Posts

Showing posts from 2021

Hitimisho la Trade with Africa Business Summit 2021

Image
Video hii ni ya hitimisho la mkutano uliofanyika tangu Mei 31 hadi Juni 4, uitwao "Trade With Africa Business Summit." Nimeshautajataja mkutano huu hapa. Kila mtu alishukuru kwa kuhudhiria kutokana na elimu kubwa na pana iliyopatikana katika mihadhara na mijadala. Mwaandaaji wa mkutano, Toyin Umesiri, alikuwa amenialika nikaongelee kitabu changu, "Africans and Americans: Embracing Cultural Differences." Kitabu kilitajwatajwa kwenye mkutano, hata katika video hii ya dakika za mwisho za mkutano. Mtoa mada Vera Moore, mmiliki wa kampuni ya Vera More Cosmetics, anaonekana mwishoni kabisa akiwa ameshika kitabu. Tulishangaa amekipataje upesi namna ile. Namshukuru Toyin kwa mwaliko wake. Ameniarifu kuwa ataendelea kunibebesha majukumu, nami niko tayari. Video zote za mkutano zinapatikana mtandaoni. Nikizingatia thamani ya elimu iliyomo, kulipia gharama iliyotajwa ni sawa na uwekezaji makini. Zinapatikana hapa: https://www.nazaru.trade/courses/5248326/content

Nina Wasomaji Butiama kwa Mwalimu Nyerere

Image
Sijawahi kufika Mwitongo, Butiama, lakini kitabu changu, ambacho ni kama nafsi yangu, kimefika. Pichani anaonekana mjukuu wa Mwalimu Nyerere akiwa anasoma kitabu hiki. Picha hii aliiweka mitandaoni akiwa ameambatisha ujumbe. Ninanukuu baadhi ya aliyosema. "My Dad gave me this book to read this morning, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences by Joseph Mbele. I just finished it. One lesson I learned is to respect, understand, and see the value in both cultures. I would highly recommend this book." .................. "My Dad gave me this book, he felt that it could be helpful for me, I’ve lived in the US since I was 7, I’ve made the decision to move back this year. There are many things which I still question. It will be a long learning process, this book has given me hope." .................. "Thank you for writing this book Professor Mbele. I’ve learned quite a lot from reading it but I’ve also grasped a better understanding of many things which

Ms. Vera Moore - Mdau Mpya wa Kitabu Changu

Image
Wiki hii nzima, nimekuwa nikihudhuria mkutano mkuu uitwao Trade With Africa Business Summit. Mkutano umejumlisha wafanya biashara, wanadiplomasia, na wajasiriamali, na wengine kutoka nchi mbali mbali. Mwandaaji wa mkutano, Toyin Umesiri kutoka Nigeria, mjasiriamali na mhamasishaji wa biashara baina ya Afrika na Marekani, alikuwa amenialika kuongelea kitabu changu, "Africans and Americans: Embracing Cultural Differences." Alikipigia debe mkutanoni, na kilitajwa mara kwa mara. Mjumbe mmoja, Vera Moore, mfanyabiashara maarufu wa vipodozi, alitusisimua alipokuwa akiongea, kwa kutuonyesha nakala ya kitabu akisema ameshanunua. Nilishangaa alivyokinunua haraka namna ile. Nafurahi kuwa na mdau maarufu huyu. Wengine wanakuja.

Nimealikwa Kuongelea Kitabu Changu

Image
Nimealikwa kuongelea kitabu changu,  Africans and Americans: Embracing Cultural Differences , katika mkutano mkubwa ujulikanao kama  Trade With Africa Summit  utakaofanyika kutumia mtandao tarehe 31 Mei hadi 4 Juni mwaka huu. Mkutano huu hufanyika mara moja kwa mwaaka. Aliniaalika ni mwanaadji waa mkutano  Toyin Umesiri , mjasiriamali na mhamasishaji maarufu wa biashara baina ya Afrika na nchi zingine, hasa Marekani. Aliamua kunialika baada ya kusoma kitabu changu kisha akanialika kwenye kipindi chake cha Nazaru TV  na kufanya  mahojiano nami . Kwa miezi ya karibuni, mimi mwenyewe nimeanza kujibidisha kutafiti namna tofauti za tamaduni zinavyoathiri biashara. Mawazo yangu tayari yanaonekana katika kitabu changu, lakini ninayaendeleza na kuyafafanua. Mfano ya juhudi zangu ni  makala katika Medium  na  maongezi katika YouTube .

