Kitabu "Matengo Folktales" Chatajwa Katika "Jeopardy."
Tarehe 23 Novemba, 2017, nitaikumbuka daima. Kwanza, ilikuwa ni sikukuu ya "Thanksgiving" ambayo ni maarufu hapa Marekani. Jambo la pili liliofanya targhe 23 iwe muhimu kwangu ni kuwa jioni ya siku hiyo, katika kipindi maarufu cha televisheni kiitwacho "Jeopardy," kitabu changu kiitwacho Matengo Folktales kilitajwa. "Jeopardy" ni mchezo kama chemsha bongo. Watu hushindana kujibu masuali ambayo mwendesha kipindi huwauliza, na wanapotoa jibu sahihi hupata fedha. Suali lililoulizwa lilikuwa kuhusu mhusika katika hadithi. Nilikifahamu kipindi hiki kijuujuu. Lakini baada ya kitabu kutajwa, nimeona wa-Marekani wanaonifahamu wanavyosisimka na kunipongeza. Hata hapa chuoni St. Olaf habari imezagaa hadi kwa wakuu wa chuo. Mkuu wa idara yangu ya ki-Ingereza ameandika ujumbe kwetu waalimu na wanafunzi: Congratulations to Joseph Mbele for an honor that few of us will ever achieve--being mentioned in a clue on Jeopardy! See the image below, referencing Joseph