na mji wa Faribault. Nimeshatembelea Faribault mara kadhaa, kutoa mihadhara na kushiriki shughuli zinazohusu elimu kwa jamii na hata kusuluhisha migogoro inayotokana na tofauti ya tamaduni, kama inavyoelezwa hapa na hapa . Kwa hapa Marekani, ni jambo la kawaida kuwaita waandishi kuongelea vitabu vyao. Huwa ni fursa ya kukutana ana kwa ana na mwandishi, kuuliza masuali, na kununua vitabu. Kitu kimoja kinachowavutia sana wa-Marekani ni kununua kitabu wakati huo na kumpa mwandishi aandike jina lake na pia ujumbe kwenye nakala ya kitabu hicho. Wengine wananunua vitabu kadhaa, halafu wanapokuja kuwekewa sahihi, inabidi wakuambie uandike jina la nani, kwani wanawanunulia pia marafiki, watoto, au ndugu wengine. Ni mila ambayo iko ndani kabisa ya mioyo ya wa-Marekani. Wanaona furaha, kama in

Maonesho ya Vitabu Minneapolis, Oktoba 16

Image
Nimerejea jioni hii kutoka Minneapolis, kushiriki maonesho ya vitabu ambayo huandaliwa na jarida la Rain Taxi na kufanyika mara moja kwa mwaka. Kama kawaida, nilipeleka vitabu vyangu. Nilikuwa nimelipia meza ndogo. Lakini hii ilitosha kwa vitabu tu, bila maandishi mengine. Kwa vile idadi ya vitabu vyangu si ile ile ya mwaka jana au mwaka juzi, siku zijazo itanilazimu kulipia meza kubwa ili niweze kuweka maandishi mengine pia. Leo ninaleta hapa picha mbali mbali nilizopiga, kama mfano wa namna wa-Marekani wanavyojali suala la vitabu. Kama nilivyosema siku zilizopita, wa-Marekani wanafurika kwenye maonesho ya vitabu. Wanafika tangu asubuhi, milango ya ukumbi inapofunguliwa. Na siku nzima watu wanakuwa wengi katika ukumbi, wakienda na kuja. Wanafika watu wa kila rika: watoto, vijana, watu wazima, na waze, wanawake kwa wanaume. Pamoja na hali ya uchumi wa Marekani kuwa mbaya miaka hii, watu wanavichambua vitabu na kuvinunua. Wana dukuduku na hamu

Vitabu Vyangu Kwa Bei Nafuu

Lulu.com, ambako nachapisha vitabu vyangu, kumetokea tangazo linalotoa fursa kwa mwandishi kupunguza bei ya vitabu vyake akipenda. Kwa heshima ya wasomaji wangu, nimeamua kutumia fursa hiyo. Nimepunguza bei ya vitabu vyangu vyote kwa mwezi huu Oktoba. Vitabu hivi vimetajwa hapo kulia na pia hapa . Bofya sehemu ya kununulia, ili kuona punguzo hilo. Wale ambao hawanunui vitu mtandaoni na wanavihitaji vitabu hivi wanaweza kuwasiliana nami kwa barua pepe: info@africonexion.com. Siku ya mwisho ya punguzo hili ni Oktoba 31.

Chukua Chako Mapema

Pale CCM ilipoanzishwa, baadhi ya wa-Tanzania walianzisha minong'ono wakitafsiri CCM kama "Chukua Chako Mapema." Nilitaja jambo hilo katika makala fupi, "Jokes Play Social Role," ambayo ilichapishwa katika gazeti la Daily News (Tanzania) (Juni 16, 1987) ukurasa 4. Ni miaka mingi imepita, na ushahidi wa nini hasa maana ya CCM umeendelea kujitokeza. Tumsikilize katibu mkuu wa CCM:

Mahojiano Yangu "Kombolela Show"

Tarehe 2 Oktoba, nilihojiwa katika "Kombolela Show." Hiki ni kipindi cha redio kinachoendeshwa na Jaduong Metty, ambaye pia ni mmiliki wa blog ya Metty's Reflections . Kusikiliza mahojiano, bofya hapa au hapa

Mwalimu Nyerere Aliongelea Uozo Katika CCM

Mwalimu Nyerere aliongelea uozo katika CCM. Kwa mfano, wakati alipokuwa anajiandaa kung'atuka uenyekiti wa CCM, alizunguka nchi nzima akikagua uhai wa CCM. Wakati wa ziara hiyo, inaonekana Mwalimu alitatizwa na yale aliyoyaona. Aliwahi kusema kuwa kuna watu ndani ya CCM ambao hata mtihani juu ya Azimio la Arusha hawawezi kupasi. Mwaka 1993 Mwalimu alichapisha kitabu kiitwacho Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania (Harare: Zimbabwe Publishing House, 1993). Pamoja na mambo mengine katika kitabu hiki, Mwalimu alisema kuwa kuna kansa katika uongozi wa CCM. Nanukuu baadhi ya maneno yake: Chama cha Mapinduzi, kwa sababu ya uzito wa historia yake, hadhi ya jina lake, mfumo wa wavu wake, mazoea ya watu, na ubovu wa Vyama vya Upinzani, kinaweza kuchaguliwa na Watanzania, pamoja na kansa ya uongozi wake. Au watu wanaweza wakachoka, wakasema, "potelea mbali:" wakachagua Chama cho chote, ilimradi tu watokane na kansa ya uongozi wa CCM. Hainifurahishi kuyasema haya, lakini uhai wa Nc