Kitabu Kimetua Abuja, Nigeria

Image
Mwezi Machi 2021 umeisha vizuri kwangu. Kitabu changu,  Africans and Americans: Embracing Cultural Differences , kimetua Nigeria. Nilikuwa nimempelekea Jennifer Chinyelu Ikeaba-Obiasor, aonekanaye pichani, ambaye anaishi Abuja. Huenda hii ni nakala ya kwanza kuingia Nigeria. Jennifer alisoma kitabu akaandika maoni kwa nyakati mbali mbali: Ni kitabu murua chenyee upeo utakaowasidia waAfrika na waMarekani. Uzoefu wangu unaendana na karibu kila kipengele kitabuni humu. Na kitawafungua macho watu wa tamaduni zote mbili. Ninakipendekeza kitabu hiki kwa kila mmoja, akisome kwa sababu kitamgusa. Jennifer nami tulikutana mtandaoni wiki chache zilizopita tukiwa wafuasi wa  Toyin Umesiri , mhamasishaji maarufu wa biashara baina ya Afrika na Marekani, ambaye aliwahi kufanya mahojiano nami kuhusu  kitabu changu  na kuhusu athari za tamaduni katika biashara baina ya waAfrika na waMarekani. Jennifer ni mjasiriamali, mwanzishi na mkurugenzi mkuu wa  Chiblenders Green . Katika juhudi za kueneza shughu

Profesa Mkatoliki Anayefundisha Uislam Nchini Marekani na Mtazamo Kuhusu...

Image

Kipigo cha Mbwa Koko na Tofauti za Tamaduni

Image

WAJIBU NA MAADILI YA UALIMU

Image

Prof Joseph Mbele akihojiwa na Hassan Saudin

Image

Africonexion Yashiriki KAN Festival

Image
Kuanzia tarehe 28 hadi 30 Januari hii, kwenye kituo cha MS TCDC, Arusha, kunafanyika tamasha liitwalo KAN Festival . Kwa kuwa sikuweza kwenda kuhudhuria, niliwasiliana na ndugu Thomas Ratsim wa Arusha akaniwakilishe. Mwaka jana aliniwakilisha pia, na ninatumia jina la Africonexion: Cultural Consultants, ambayo ni kampuni ndogo niliyosajili mwaka 2002 hapa katika jimbo la Minnesota, Marekani.  Shughuli za Africonexion: Cultural Consultants ni kutafiti, kuandika, na kuelimisha kuhusu za tofauti za tamaduni katika dunia ya utandawazi wa leo. Wateja ni wa aina nyingi, kama vile waMarekani wanaokwenda Afrika na waAfrika wanaofika Marekani, taasisi, makampuni, jumuia na vyuo. Lengo ni kuwawezesha watu kuelewa changamoto za tofauti za tamaduni ili kuboresha mahusiano na ufanisi katika shughuli. Matamasha ni fursa ya kutangaza shughuli za Africonexion: Cultural Consultants , ikiwemo kwa njia ya vitabu na maongezi na watu wanaokuja kwenye meza yetu, na pia ni fursa za kujifunza kutoka kwa wa

Kitabu Kimefika Somalia

Image
 Juzi tarehe 25, mama mmoja mSomali aishiye mjini Faribault hapa katika jimbo la Minnesota alinipigia simu. Nilikutana naye mara ya kwanza mwaka jana tamasha la kimataifa Faribault , nikampa nakala ya kitabu changu, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences. Alivyonipigia jana alisema kuwa alikuwa amerejea kutoka safarini Somalia. Baada ya maongezi na fupi ya simu, aliniandikia ujumbe huu: J oseph, I forgot to tell you that I took your book to Somalia. The people loved reading your book. Yaani, Joseph, nilisahau kukuambia kuwa nilienda na kitabu chako Somalia. Watu walifurahia kusoma kitabu chako. Nafurahi kuona jinsi kitabu hiki kinavyokubalika na waAfrika wa kila taifa, jinsia, dini, na kadhalika. Kuna vipengele fulani katika kitabu hiki ambavyo ninaposoma, ninapata wasi wasi kuwa huenda niliandika bila kuwaza kuwa kuna waIslamu Afrika. Ajabu ni kuwa waIslamu wenyewe hawajawahi kukwazika. Mmoja kati ya wasomaji wa kitabu hiki wa mwanzo kabisa alikuwa mama muIslamu msomi

Africans and Americans - Embracing Cultural Differences - With Guest Pro...

Image

Msomaji Wangu Kutoka Somalia

Image
  Huyu ni Salah Habib-Jama Mohamed kutoka Somalia, akiwa na kitabu changu  Africans and Americans: Embracing Cultural Differences . Alihitimu shahada ya kwanza hapa katika  Chuo cha St. Olaf . Salah aliniambia katikaa maongezi ya simu kuwa aliwahi kuwa na kitabu hiki akakisoma.  Alikipenda sana, ila mtu alikiazima na sasa haijulikani kiko wapi. Nilicheka niliposikia hivyo, kwani nimewasikia waMarekani nao wakilaalamika kuwa nakala zao ziliazimwa na sasa hazijulikani ziliko, kwani waazimaji huwaazimisha wengine, na hivi kitabu kutoweka. Katika ukurasa wake wa Facebook, Salah aliandika kuhusu kitabu hiki kwamba, "It is a great book and a must read allowing us to understand each other better with humor," yaani ni kitabu bora sana na muhimu kusomwa kwa namna kinavyotuwezesha kuelewana huku kikituchekesha. Nafurahi kuwa kitabu kinapendwa na wote ambao wamekisoma. Nafarijika kuwa kinapendwa na waAfrika kutoka bara lote, wanawake kwa wanaume, wa makabila na dini mbali mbali. Nafarij